Wanazuoni wasikitishwa na sera za mgombea urais

Wanazuoni wasikitishwa na sera za mgombea urais

WANAZUONI WASIKITISHWA NA SERA ZA MGOMBEA URAIS

Hatimaye mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dr John Pombe Magufuli amezidi kutikisa ngome ya wanazuoni hususani ktka ajenda zake za elimu bure kuanzia darasa la awali hadi form six.

Awali kulikuwa na mijadala kadhawakadha kama swala hilo anaweza kutekeleza kiurahisi lkni kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, Wanazuoni hao baada ya kupitia tafiti mbalimbali kutoka nchi wanachama wa ECOWAS, pamoja na EU.

Kuna baadhi ya nchi zilizfanikiwa sana katika sekta ya elimu hivo kwa nchi kama Tanzania kwa kuanzisha sera mpya ya elimu pamoja na elimu bure itakuwa ni chachu ya maendeleo.

Aidha Wanazuoni hao wamezidi kupinga vikali hoja ya elimu bure hadi chuo kikuu, kwa mujibu wa tafiti zao hata nchi zilizoendelea kiviwanda hususani Japani, China, Ujerumani, Marekani na hata Uingereza pamoja na kuwa na uchumi imara bado nchi hizo wazijafikia hatua ya kutoa elimu bure hadi chuo kikuu.

Swali itawezekanaje kwa nchi changa kama Tanzania inayotegemea misaada kutoka nchi hizo? Kwa mujibu wa wanazuoni hao ni wakati stahiki kwa Tanzania kupata kiongozi mwenye sera zinazoweza kutekelezeka na kwa wakati.
Lowassa is telling lies. Hafai kuwa Kiongozi wa nchi.
 
Mapenzi mabaya, mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo, usimkabidhi mtu hatma ya maisha yako kwakua unampenda mtazame ,umchunguze, jiririshishe je ataweza, kwa msaada kidogo nikupe mwongozo kwamba huyo unayempenda alishawahi fanya nn kukusaidia wewe, alishafanya nn kulisaidia taifa, mwenye historia ya kufanya vizuri, hahitaji king'amuzi kuionyesha dunia kuwa anaweza
 
Mapenzi mabaya, mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo, usimkabidhi mtu hatma ya maisha yako kwakua unampenda mtazame ,umchunguze, jiririshishe je ataweza, kwa msaada kidogo nikupe mwongozo kwamba huyo unayempenda alishawahi fanya nn kukusaidia wewe, alishafanya nn kulisaidia taifa, mwenye historia ya kufanya vizuri, hahitaji king'amuzi kuionyesha dunia kuwa anaweza

Kila mtu ana haki ya kuchagua kwa namna yoyote ile iwe kwa ushabiki,kupenda,mkumbo,maslahi binafsi,kushawishiwa au kumtambua kiongozi anayefaa.Na hata kwa ukabila kama watu wengi wa kanda yetu ya ziwa wanavyodai.Kikubwa watu wawe huru kuchagua viongozi wanaowataka na wasishurutishwe na kulazimishwa kwa kupitia pro-magandaz..
 
Zipo nchi ambazo bado zinatoa elimu ya chuo kikuu bila ada. Kwa mfano vyuo vikuu vingi vya umma vya Ujerumani vinatoa shahada ya kwanza bila ada. Hii hata hivyo inategemea jimbo alipo mjerumani husika. Baadhi ya majimbo yanadai ada.

Kwa Norway, Sweden na Dermark wao akili yako tu shahada ya kwanza unaizoa. Hakuna ada. Na hizo ni kati ya nchi ambazo zinafanya vizuri sana katika viwango vya elimu duniani.

Hapa kwetu pia inawezekana. Tukiacha matumizi (matanuzi ) ya kipuuzi tuna rasilimali za kutosha kutoa elimu bure. Hili halifanyiki kwa kupenda, lakini kwa sababu tumekubaliana kuwa ujinga ni adui wakati pia tukijua kuwa adui mwingine yaani umasikini bado ametamalaki miongoni mwa sehemu kubwa ya watanzania. Kwa wale ambao walikuwepo, watakumbuka jinsi kila kitu kilivyotumika umshughulikia adui Idd Amin alipovamia sehemu ya nchi yetu. Mtindo huohuo ukitumika elimu bure inawezekana kabisa. Siku zilizopita walisomeshwa bure, si watoto tu bali hata watu wazima. Hiyo ndiyo namna ya kumtwanga adui ujinga.

Kinyume cha hapo ni porojo. Maskini gani Tanzania hii anaweza kumsomesha mwanae shuleni siku hizi. Ndio maana wazazi wengine wanawashauri wafeli mtihani darasa la saba ili kuwaondolea gharama. Maana hata baada ya kugharimia mpaka chuo kikuu hakuna uhakika wa kupata ajira.

Tumedhani elimu ni gharama tukathubutu kujaribu ujinga, weeh!
 
Back
Top Bottom