Wanawake wanauwezo mkubwa zaidi wa kunusa.

Wanawake wanauwezo mkubwa zaidi wa kunusa.

tehee........tehee..........tehe.... bora mke wangu huwa aingii humu kiwango chake cha utambuzi kingekuwa balaaa! sasa tutanuswa mpaka tukome bora kwa wale tunao tumia usafiri wa daladala unaweza kuchanganya uwongo sasa ninyi wewenye magari inakuwaje
 
hiyo ni kweli kabisa ndugu yangu..achana na wanawake ni viumbe wa ajabu..mwanamke hakosei anapohisi.., nikupe mfano mmoja ambao ulinitokea mimi binafsi.
Kuna siku moja from no where tu nilihisi mume wangu anatembea na msichana mmoja, sijui ni kwa nini nilihisi hivyo kwani sikuona dalili zozote isipokuwa hicho kitu kilikuja tu kichwani mwangu niseme ghafla tu..huyo msichana aliwahi kukaa nyumbani kwangu huko nyuma, na niliishi naye vizuri sana na tulielewana sana na aliondoka kwa vizuri tu akaenda kuishi mkoani.
nilipoteza simu yangu kwa hivo sikuwa na mawasiliano naye kwani namba zilipotea pia.. japo nilisikia amejifungua mtoto nikatamani kumpa hongera na zawadi ya mtoto..
Baada ya miaka mingi kupita, Ghafla tu sijui ilikuwaje, nikaanza kumkumbuka yule msichana na cha ajabu zaidi nikawa nahisi km mume wangu anatembea nae hivi..sijui mawazo haya yalitoka wapi kwani huyo msichana alikuwa anaishi mkoa wa mbali, na pia ni miaka mingi ilikuwa imepita tangu aondoke nyumbani kwangu..
Kwa hivo nikatafuta namba yake ya simu nikaipata, nikampigia kumsalimia na kumpa hongera ya kupata mtoto..

Kwa kawaida mie huwa naifuatilia simu ya mume wangu japo sio mara nyingi lkn ikiingia kwenye 18 zangu tu naisachi..sasa ikatokea tu from no where kila namba niliyokuwa na wasiwasi nayo nilikuwa nailinganisha na ya yule binti..hata sijui ni kwa nini nilifanya vile..
Siku moja nikiwa na mume wangu tumejipumzisha hotelini, tunapiga stori za kawaida tu, mie nilimtaja yule msichana nikiwa nasimulia kitu fulani cha enzi hizooo..cha ajabu mume wangu hakucoment chochote mara ghafla akasimama na kutoka nje..nikajiuliza imekuwaje mbona nilipomzungumzia yule dada hakukomenti chochote na kwanini katoka nje ghafla? zile hisia zangu nilizokuwa nazo kuhusu yule binti zikanijia tena, nikachukua simu za mume wangu nikaanza kuzikagua.
Nikakutana na msg moja ya mtu anaomba hela, ila hilo jina lilikuwa la mwanaume sio la mwanamke, na msg yenyewe haikukaa kimapenzi ni msg ya kawaida tu ya kuomba hela..LAKINI UJUE MUNGU NI WA AJABU, pamoja ile namba ilikuwa imeseviwa kwa jina la kiume, na msg yenyewe haikukaa kimapenzi lkn HAPANA moyo wangu haukukubali...mie nilichukua simu yangu nikalinganisha ile namba iliyoseviwa kwa jina la kiume na ile namba ya yule msichana niliyekuwa namhisi ambaye aliyeondoka nyumbani kwangu miaka kadhaa iliyopita..
LA HAULA!!!!!!NUSURA NIZIMIE!!!!!!!!Namba ndio ile ile...GHAFLA NILIANZA KUUMWA TUMBO LA KUENDESHA!!!!!!!mara nikaanza kubleed, mara presha imepanda, ilimradi sijui nieleze nini..
Mume wangu aliporudi ndani hotelini, nikamkalisha chini nikamuuliza!!!!!!!ALISTUKAJEE?!!!!!!HAKUWEZA KUONGEA CHOCHOTE kwa masaa kadhaa, kapiga KIMYAAA!!!!!!!Kalowa jasho wakati mule chumbani hotelini kuliwashwa AC.. wakati huo mie machozi nakaribia kujaza debe...
Mwisho alikiri kuwa yule msichana aliondoka pale home akiwa na mimba yake, kwamba siku moja alifanya upuuzi wkt mie nilipokuwa safarini kimasomo..kwa hivo sasa ndio anamtunza mtoto na ndio maana nimekuta msg ya kuomba hela..ila alibisha kuendelea na uhusiano nae akasema anamtunza mtoto tu..
Aliniomba msamaha saaana, na kupiga gooti, baada ya miezi kadhaa, tulifikia terms za makubaliano..NIKAMSAMEHE...after all kitu chenyewe kilitokea miaka mingi na mtoto mwenyewe ni mkubwa tu sasa, basi, ikabidi nipige moyo konde tundelee na ndoa..
ILA NAJIULIZA HADI LEO, ILIKUWAJE MIE NIKAMUHISI YULE BINTI FROM NO WHERE TU NA BAADAE IKAJA KUWA KWELI? KWA NINI NISIMUHISI MTU MWINGINE NA NYUMBANI KWANGU KUMEISHI WATU KIBAO NA MUME WANGU ANA MARAFIKI KIBAO?. KWELI SIJUI, HATA MIE SIJUI ILIKUWAJE!!!! naye mume wangu akiniangalia hanimalizi, anasema anaishi na CIA nyumbani kwake..yeye alipanga kuniambia kuhusu huyo mtoto pale nitakapozeeka miaka zaidi ya 20 ijayo kama nitakuwa hai..
NIWAAMBIE JAMBO MOJA TU NYIE WANAUME......HAPANA CHEZEA WANAWAKE!!!!!!!!!!!..

...touching story, God bless u
 
ila huo unusaji wa harufu unaumiza sana mioyo

kuna saa unaona kabisa hali si sawa ila huwezo kusema sana maana huna evidence

mpenzi anapiga chepuo nje, unahisi, huwezi sema, huna evidence

ni maumivu badala ya furaha, mie siipendi kabisa.
 
cha ajabu bi. Mkubwa anaweza kuwa darasa la saba tu.

Lakini anakusoma kama gred one pamoja na elimu yako.

Kuna wakati bi .mkubwa alinitesa sana, ndio nimempata mchuchu kwa mara ya kwanza kwanza, napagawaje?

Movement zangu zote mule ndani b. Mkubwa alikuwa ananigundua, nilikuwa sipendi hata kidogo.

Akishagundua maana yake hata kutoka home naogopa, maana atajua naenda kumsalimu.

Hilo ni kweli kabisa, wanawake wana sense za ziada za kila aina na si ya harufu tu na si kwa bahati mbaya, ni uwezo aliowapa muumba wetu kwa kuwa wao ni walezi wetu toka wanapotuzaa, hakuna mama asyekuwa na ESP, "Extra Sensory Perception".

Kuna wakati nilivyokuwa "teenager" nilikuwa nasema, huyu mama'ngu kwanini hajaomba kazi CIA, maana alinijuwa kuliko nnavyojijuwa mwenyewe, sina cha kumficha hata nikijaribu vipi, akiamuwa anashusha nondo kwenye "bulls-eye" nikiona kuwa ni wa ajabu, kuja kuoa nikayakuta yale yale.
 
Ninavojua mm ni kwamba nguruwe ni highly sensitive ktk kunusa akifuatiwa na mbwa na ndio maana baadhi ya nchi walifikiria kutumia nguruwe kutumia madawa ya kuluvya. Lakn kwa wote their sense of smell inaqeza kuwa blocked na harufu ya baadhi ya vitu to the extent that they can fail to get the right smell in some instances. Sasa, nakubaliana na wachangiaji wengine kwamba matumizi ya strong colognes,musks nk zitakuwa na effect kwa hao kinamama. Imagine umepaka after shave baada tu ya kunyoa,then aftershave cream, then body lotion,then unamalizia na musk na zote ni brand tofauti,hyo sense of smell bado itakuwa na nguvu? Mbwa anaishi kwa kuzoea smell ya master wake lakn ukisafiri wiki moja na kubadili manukato yako huchukua muda kukutambua. Au Sense of smell ya mwanamke iko juu zaiidi ya hyo ya mbwa?
 
Nilisikia jana hayo BBC asubuhi kupitia radio one. Verry interesting. Issue ingekuwa kama wanaweza kuhisi ikitokea jamaa katoka kuchit, pangechimbika.
 
duh!kweli jf ni zaidi ya elim.......ila kiukweli mi nikihisi kuna kitu huwa hivyo!wanawake tupo juu!
 
kuongezea ni kuwa inasemekana binadamu wote wana 5senses ila wanawake wana 6senses fanya uchunguzi wa hili pia .mimi nikimuangallia tu mtu m,achoni huwa najua kaniwazia nini sijui wenzangu mume wangu akiwa anaongea especialy na mwanamke kwenye simu au face o face kama niko pale huwa najua mawazo yao beyond that so mume wangu huwa anaogopa maana naweza mwambia kitu cha mbali sana ambacho hakujua ningeweza waza huko au kuhisi huko,namwambia "watch out that chick wants you "anashtuka anacheka lol anasema kweli inawezekana.pia kuishi mujini kunachangamsha hzi senses
au sio Boflo za weekend lakini

hayo ni machale tu ya kawaida hata mimi mwenyewe demu wangu hata akiongea vipi na jamaa kama ni basha wake mi najua tu kwa machale yangu,kwa hiyo hapo there is nuthing spesho.kuhisi kuwa bwana wako leo katembea na mtu ni kitu cha kawaida tu unaweza kukijua kwa kukaa na mtu muda mrefu kwa kuona tofauti ktk tabia zake,hata wanaume wengi madem zao wakipata mabwana huwa tunajua tu machale yanatucheza kwa kucheza na saikolojia yao tu.wala siyo hiyo spesho sense mnayoisema hapa.hakuna kitu kama hichoooo.
 
ila huo unusaji wa harufu unaumiza sana mioyo

kuna saa unaona kabisa hali si sawa ila huwezo kusema sana maana huna evidence

mpenzi anapiga chepuo nje, unahisi, huwezi sema, huna evidence

ni maumivu badala ya furaha, mie siipendi kabisa.

....dah inaumiza sana hii!.........tena ukishahisi ukaamua kumchunguza unaweza kukutana na harufu ya condom au harufu tofauti....
 
hiyo ni kweli kabisa ndugu yangu..achana na wanawake ni viumbe wa ajabu..mwanamke hakosei anapohisi.., nikupe mfano mmoja ambao ulinitokea mimi binafsi.
Kuna 1-siku moja from no where tu nilihisi mume wangu anatembea na msichana mmoja, sijui ni kwa nini nilihisi hivyo kwani sikuona dalili zozote isipokuwa hicho kitu kilikuja tu kichwani mwangu niseme ghafla tu..huyo msichana aliwahi kukaa nyumbani kwangu huko nyuma, na niliishi naye vizuri sana na tulielewana sana na aliondoka kwa vizuri tu akaenda kuishi mkoani.
2-Baada ya miaka mingi kupita, Ghafla tu sijui ilikuwaje, nikaanza kumkumbuka yule msichana na cha ajabu zaidi nikawa nahisi km mume wangu anatembea nae hivi..sijui mawazo haya yalitoka wapi kwani huyo msichana alikuwa anaishi mkoa wa mbali, na pia ni miaka mingi ilikuwa imepita tangu aondoke nyumbani kwangu..
Kwa hivo nikatafuta namba yake ya simu nikaipata, nikampigia kumsalimia na kumpa hongera ya kupata mtoto..

Siku moja nikiwa na mume wangu tumejipumzisha hotelini, tunapiga stori za kawaida tu, mie nilimtaja yule msichana nikiwa nasimulia kitu fulani cha enzi hizooo..
zile hisia zangu nilizokuwa nazo kuhusu yule binti zikanijia tena, nikachukua simu za mume wangu nikaanza kuzikagua.
Nikakutana na msg moja ya mtu anaomba hela, ila hilo jina lilikuwa la mwanaume sio la mwanamke, na msg yenyewe haikukaa kimapenzi ni msg ya kawaida tu ya kuomba hela..
LA HAULA!!!!!!NUSURA NIZIMIE!!!!!!!!Namba ndio ile ile..
Mwisho alikiri kuwa yule msichana aliondoka pale home akiwa na mimba yake....
3-ILA NAJIULIZA HADI LEO, ILIKUWAJE MIE NIKAMUHISI YULE BINTI FROM NO WHERE TU NA BAADAE IKAJA KUWA KWELI? KWA NINI NISIMUHISI MTU MWINGINE NA NYUMBANI KWANGU KUMEISHI WATU KIBAO NA MUME WANGU ANA MARAFIKI KIBAO?. KWELI SIJUI, HATA MIE SIJUI ILIKUWAJE!!!! naye mume wangu akiniangalia hanimalizi, anasema anaishi na CIA nyumbani kwake..yeye alipanga kuniambia kuhusu huyo mtoto pale nitakapozeeka miaka zaidi ya 20 ijayo kama nitakuwa hai..
NIWAAMBIE JAMBO MOJA TU NYIE WANAUME......HAPANA CHEZEA WANAWAKE!!!!!!!!!!!..

Nimejaribu kuedit kutaka kuonyesha point zangu.Kitu kimoja wadada zangu napenda mkijue ingawa watu huwa hawataki kukisikia ni kwamba 90% ya wanawake wote duniani wana mashetani.
hapo nilipoweka namba moja ni kwamba wewe una mashetani tena hujijui,ila bila kujijua unayapenda kwa kujiona kuwa upo mtu spesho kushinda wengine hiyo ndiyo sifa mojawapo ya shetani!! hujawahi kusikia wa2 wakisema mimi nikiwa sina hela ghafla nakutana na mtu tu ananipa hela hata kama sijamwomba??
kuhusu machale yako kuna dada yangu 1 alikuwa anaweza akakaa hivi aksema jina la mtu fulani ambaye hayupo na kabla hajalimalizia lile jina simu inalia na ukiangalia jina unamwona yule mtu aliyemtaja,hayo ni mashetani dadangu,kuhusu hilo jina la huyo dada kukujia ni hao majini ndio waliolileta,sema wewe hujui ndio maana unajizania ni wewe kwa uwezo wako.

2-hapo nilipoweka namba 2 inaonyesha ya kwamba wewe una mashetani dhahiri shahiri tena una mashetani ya utambuzi na usipoangalia unaweza ukawa mganga wa kienyeji!!! sikutukani lakini ndiyo uzoefu wangu unavyoniambia hivyo tena pia wewe una majini mahaba na yanaweza yakakusababishia wewe usizae usipoangalia!!! inavyoonekana hayo majini unayo pia yakuwa mganga ila inawezekana kwamba ni hayo majini mahaba hayataki wewe uwe na mwanaume na ndio maana yakakupa hayo machale ili ukijua uachane na mume wako!!! ni wagombanishi hao ndio maana wakaitwa mashetani.
3-hapo kwenye namba 3 nataka nikuambie tu usijishangae kuwa unauwezo wa ajabu si wako bali ni mashetani yaliyoko ndani yako ndiyo yanayofanya kazi kwako.mfano:kuna rafiki yangu mmoja wa kike naye alikuwa nayo hayo madude yeye alikuwa akikaa mara ghafla anakwenda kwenye ramani basi ataishika misri na haipiti siku 2 kuna tukio kubwa litatokea huko!!! ni mashetani tuu!! ipo mingi tu mifano sema muda tu.
ila point yangu hapa ni kwamba machale mengi ya wanawake siyo kwamba kuna harufu wamebarikiwa kunusa bali ni kumjua mtu kwa saikolojia yake kwa kuijua vizuri tabia ya mumewe au mtto wake na pili kama nilivyosema 90% ya wanawake wote wana majini ndiyo yanayowajulisha baadhi ya mambo ambayo kwa akili za binadamu wa kawaida ni vigumu kujua.
mfano ukikaa na mwanamke halafu mkaachana labda kama mmchokana basi mara nyingi wewe mwanaume huwa haufanikiwi kwa sababu majini ya yule mwanamke huwa yanakuja kukushambulia na kukunyima mafanikio ili kumridhisha mwanamke. angalia mifano Tiger Woods, Chris Brown na wengineo kuna baadhi ya watu walidiliki kusema mademu huwa wanalana zao ukiwaudhi wanakutupia sababu ya vitu kama hivi lakini siyo lana bali ni hivyo viumbe vyake ndivyo vinavyowasumbua, wanawake wakuwa na viumbe hivyo vingi na ndio maana hata ukienda kanisani utawakuta kibao ni wa,ukienda kwa waganga wenye tatizo wengi ni wao......etc
 
AISEE mbona unanitisha hivyo ndugu yangu? Hayo majini yametoka wapi tena? Yaani mie niwe mganga wa kienyeji!!!!!!Acha utani bwana...EEH...Mungu aepushe mbali..
hayo ni mambo ya kawaida tu ndugu yangu kama mtaalamu muanzisha thread alivosema..ukiamini hayo mambo ya majini ndio utayapata kweli..
Ndoa yangu ina miaka mingi na pia nina watoto kwa hivo sidhani km uko sahihi sana ndugu yangu, ila nashukuru kwa ushauri..I NEVER tought on that side, it is the first time to hear from you....
 
Niamini ninachokuambia na kama unabisha na wewe ni mkristo nenda kanisani kwa pasta mzoefu halafu mwambie akuombee (ila kumbuka sio majini wote huwa wanatoka kanisani) au kama ni muislamu nenda kamwelezee maelezo haya sheikh anayejua kusoma rukiya na utamwona huyo jini,au kama wewe ni wenzangu na mimi nenda kwa wataalam asili
mpe maelezo yako naye akitazama kwenye darubini yake atayaona tu na atakwambia.

ieleweke kuwa hakuna hiyo 6 sense ya kunusa bali kuna 6 sense of danger hii binadamu wote wanayo wanaume na wanawake,unaweza ukakaa sehemu ukamwangalia mtu ukagundua kuwa kuna kitu anakufanyia na ukija kuchunguza ni kweli!! hayo ndiyo yanaitwa machale kuna wengine yamezidi na wengine yamelala kabisa.
This nuthing but a nature design to protect human specie from extinct!! hujawahi kuona kuna vijidudu vinavyotambaa ukivigusa tu vinajikausha kama vile vimekufa? ukikaa dkk 2 tu kimya hakuna mtikisiko wowote vinaanza kuondoka??
Au haujaona wewe kuna baadhi ya mimea ukiigusa tu unadhulika sababu huwa inagerate poison ambayo ndiyo ulinzi wa huo mmea dhidi ya wanyama walao majani?? hiyo yote ni nature's design tu.
 
A woman knows. Inakuwa kila nikihisi kitu naongea na kujiambia aah, my illussions. Yaani pazia lilikuja kufunguka like 6years later. Na ni ile unaskiliza habari unajumlisha moja na moja tena in series.

I hate my sixth sense. Pua ndo usiseme. Someone just walked in here and stoped 10 meters from me and i can smell his sweat, gross!
 
Back
Top Bottom