Wanawake wa zama hizi hawalii mahusiano yakivunjika

Walie wanapungukiwa nini wakati kuna foleni ya watia nia wanasubiri ridhaa ya kuchukua jimbo.

Tuendelee kutafuta pesa tu.


Let's meet at the top, Cheers 🥂
 
Kuvunjika kwa mahusiano kunaumiza sana iwe wanawake, wanaume wa kizazi chochote kile. Unaweza ukadhani mtu alii lakini maumivu anayoyapata kwa ndani ni makubwa sana kuliko hata kilio unachokiona kwa macho.

Unadhani hawalii kwa kuwa sasa hivi kuna mitandao mtu anaweza ku-act kama mzima kumbe rohoni anaumia sana.

Mtu kama Shishi kwa sasa ana maumivu makubwa sana kuachana na mumewe na ukute anatembelea magoti huko warudiane
maumivu ya mapenzi ni makali kushinda hata msiba. Mapenzi yanauma asikwambie mtu
 
Mambo ya kuumizana yalikua yakitoto sana, yani mwanamke akulilie wakati wanaume wapo wengi wanaojua kujali, ukikitupa mwenzako anakisubiri kiwe pendending
 
Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi, ukisusa wenzio wanakula,, ukisema Cha Nini wapo wanaolia kukipata lini, ukishuka wenzio wanapanda,, naanzaje kujiliza sasa hapo
 
Tuna mambo mengi sana ya msingi ya kutuliza
Imagine;
Manchester inilize
Nikichana mkeka nilie
Barcelona inilize
Bado matatizo ya kifamilia yanilize

Hadi mwanaume akiniacha nae nilie?hell no aseee!!siku hizi tunalizwa na mambo ya msingi tu
Nakazia 📌📌

Pua ikiziba unatumia mdomo unalia Nini Sasa😅
 
Back
Top Bottom