The Intelligent
JF-Expert Member
- Dec 27, 2013
- 2,459
- 824
Sera ya elimu ya bure ndio mpango unaofanya kiwango cha elimu kishuke vile vile kuwapotezea muda vijana kwa kukaa darasani na mwisho wake kukosa ajira baada ya kuhitimu.
Hawa walitakiwa kuboresha elimu ya ufundi na stadi za kazi ili iwasaidie vijana wakiwa bado wapo mashuleni, hii itamfanya kijana awe na ujuzi mapema na sio kumaliza kudato cha nne na kuishia kukaa nyumbani eti kwa kuwa hana credit za kumfanya aendelee na elimu au sababu ya kukosa fedha.
Tumeona mpango ya BRN, umerundika vijana shuleni matokeo yake tumeona vijana wakirudi nyumbani baada ya kumaliza masomo yao na kuhitimisha safari yao kitaaluma kwa kushinda vijiweni huku wengine wakifanya shughuli ambazo hata wasingeenda shule wangeweza kuzifanya.