Wanawake wenye ndevu na kisimati cha pesa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Salaam nyingi sana wanaJF.

Neno 'kismati' limekuwa likitumika kuashia mtu kuwa na bahati nzuri au zali kwa wenzetu vijana huku mtaani.

Wanawake wenye ndevu ni kama wana kismati.Mwanaume ukishakuwa na mahusiano na mwanamke mwenye ndevu (hata kama chache),unakuwa mtu wa bahati sana,mambo yako hunyooka vizuri sana.Unaondokana na mabalaa ya ajabu ajabu. Ukipanga plan zako,zinakwenda vizuri kabisa (hata kama si kwa 100%).Kazini mambo yanakunyookea, biashara inakaa safi, marafiki unakuwa nao wazuri sana na pia unakuwa mtu wa amani sana saa zote.

Sasa ukijaribu kumuacha au kumnyanyasa pasipo sababu ya msingi, unapata mamikosi, mabalaa kila kona na unakuwa mtu wa stress muda wote.Na kazini unapata matatizo au kama unatafuta kazi ,hauipati kabisa huku yeye mambo yakimnyookea.Ni kama tu baraka zinatoka kwako halafu zinahamia kwake au kwa mwanaume atakayemuoa.

Waliooa au wenye mahusiano na wanawake wenye ndevu watakubaliana na mm. Hata kama huna hela nyingi lakini unakuwa na life fulan tamu sana ndani ya nyumba.

Ukiwa na mwanamke mwenye ndevu jivunie sana, ni bahati kubwa.Ni asali.

Wanawake wenye ndevu kismati chao hutokea wapi?Mambo ya imani nini au ni kizazi kingine?
 
Naomba kuulza kitu, hv Jacqueline mangi ana ndevu, wena sepetu ana ndevu, na mbona kuna wauza vtumbua na maandaz kina mama lishe wengi wana ndevu na maisha yao n ya kawaida?
 
Mimi ninazo jamani unachoongea ni kweli kabisa, nina ushahidi mpaka inafika kipindi kuachana na mtu inakuwa shida, analia kabisa kwamba mambo yake hayaendi asipokuwa na wewe au mkigombana, wengine wamekuwa ving'ang'anizi mpaka inakuwa kero, sio wanaume tu hata kwenye mambo kama ya biashara nk. mara nyingi huwa nafanya utafiti nagundua mambo mengi mbalimbali, am not sure kama yanahusika moja kwa moja na mimi kuwa na ndefu but what i see there must be a strong connection.
 
Tatizo hamjamuelew vizuri mleta mada ..
Hajamaanisha mwanamke ukiwa na ndevu au mwanaumwe ukiwa na mwanamke mwenye ndevu unakuwa Tajiri anachomaanisha ni kwamba katika sekta yako u akuwa na bahati..
Unaweza kuwa mpika vitumbua kwenye hiyohiyo biahsra ya vitumbua ukawa na bahati kuliko wauzaji wengine..
 
Naomba kuulza kitu, hv Jacqueline mangi ana ndevu, wena sepetu ana ndevu, na mbona kuna wauza vtumbua na maandaz kina mama lishe wengi wana ndevu na maisha yao n ya kawaida?

Jamaa anaongelea wenza wao na sio wao wanawake.
 
Back
Top Bottom