Wanazuoni wasikitishwa na sera za mgombea urais

Wanazuoni wasikitishwa na sera za mgombea urais

Nchi nyingi zilizo endelea hawana swala hilo ukilinganisha na uchumi wao vipi kwetu sisi?
 
Kweli wanazuoni wetu mnastahili pongezi kubwa sana kwa hoja hii.
 
Ngoja niulize swali. Wanafunzi wa elimu ya juu kwa sasa wanasoma kwa mikopo kutoka board ya mikopo. Kwani hizo fedha zinatoka wapi? Jibu ni serikalini. Swali la pili hivi ni kweli hiyo mikopo inarejeshwa? Jibu linaweza kuwa ndiyo ama hapana. Kwa kiasi kikubwa mikopo hiyo hairejeshwi kwa kuwa wengi wa wahitimu hawapati ajira mara wamalizapo masomo yao. Je serilikali.imeyumba kwa kutorudisha hiyo mikopo? Angalau hatujasikia hata serikali yenyewe ikisistiza kurejeshwa kwa hiyo mikopo. Hiyo maana yake elimu bure vyuo vikuu inawezekana kabisa. Wakwepa kodi wote Ukawa wakiingia Ikulu hawatapata nafasi hiyo. Wananchi walipe kodi. Misamaha ya kodi ipunguzwe kabisa. Elimu bure inawezekana.
 
hawa wanazuoni wa wp? ela zinazoibwa kwa mwaka hazitoshi kuwasomesha mpaka chuo kikuu bure? kama makampuni ya umeme yanalamba milioni mia na hamsini kila siku iweje tushindwe kusomesha? ni lini hao wanaojiita wanazuoni watawaza nje ya box? gadafi angewaza kutegemea wazungu kama sisi asingefika mbali yeye alitumia kijitabu chake binafsi greenbook badala ya katiba za kizungu na akaweza sasa nyie wanazuoni mnaimani kama wazungu wameshindwa na sisi hatuwezi? tukitegemea watu kama nyie tutaendelea kuwa maskini daima.
 
Hata elimu ya bure kuanzia awali mpaka kidato cha 4 mulikuwa mnasema haiwezekani,leo mnajifanya kuwa inawezekana,kuiamini CCM ni kama kumwamini shetani.

tatizo la wanazuo wetu hawaamini kitu kikisemwa na upinzani isipokuwa ccm. hii ni shida..
 
Tatizo liko wapi, hongera sana mwandishi hao wengine walete fact zao na sio kupinga tu.Nchi za uraya ndizo zinazotoa misaada kwetu sisi na hazitoi elimu bure pamoja na uchumi wao kuwa juu leo wewe mwenye matatizo tele na idadi kubwa ya wanafunzi utaweza vipi, kwa uchumi upi tulionao kwa sasa?

tatizo la wanazuoni wetu hawajalisaidia taifa letu.wao wanaamini taifa letu litaendelea kwa kutegemea misaada toka ulaya...elimu bure inawezekana sana tu kama tukijipanga vizuri. kwa mfano kupunguza matumizi yasiyo yalazima serikalini...
 
Hao wanazuoni ni wazembe hawajatembelea nchi ya Algeria tu hapo ambapo elimu kuanzia shule ya msingi hadi chuoni ni bure, na kila mkoa unajitegemea kwa kuwa na chuo chake... Elimu bure mpaka chuoni si nadharia, inawezekana...
 
Ngoja niulize swali. Wanafunzi wa elimu ya juu kwa sasa wanasoma kwa mikopo kutoka board ya mikopo. Kwani hizo fedha zinatoka wapi? Jibu ni serikalini. Swali la pili hivi ni kweli hiyo mikopo inarejeshwa? Jibu linaweza kuwa ndiyo ama hapana. Kwa kiasi kikubwa mikopo hiyo hairejeshwi kwa kuwa wengi wa wahitimu hawapati ajira mara wamalizapo masomo yao. Je serilikali.imeyumba kwa kutorudisha hiyo mikopo? Angalau hatujasikia hata serikali yenyewe ikisistiza kurejeshwa kwa hiyo mikopo. Hiyo maana yake elimu bure vyuo vikuu inawezekana kabisa. Wakwepa kodi wote Ukawa wakiingia Ikulu hawatapata nafasi hiyo. Wananchi walipe kodi. Misamaha ya kodi ipunguzwe kabisa. Elimu bure inawezekana.

nakushukuru sana. pia ni muhumu kubana matumizi serikalini...
 
Acha kupotosha. Si Dk. Magufuli wala Lowassa aliyesema atatoa elimu bure kuanzia elimu ya awali. Wote wamesema elimu bure itaanza kutolewa kwa elimu ya msingi. Pili, Magufuli kasema atatoa elimu ya msingi hadi kidato cha nne, bure; na si kidato cha sita kama unavyoongopa hapa. Lowassa ndo kasema atatoa elimu bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu. Uwe makini unapoleta taarifa hapa JF.

Upo sahihi kabisa, Watu wanakurupyuuka tu, sore(kurupuka tu) na threa za ajabu ajabu! Unasema wanazuomi wamemsikia Makufuli wa wapi? Jana tu tumemsikia hapa anasema mpaka KIDATO CHA NNE! We na wenzako kaa na mjadili kabla ya luja hapa
Sawa sio Ombi
 
Sawa?. Sio ombi.
 
Kuna kipindi cha kampeni zilizopita CCM ilisema elimu BURE haiwezekani hadi secondary, Leo mbona mwasema yawezekana
 
Kama utashi wa kisiasa utakuwepo kwa viongozi wetu na kudhibiti mianya ya ufisadi/rushwa, utoaji wa elimu ya bure unawezekana kwa kutumia raslimali zetu!
 
hao wanazuoni wako wanaonekana hawajui kufikiria nje ya sanduku..wamekariri
 
WANAZUONI WASIKITISHWA NA SERA ZA MGOMBEA URAIS

Hatimaye mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dr John Pombe Magufuli amezidi kutikisa ngome ya wanazuoni hususani ktka ajenda zake za elimu bure kuanzia darasa la awali hadi form six. Awali kulikuwa na mijadala kadhawakadha kama swala hilo anaweza kutekeleza kiurahisi lkni kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, wanazuoni hao baada ya kupitia tafiti mbalimbali kutoka nchi wanachama wa ECOWAS, pamoja na EU. KUNA BAADHI YA NCHI ...ZILIZOFANIKIWA SANA ktka sekta ya elimu hivo kwa nchi kama Tanzania kwa kuanzisha sera mpya ya elimu pamoja na elimu bure itakuwa ni chachu ya maendeleo.
Aidha wanazuoni hao wamezidi kupinga vikali hoja ya elimu bure hadi chuo kikuu, kwa mujibu wa tafiti zao hata nchi zilizoendelea kiviwanda hususani Japani, China, Ujerumani Marekani na Hata Uingereza pamoja na kuwa na uchumi imara bado nchi hizo wazijafikia hatua ya kutoa elimu bure hadi chuo kikuu, swali itawezekanaje kwa nchi changa kama Tanzania inayotegemea misaada kutoka nchi hizo?.
Kwa mujibu wa wanazuoni hao ni wakati stahiki kwa Tanzania kupata kiongozi mwenye sera zinazoweza kutekelezeka na kwa wakati.

Kwa kumbukumbu yangu siku ya uzinduzi wa CCM waliahidi kutoa elimu bure kuanzia Primary mpaka form four Tu...
 
Kama utafiti umefanyika kwa manufaa ya umma kwanini ufikie mikononi mwako mtoa post we ni nani kwenye serikali hii acha unafki wa hoja haturudi nyuma mtasema sana mwaka huu kuliko ,2010.
 
Sera zenu za kijinga zimeanza tena! Hata kwa Slaa mlisema hakuna nchi yoyote inayoweza kutoa elimu bure hadi kidato cha nne! Mmekalia siasa uchwara na za hovyohovyo!!
 
Hao wanazuoni ni wazembe hawajatembelea nchi ya Algeria tu hapo ambapo elimu kuanzia shule ya msingi hadi chuoni ni bure, na kila mkoa unajitegemea kwa kuwa na chuo chake... Elimu bure mpaka chuoni si nadharia, inawezekana...
Huyu naye hatofautishi chuo na chuo kikuu
 
Back
Top Bottom