Wanawake wakati mwingine, hapana jamani!

Wanawake wakati mwingine, hapana jamani!

Siku hizi nikitoka job, siwashi taa alafu ndani sikaagi. Nafika na kutoka narudi usiku, hadi nafikiria kutafuta nyumba nyingine ndugu yangu, swala ni kwamba vitu alivyohamishia kwake nitamdaije? maana vingine vina mwezi na zaidi na hana mpango wa kurudisha, yeye akifika anaangalia nimeongeza kitu gani ili abebe. Tunapishana bafuni wala hana time kabisa, dahh!! Shida ndugu
Subiri tu aje akwambie gas imeisha ukanunue then achukue tena... kwani huyo dada yako?
 
kama hataki kukusemesha mwache hivyo hivyo, jifanye kama hujaona any changes kwake, msalimie endelea na shughuli zako, hafai hata kwa bure huyo
 
wanawake sazingine wana vitabia flan amazing kama vitoto vile wewe muangalie wife hapo home na hawa ma-ofisini yaani anaweza kukujengea mazingira flan ambayo atakupeleka nayo sasa ukishamstukia wewe nenda nae vile atakavyo ilimradi haikukost
Lakini kaninunia mkuu, pesa achukue asitake kulipa, halafu anahitaji zingine kumwambia sina imekuwa kosa, kaamua kunichunia
 
kama hataki kukusemesha mwache hivyo hivyo, jifanye kama hujaona any changes kwake, msalimie endelea na shughuli zako, hafai hata kwa bure huyo
Nashukuru mkuu kwa wazo lako, nitalifanyia kazi
 
Itabidi ukae kimya kidogo kama njia ya kumuonyesha kuwa hukupendezwa na hyo tabia yake,na epuka majibizano ili asije ku take advantage ukawa wewe ndio umekosea,
Nakushukuru mkuu kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi
 
Wana jamii

Kuna mwanamke mmoja nimezoeana nae sana kwa issue za kiofisi, lakini huwa tunapiga story mbalimbali kama dada yangu ambaye namuhushimu sana na pia kama mteja na yeye mara nyingi huwa anakuja ofisini kwangu kwa ajili ya huduma mbalimbali. Kwa kweli tumezoeana sana

Wakati mwingine anakuja, ananiambia nina shida sina pesa ya ada kwa ajili ya mtoto, huwa nampa. Mara ooo sina pesa ya matumizi nampa. Mara nikopeshe pesa kwa ajili ya kupeleka VICOBA, huwa nampa na wala harudishi.

Sasa juzi kaniomba nimkopeshe pesa, na anadai kuwa atanipa baada ya mwezi mmoja, mi nikamwambi kwa sasa pesa sina, ningekuwa nayo ningekupa. Nimefanya hivo kwa sababu najua nikimpa tu ndo imekwenda hiyo, hairudi tena.

Tulipoonana, naona mtu kanuna wala hataki kunisalimu kabisa. Nkajiuliza ina maana tatizo ni pesa? Hapo sina mahusiano naye kabisa ya kimapenzi, ingekuwa hivo si anaweza kunitoa roho!

Hivi wanawake hiyo ni tabia yenu mpaka mnajisahahu kana kwamba imefikia mahala rafiki tu kiume unamfanya kama mpenzi wako jamani au mmeo?
Mkuu pole sana na inasikitisha sana, pesa ni tamu sana na pia ni mbaya sana na haina rafiki, mpenzi, ndugu, humantarian, hekima, busara nk... Pesa inatoa watu roho sembuse kununa, ingawa pia mwanamke ana jinamizi lake hapo..
 
Bora wewe mimi wangu nikimtumia pesa chini ya laki kama nilivyomzeashaga enzi za kikwete hata Asante sipewi na simu sipigiwi
 
Back
Top Bottom