Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,443
Huweza kuanguka mahali hata usipotarajia......
Kama hujawahi kusikia au kama hujui, naomba nikwambie kwamba, wanawake wanaumia zaidi au ni rahisi kwao kuumia wakiwa kwenye mzunguko wa siku zao (Hedhi). Naomba ujaribu kumfanyia utafiti mtu wako wa karibu ambaye unaweza kujua kwamba, hivi sasa yuko kwenye mzunguko wa siku zake, au kama ni wewe mwenyewe mwanamke, hebu jichunguze.
Kama ni kuumia mara nyingi hutokea ukiwa kwenye mzunguko wa siku zako. Je ni kwa nini?
Ni kwa sababu, wakati wa mzunguko huo wa siku kuna mabadiliko kadhaa ya kihomoni mwilini mwa mwanamke. Mabadiliko haya huwa ni ya kupwa na kujaa, yaani hayakai kwa muda mrefu, hubadilika kila baada ya muda mfupi.
Kwa mabadiliko haya, musuli wa nyama nyingine za mwili huathiriwa kwa njia moja ama nyingine. Katikati ya mzunguko wa siku, musuli na nyama za mwili huwa rahisi kuathirika. Katika kipindi hiki, homoni ya kike ya oestrogen, ambayo moja ya kazi yake ni kutoa nguvu kwa musuli wa mwili, hushuka sana. Kushuka kwa kiwango cha homoni hii, hufanya mwili kuwa dhaifu. Ni udhaifu wa ghafla wa mwili.
Mwishoni mwa mzunguko wa siku, homoni nyingine ya relaxin huongezeka. Kuongezeka huku ni kuruhusu nyonga kujifungua, ili hedhi itokee. Lakini kuongezeka kwa homoni hii hufanya nyama za mwili kuwa tepetepe, kinyume na zinavyotakiwa kuwa imara. Kwa hiyo muda mfupi kabla mwanamke hajaziona siku zake ama pale anapoanza kuzioana, yupo kwenye hatari ya kuumia kirahisi. Wakati huu kuteleza au hata kujikata ni rahisi zaidi.
Dk. Stephen Sandler anasema kuna uhusiano wa karibu kati ya kiwango cha homoni kwenye mwili wa mwanamke wakati wa mzunguko wa siku zake na uimara wa mwili wake. Anasema uhusiano huo uko wazi na hauna mjadala. Kwa sehemu kubwa, wanawake wakiwa kwenye mzunguko huu, maeneo ya viungo kama magotini, viungo vya vidole na miguu huwa na udhaifu.
Kwa hiyo kitendo cha kuvuka mahali pafupi tu, kinaweza kumsababishia mwanamke maumivu. Kuinama na kuokota kitu kunaweza pia kumsababishia maumivu. Wataalamu wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu ni kwa nini wale wanawake wanamichezo, huwa wanaumia kirahisi wakati fulani, kuliko wakati mwingine. Hivi sasa wamepata jibu, kwamba ni kutokana na mzunguko wa siku…..
Naomba Mods wasipeleke huu uzi Jukwaa la JF Doctor maana unahusika sana hapa MMU...
Copy to: Kaunga, Madame B, lara 1, Lisa, nivea, MadameX, BADILI TABIA, AshaDii, marejesho, Zinduna, Preta, Zion Daughter, Remmy, mwaJ, Asnam, Kipipi, snowhite, cacico, Paloma, Mamndenyi, vivian, King'asti, amu
Last edited by a moderator: