Wanawake wakubwa ndio wanafaa zaidi.

Mkuu naona umeamua kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Vikongwe waende na vikongwe wenzao tu, tusidanganyane hapa! Mtu mautamu kashamalizia kwa wenzie wa umri wake huko, ati nije nikajifyonzee makapi ya mua yenye miaka 38 wakati vitu vipya kabisa vya 25 and younger vipo? Hapo unakuta mua ushatafunwa hadi na wavuta sigara na wala ugoro! Phew!
 
wanawake wengi tunapenda kuwa na wanaume waliotuzidi umri......hii inakufanya ujisikie amani zaidi.....vitherengeti boys vinasumbua sana


hujanielewa kabisa...
Sizungumzii wavulana wadogo wanaolelewa..
Hapa nazungumzia mwanaume ila kiumri ni mdogo but ni mtu mzima...
Say man ni 30 but mwanamke 36 hivi au 40 kwa 45.
 
Boss nafikiri leo umekula msuba kama siyo ganja kabisa. No. 9 haipo kwa mwanamke yeyote mwenye akili timamu. Labda awe kichaa au taahira
 
Kuna mkaka ameoa mwanamke mkubwa wakigombana kidogo utamsikia mwanamke anasema 'niache na uzee wangu, niache'.
Nahisi wanawake hukosa furaha na ujasiri wanapoolewa na wanaume wadogo.
 
kuna mkaka ameoa mwanamke mkubwa wakigombana kidogo utamsikia mwanamke anasema 'niache na uzee wangu, niache'.
Nahisi wanawake hukosa furaha na ujasiri wanapoolewa na wanaume wadogo.

jiulize mbona hamuachi?????????
 
Kuna mkaka ameoa mwanamke mkubwa wakigombana kidogo utamsikia mwanamke anasema 'niache na uzee wangu, niache'.
Nahisi wanawake hukosa furaha na ujasiri wanapoolewa na wanaume wadogo.

Husni umenchekesha sana! Yaonekana huyo mke ni mzee sana eh?..lol
 
mbibi haswa, nahisi ana mvi. Hahaha! Sio mzee sana mwaya ila kwa kuwaangalia tu unaona tofauti. Mzma wewe?

Hahaha!.. Mi mzma sana! Naiman we pia uko poa!..vp na wewe hutafuti kiserengeti? Nna young bro hapa...lol..
 
Back
Top Bottom