Wanayoyasema juu ya haki

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,129
2,003
Habari wanajamii,
Haki ni kitendawili ambacho kimewaandama wanafalsafa wakubwa waliowahi kutembea kwenye uso wa dunia hii tangia enzi hizo watu walipoanza kufikirisha mbongo zao huko UGIRIKI.
Kwa kufwata mtiririko ntaeleza yaliyowahi semwa juu ya haki.

Ntaanza na plato yeye alifika hitimisho ya kuwa hapa duniani hapatatokea HAKI mpaka pale wanafalsafa watakapokuwa watawala. Alisema haya kutokana na misingi ya kwamba watu wengi ikiwemo na watawala wanakuwa wanakosa hali ya kuchunguza matendo yao na wengi wanafanya mambo kwa kuigiliza.

Hapa nakuja na mwanafalsafa wa uzito wa juu anayekwenda kwa jina la Emanuel Kant huyu mwanafalsafa alipiga pini juu ya fikra za mwanadamu kwa kuonyesha ukingo wa fikra chanya kwa mwanadamu.

Yeye katika kujibizana na mbongo yake alifika hitimisho ya kwamba binadamu anajua HAKI kwa sababu kuna chanzo chake ambacho mwanadamu anaweza kukitambua kwa jina moja la MUNGU. Hivyo basi Kant anasema ya kwamba tunafahamu juu ya haki kwasababu Mungu anatutaka tutende haki. Kama Mungu asingekuwepo basi kusingekuwa na haki.

Kutoka kwa huyo tunakuja kwa mwanafalsafa wa pepo za kali za Mlimani huyu ni Friedrich Nietzsche huyu jamaa alikuwa na wasiwasi juu ya binadamu kujiafanya tuanijua haki alikuwa na wasiwasi kutokana na falsafa za uwili ya kwamba tunapenda haki kwasababu kiasili sisi ni waovu na hivyo kupelekea kujua tofauti ya uovu/ kuangamiza ambayo ni HAKI.

Napenda kufunga huu mjadala na mwanafalsafa anayekwenda kwa jina la albert Kamusi ambaye yeye kwa mtizamo wake aliona ya kwamba haki inatokana na akili zetu mwanadamu, inatokana na utendaji kazi wa akili zetu , na pia inatokana na muundo wa akili zetu sisi wanadamu Lakini cha kusikitisha ni kwamba katika ulimwengu haki hakuna hapo ndo shida za kushangaa hii haki ni kitu gani.

Hao watajwa ni baathi tu ya waliojaribu kusema juu ya haki. Haki ni kitendawili, unafikiri kwa nini tunapenda haki sisi wanadamu.
 
Back
Top Bottom