Wanawake wanasheria ni ngumu sana kuolewa, wakiolewa wengi ndoa zao hazidumu. Walimu wanaolewa sana na ndoa zao zinadumu kwanini?

ndoa halisi ni ile ambayo umempata mume au mke kwa kumwomba Mungu na Mungu akakupatia halisi yake unayefanana naye. ukimpata huyo, ng'ang'ana, kwasababu ni almasi. ila hawa wa kuokotana tu kwa akili za kibinadamu, wanawake wengi huwa wanaolewa kwa kufuata kipato au mafanikio, na kama mwanamke wa aina hiyo akipata kile alichokuwa anakitafuta huwa anaona hakuna haja tena ya ndoa.

mimi ni mwanasheria, dada zangu wengi sana wapo frustrated mno over 30s huko, wengine sio kwamba wana tabia mbaya, ila kwasababu tu inasemekana wanasheria ni wabishi. bila kujua kuwa kuna wanasheria wanapigwa hadi vibao kimya kimya majumbani huko. kuna hakimu mmoja alikuwa anakuja mahakamani ana nundu kabisa anaendeelea kuendesha kesi, kimya kimya na hadi leo yupo kwenye ndoa.

hata hivyo, ndoa bora ni ile ambayo mume na mke mnakaa na kujadili na kukubaliana au kukubaliana kutokukubaliana, asiwepo mbabe. Biblia inasema wanawake wawatii waume zao, na wanaume tuwapende wake zetu. ukimpenda mke, utamsikiliza kile anachotaka kutoa hoja, na vingi huwa vinasaidia. sio akitaka kuongea unampiga block, No, msikilize, kama ana mapungufu mweleweshe na toa maamuzi kama mwanaume yenye hoja, maisha yanaendelea; na yeye atoe kwa hoja, basi. huu ni ushauri wangu.
 
Kipato mkuu Sasa mwalimu alete jeuri Umsuse na watoto ataishije?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…