Kwa ulinganisho huu wanaume ndo wana roho mbaya zaidi ya wanawake!
1 ni rahisi kusema hgeli anaonewa kwa sababu anagombezwa kwa kutofanya wajibu aliopangiwa. Hata wewe kazini kwako unagombezwa kwa email ama kwa simu (wanajeshi wanarushwa vichura na boss wao, sio?). Siku utaachiwa jukumu la kusimamia hgeli na watoto utapata wazimu. Ningekuwa mkeo ningesaka sababu ya kuondoka home 3 months only nikusikie!
2 hivi kuna mwanaume anaishi na mtoto wa kambo? Ni wachache sana na huwa wanakuwa na mambo yao mengi tu! Sema wanawake tunajua ku-appreciate na kusema walau kaniruhusu mwanangu ajibanze hapa niishi nikimuona. I bet wanawake wenye watoto wao huwa wanakuwa na kafungu ka ziada kuweza kuleta ulinganifu.
3 wanaume wangapi wanaishi na wakwe zao? Hivi baba wa mkeo akihamia kuishi na wewe hapo ndani, na ajitie faza house utabaki unachekelea? Ukisema una hamu na ugali anamuambia mwanae hakuna kupika ugali usiku, anaanza kukupangia na muda wa kurudi nyumbani kwako na kukataza kuvaa jeans anataka uvae sarawili za kijani kuenzi ccm?
Ili ujitambue una roho mbaya kiasi gani, mara ya mwisho lini umetoa hela ukamtumia baba mkwe wako? Amesomesha mwanae hukuwepo, mwanae ana kazi ya kuchangia kukutunza na wanao na kujenga nyumba yenye jina lako, na unatamba staki ngebe nyumbani kwangu, utasema mkeo ni mgeni! Unamtumiaga mkweo hela bila kuombwa?
4 Ungekuwa na vishemeji vinakaa kwako na vinataka kukusaidia kuendesha mji wako ungekuwa na roho nzuri sana na kuwaachia jahazi?
Dawa ya kukaa vizuri na watu ni kuweka pua yako inapostahili. Sikatai wapo wagomvi na wachokozi. Mie nimekua na kaka wa kambo lakini sikuwahi kujua ana mama yake hadi nikiwa std 5, na ni kwa sababu mama yake alikuja kumtembelea. Yeye mwenyewe alijua ana mama yake wakati. Kamaliza form 4! Wanawake hawana roho mbaya, wana VISASI vibaya.
Wanawake wana roho mbaya sana na sijui ni kwanini. Ukitaka ku prove fuatilia haya hapa.
1. Wanavyoishi na ma house girl
2. Wanavyoishi na watoto wa kambo
3. Wanavyoishi na wakwe zao
4. Wanavyoishi na mawifi.
Na pia angalia mwanamke akawa Blandina Nyoni fulani hivi usipime huo moto wake kwa wanawake wenzake.