Wangapi mko tayari kuchangia gharama ya kesi ya kuomba kurekebishwa Sheria ya Mikopo?

Hatupo tayari kuchangia gharama zozote.

Kwani wabunge kazi yao nini? Si kutunga na kurekebisha sheria? Nenda kawakinaishe wabadili sheria kama unaona una hoja ya maana.

Usituletee mambo ya michango hapa. Tuliyonayo tumboni inatutosha.
Kwa heshima zote dada yangu naomba usiwasemee watu, acha wanao hisi kuguswa wachangie.
Uzuri mdau kaweka na utambulisho wake hivyo atafuatiliwa vizuri kusiwe na ulaghai.
 
Kwa heshima zote dada yangu naomba usiwasemee watu, acha wanao hisi kuguswa wachangie.
Uzuri mdau kaweka na utambulisho wake hivyo atafuatiliwa vizuri kusiwe na ulaghai.
Nawasemea wengi tu, wewe kama unachangia mimi hainihusu. Inayonihusu ni wasio changia tu.

Watanzania hatuendelei kwa michango hii. Harusi michango, kifo michango, sasa tena mambo ya mtu haipendi sheria au kanuni fulani michango!

Khaa! Inahusu nini? Ndiyo maana watu wanachangia wake na waume za watu kama hawana akili vizuri, si walichangia.
 
Ngoja nikukumbushe hili sakata lilipoanza nakuleta huu ujinga naimani mh rais ajui kilichopo nyuma ya pazia kuna hili sakata


Baada ya hili sakata wakopeshaji wa kadi inchi nzima waliogopa serikali iliwakalia kooni kwa sababu walikuwa wanafanya biashara kinyume na sheria

Baada ya hapo hawa maboss inchi nzima wakaitana Dodoma, wakatafuta hotel nzuri wakachanga pesa nzuri kila tajiri wakawaita viongozi wa serikalini wakiomba sheria hii itungwe viongozi wenye dhamana wakaona hapana haiwezekani

Basi hawa matajiri wakaitana tena wakachangishana pesa nyingi sana wakatumia watu kwenda serikalini wanaanza kucheza na wizara ya feza kuwahonga ili waweze kutungiwa hii sheria wamehonga pesa nyingi sana yani wamehonga kupita maelezo lengo sheri a iwepo iwape Uhuru wakuendesha biashara zao ambazo zipo kinyumbe na utaratibu za inchi na ni zakihujumu uchumi

Kwaiyo hiyo sheria imetungwa baada ya kundi furani kuhonga pesa ili wakafanye mambo yao uko mitaani

Ajabu vyombo vya usalama vipo unajiuliza hawajui haya mambo yani kiufupi viongozi wa serikali wamekuwa corrupted na hili genge la wakopeshaji wa mitaani maana jamaa ni wizi wanawanyonya sana watu

Ngoja ipo siku takuja na Uzi mzima wamehonga bei gani mpaka wametunguiwa sheria hii ya hivyo na inayoenda angamiza taifa
Kwa nini unawadanganya wadau? Mm kwenye hicho kikao nilikuwepo lakn mambo ya namna hii hayakufanyika kabisa!
 
Nimefurahi kuona kuna wadau mnaojali kuhusu hili suala.

Sasa naomba wale wote ambao mko tayari kulivalia njuga mnitumie namba zenu za simu kwa INBOX
 
Back
Top Bottom