Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Tupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.

Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.

Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"

Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.

Akajibu "Wee naweee, haya andika..."

Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.

Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"

Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,

Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"

Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa

Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"

Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia

Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).

Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)

Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.

Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"

Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?

Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.

Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.

Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.

Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".

Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza

"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."

ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.

Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.

Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".

Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.

Sisi tukasepaa.
 
Aisee huyo mama ana kiburi Sana alafu Hana Hela. Angekuwa ana Hela asingepokea zile alizopewa. Mtu kaambiwa shuka anakataa alivyoona kibunda akalowa. Akaona Bora achukue maana ana shida na Hawezi pata bahati kama hiyo Tena. Nimeamini wanawake unaweza kuwavuta Kwa pesa.Tutafutee Hela tu.
 
Siwezi laumu maana hakuna ata mmoja wenu alijaribu kufahamu anasumbuliwa na nini hadi yeye kufanya au kujibu hivyo.

Ukute kuna tatizo binafsi limenfanya asafiri. Umeishia kuhukumu tuu mkuu
Matatizo hayahalalishi ugomvi na wengine, kila mtu humo lazima ana yake..

Pili mtoa mada kama sikosei kaandika ya kua ali note kupitia mawasiliano yake kabla, ya kua ana matatizo ndio maana akajiwa na nia ya kumsaidia na kweli alisaidia kwa mawazo lakini pia kukaa kimya..

Na usikute hata hayo matatizo ni ya kujitakia, binafsi naona wame msaidia sana, wewe na kisirani chako unakuja kutukana watu gari zima, watu wanahitaji utulivu, kumbuka hio ni safari, kuna wanaosafiri kwa shida, biashara, makutano, mapatano n.k n.k. Hivyo wanahitaji utulivu.

Binafsi nampongeza kwa utulivu, mwingine angemkaba koo..... oohoooo, utulivu ni kipaji kingine.

Sidhani kama umesoma vzr.
 
Bila shaka mnasafiri kutokea maeneo ya Morogoro hususan Ifakara au kwa ujumla maeneo ya mashariki mikoa ya pwani. Ujasiri wa watu wengi huku ni midomo yao na ka-uchawi.
Umeionaje Morogoro Mkuu? Nijibu chap kwa haraka
 
Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele"
Mshana Jr,ungekua Hakimu/ Judge,hukumu zako zingekua zimenyooka sana na hazina mashaka! Maana unajua sana ku cote vile vipengele muhimu kwenye story!!!
 
Maisha yana mengi sana, huenda anapitia mengi magumu yanayohitaji msaada. Japo pia sio sawa kutukana wapi hovyo hata kama una matatizo binafsi.

Ila watu wanapitia magumu me gi, kiuchumi, kiafya, kimahusiano na kijamii.
 
Back
Top Bottom