Wanawake watengwa kwenye basi Israel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake watengwa kwenye basi Israel

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Dec 27, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mamia ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasilia, wamepambana na polisi karibu na Jerusalem kwa sababu ya mvutano kuhusu kuwatenga wanawake na wanaume.
  [​IMG]

  Afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa katika mji wa Beit Shamesh, wakati polisi walipoitwa kuondoa ilani kwenye barabara kuu, inayoamrisha wanawake wajitenge na wanaume.
  Makundi ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasili waliwafukuza polisi na kuwarushia mawe.
  Ghasia hizo ndio za karibuni kabisa katika mfululizo wa matukio mengine nchini Israil, ambapo wanawake walilazimishwa kukaa nyuma kwenye mabasi, katika maeneo ya Wayahudi hao, ingawa mahakama yametoa amri kuwa wanaweza kukaa watakapo.
   
Loading...