Wanawake wakibeba mimba wanatukomoa

mm ni mjamzito ghafla simpend mume wangu yaana ananipa hasira kila wakati afu tenda la ndoa sitaki hata kidogo ,natamani nisafiri niende mbali sana kusikojulikana
 
Mimba bwana balaa asa miezi ya mwanzon mm binafsi now namimba ya miezi Tisa muda wowote najifungua ila nilivyo teseka mmmm apana na unakuja tu hamna kujifanya wala nn
Nilikuwa sipiki home Mume inabidi ale chips na nikimkuta analia ndani atanikoma maana harufu nilikuwa sipend,mafuta yake ndo kabisa ikabidi asiwe anataka mafuta wala pafmu akiingia akiwa na jasho kosa jamani mimba zisikien tu nashukuru Mume alinivumilia mpaka mwezi wa tano hiv nikarudi normal mpaka now
 
Nakumbuka kipindi flani wakati nina mimba nilizunguka dar nzima natafuta miwa mida ya jioni,nikawa mwenyewe nalia kwenye gari kisa sioni muuza miwa,bahati nzuri nikaja kuipata kimara mida ya saa nne usiku,nikapark gari nikaagiza kama paketi kumi hv,ile namaliza tu,kichefu chefu kikaanza,hah hah nikaanza kujuta kwanini nimekula,tofauti na wengine mimi muhusika aliikataa mimba,so nakumbuka mara nyingi hzo story za kuamka saa tisa usiku nilikua nafanya mwenyewe,now mtoto wangu ana miaka miwili,all the best kwa mama watarajiwa na wito wangu kwa baba watarajiwa ni wawe wavumilivu hakuna kudeka bali ndo hali halisi
 
Kwan ulilazimishwa kubebesha mimba?? ukishindwa majukumu utasaidiwa ila usije kuwa na hasira ukikuta mkeo kakunjwa mithili ya samak
 
Basi upande wa pili mumeo atakuwa anasikia kichefuchefu na hasira
wewe muangalie tu tumbo lake linavyomuuma kila mara
uwe unaenda naye Klinik mara kwa mara ndio utaepika michafuko hiyo

Hongera

Hivi hiyo hua inasababishwa na nini? Kwamba mwenzangu anisaidie hicho kichefucgefu na hasira!
 
Huo ni upu.mba.vu tuuu, mm wife bro wangu anawacheka wanawake wanojifanya eti kmimba zinawazingua ,Mke yule very good kwa kweli kakomaa mpaka mwisho anajifungua mapacha BILA MBWEMBWE SASA MWANAMKE mimba mtoto mmoja lakini KELELE hadi irani anjua UNAMIMBA sheme
 
Hivi hiyo hua inasababishwa na nini? Kwamba mwenzangu anisaidie hicho kichefucgefu na hasira!
ukiona Mume wako anashikwa uchungu ujue ni mapenzi yako na mtoto mtarajiwa na wala sio LIMBWATA
Wanaume tunapewaga maadhabu ww acha tu
ukute basi ni mke wa kwanza na mimba ya kwanza
 
Sijui wanawake wote wakibeba mimba wanakuwa hivi au ni huyu wa kwangu tangia abebe mimba ndani hakukaliki mara nina hamu na kitu fulani ukileta hali, amehama chumbani eti kinatoa halafu mbaya analala kwa housegirl.

Nimejitahidi kufanya usafi lakini wapi hataki hata kuingia humo nimebaki nalala mwenyewe kwa kweli kuna maudhi mengi mpaka nachoka hivi ni kweli hizo mimba zinawafanya hivyo.

Nimejaribu kuongea na marafiki ambao wenzi wao walibeba mimba walichonieleza anayoyafanya huyu wangu ni cha mtoto hivi kweli kwamba mimba huwafanya hivyo au mnatufanyia makusudi.
mara nyingi ni mabadiliko ya mwili! Na mama anateseka kweli!haaa mimba ikiwa ndogo! Wengine ikifika miezi minne na kuendelea anaweza kuvumilia ila wengine hawawezi!
Jitahidi kupeleka anachopenda as long una uwezo nacho!
 
Mabeki tatu na wanafunzi wakibeba mimba wanakomaa nayo kimya kimya bila kusumbua mtu, hawa walio kwenye ndoa ndio wana hizo sera za mimba kutaka mafenesi saa nane usiku!
Huwa wanakua na hizo hali za kutaka au kukataa kitu flani, ila hawana jinsi ya kuelezea! Waliowapa ujauzito wamepepea! Asumbue matron au mwajiri wake hajipendi?
 
Ni hali ya kawaida,mi kipindi changu sikutaka kuongea na mwenzangu hd najifungua. Yaan nilikuwa nahisi km donge fulan limenikaba rohon hivyo nafuu yangu ilikuwa ni kutomsemesha. Alikuwa anataman sn kuongea na mm ila ndio hivyo na ht nilipokuwa namjibu basi badae ntahangaika sn kwa kutapika.

Thanks God now mtoto wetu ana mwaka na miezi 6 ila baba ndo hayupo tena......dah kwakweli Mungu ana makusudi yake,hamu yote ya mtoto aliyokuwa imepotea km ndoto. Apumzike kwa amani!
Pole sana mpendwa
 
Nashukuru sana wachangiaji nimegundua kitu kutoka kwa hawa watu,
kwa maana nipo katika kipindi kigumu kweli,
ila baada ya huu mwezi kuisha nitaitwa baba.

Hahaahahaha usijifu peke yako..msifu na aliyeibeba tena umheshimu kweli kweli maana amebeba evidence ya kufanya Sex bila kondomu tena kwenye siku hatarishi
miss chaga aione hii
 

Attachments

  • 1432392201998.jpg
    1432392201998.jpg
    26.4 KB · Views: 184
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom