Wanazuoni wasikitishwa na sera za mgombea urais

Wanazuoni wasikitishwa na sera za mgombea urais

Robethn

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
2,103
Reaction score
354
WANAZUONI WASIKITISHWA NA SERA ZA MGOMBEA URAIS

Hatimaye mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dr John Pombe Magufuli amezidi kutikisa ngome ya wanazuoni hususani ktka ajenda zake za elimu bure kuanzia darasa la awali hadi form six.

Awali kulikuwa na mijadala kadhawakadha kama swala hilo anaweza kutekeleza kiurahisi lkni kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, Wanazuoni hao baada ya kupitia tafiti mbalimbali kutoka nchi wanachama wa ECOWAS, pamoja na EU.

Kuna baadhi ya nchi zilizfanikiwa sana katika sekta ya elimu hivo kwa nchi kama Tanzania kwa kuanzisha sera mpya ya elimu pamoja na elimu bure itakuwa ni chachu ya maendeleo.

Aidha Wanazuoni hao wamezidi kupinga vikali hoja ya elimu bure hadi chuo kikuu, kwa mujibu wa tafiti zao hata nchi zilizoendelea kiviwanda hususani Japani, China, Ujerumani, Marekani na hata Uingereza pamoja na kuwa na uchumi imara bado nchi hizo wazijafikia hatua ya kutoa elimu bure hadi chuo kikuu.

Swali itawezekanaje kwa nchi changa kama Tanzania inayotegemea misaada kutoka nchi hizo? Kwa mujibu wa wanazuoni hao ni wakati stahiki kwa Tanzania kupata kiongozi mwenye sera zinazoweza kutekelezeka na kwa wakati.
 
WANAZUONI WASIKITISHWA NA SERA ZA MGOMBEA URAIS

Hatimaye mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dr John Pombe Magufuli amezidi kutikisa ngome ya wanazuoni hususani ktka ajenda zake za elimu bure kuanzia darasa la awali hadi form six.

Awali kulikuwa na mijadala kadhawakadha kama swala hilo anaweza kutekeleza kiurahisi lkni kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, wanazuoni hao baada ya kupitia tafiti mbalimbali kutoka nchi wanachama wa ECOWAS, pamoja na EU.

Kuna baadhi ya nchi zilizfanikiwa sana katika sekta ya elimu hivo kwa nchi kama Tanzania kwa kuanzisha sera mpya ya elimu pamoja na elimu bure itakuwa ni chachu ya maendeleo.

Aidha wanazuoni hao wamezidi kupinga vikali hoja ya elimu bure hadi chuo kikuu, kwa mujibu wa tafiti zao hata nchi zilizoendelea kiviwanda hususani Japani, China, Ujerumani, Marekani na hata Uingereza pamoja na kuwa na uchumi imara bado nchi hizo wazijafikia hatua ya kutoa elimu bure hadi chuo kikuu.

Swali itawezekanaje kwa nchi changa kama Tanzania inayotegemea misaada kutoka nchi hizo? Kwa mujibu wa wanazuoni hao ni wakati stahiki kwa Tanzania kupata kiongozi mwenye sera zinazoweza kutekelezeka na kwa wakati.
 
Anayesema 50ml kila kijiji yy mnaona anaweza hv unajua kuna vijj vingap tanznia bara na visiwani
Heb jiulize tu ni madenu mangapi mpaka ss serikali inadaiwaaa na hawajui watalaipa nn miradi mingi imecmama take note mkuu
 
Hongereni sana Wanazuoni wetu kwa kutuweka wazi mambo hayo mtambuka kwa taifa letu. Kamwe hatudanganyiki.
 
Tunapaswa kutafakari kwa kina sera za wagombea na sio kukurupuka tu. Magufuli sera zake zinatekelezeka.
 
Acha kupotosha. Si Dk. Magufuli wala Lowassa aliyesema atatoa elimu bure kuanzia elimu ya awali. Wote wamesema elimu bure itaanza kutolewa kwa elimu ya msingi. Pili, Magufuli kasema atatoa elimu ya msingi hadi kidato cha nne, bure; na si kidato cha sita kama unavyoongopa hapa. Lowassa ndo kasema atatoa elimu bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu. Uwe makini unapoleta taarifa hapa JF.
 
Zile fedha za escrow na uswiss zisingeweza kusomesha watoto wetu mpaka chuo kikuu?. Badala yake unatoa mifano china , usa,
 
Asitoe mifano ya usa na china nchi hizo watu hawakuvumilii ufanye ufisadi wa escrow au ule wa mabilioni ya uswisi
 
elimu bure inawezekana kwa ngazi zote. tatizo tu viongozi wetu ni watumbuaji mno...
 
wanazuoni wa Tanzania au wa wapi... nakuambia watanzania waliofanikisha kupata milo mitatu hawajali watoto kutoka familia maskini.

Kama mtu ashasema elimu Elimu elimu. sector nyingine zitapewa vipaombele lakini elimu kwanza...

tofaut na anasema sio bure chuo, maana ake atakopesha au sio. Source ya pesa wanayokopeshwa wanfunzi ni wapi au ni ipi.


Mabilioni yenu kule uswisi yatatusomesha bure.

kule chuo kikuu wakihitimu elimu ya hujasikia mali wakitoka moja kwa moja watajiajiri mashambani na sector mbalimbali, kodi hata ya 500 kwa population ya watanzania niliona ni pesa mingi,

mabadiliko yana maana ndefu, na ni lazima
 
Tatizo la vijana wa FU movement nyie mnasukumwa tu hoja hamna, wenzenu chadema asilia wako kimya maana wanajitambua palipo na ukweli uongo hujitenga. Jitambueni mapema.
 
Hata elimu ya bure kuanzia awali mpaka kidato cha 4 mulikuwa mnasema haiwezekani,leo mnajifanya kuwa inawezekana,kuiamini CCM ni kama kumwamini shetani.
 
Tatizo liko wapi, hongera sana mwandishi hao wengine walete fact zao na sio kupinga tu.Nchi za uraya ndizo zinazotoa misaada kwetu sisi na hazitoi elimu bure pamoja na uchumi wao kuwa juu leo wewe mwenye matatizo tele na idadi kubwa ya wanafunzi utaweza vipi, kwa uchumi upi tulionao kwa sasa?
 
Hongera sana mwandishi na wanazuoni wetu kwa kutuweka sawa.
 
Back
Top Bottom