Ni kweli, ila kuvaa wanajua ila mpangilio ndo ishu,unaweza kukuta mtu kavaa nguo za club anakata nazo mitaa kariakoo, mwenge posta, au kwa arusha huku kilombero mbauda ungalelo mchana kweupee, wengine hadi weekend wamenyuka suti, ukienda sehemu za starehe ndo utacheka, wengine yupo outing na mpenz wake, mwanaume kakung'uta kaunda au suti hiyo, mwanamke yupo na satini yake au suti na yeye, mh si kwamba ni kuiga utamaduni wa watu hapana, mpaka sasa hatuna vazi rasmi la taifa, ila kuna vitu tumezaliwa tumevikuta, mbona hata tulivyokua wadogo tuliambiwa nguo hii ya shule, hii ya kanisani, hii ya sokoni, hii ya shambani, hii ya mjini n.k so hapa utaona kumbe mpangilio wa mavazi haujaanza leo, kilichobadilika ni aina ya mavazi tu sasa shida ni kujua wap nivae vip na wap nivae vip.ila hili nalo halihitaj gharama kubwa, wanohitaj gharama ni wale sisterdooz wanaopenda kumatch everything, hapo ndo atahitaj hela ya kubadilisha matchin kila week, ila yote kwa yote elimu zaid inatakiwa kutolewa either kwenye vituo vya TV, radio au blogs, or magazeti ili kuwaelimisha watu jinsi ya kuvaa, wapi uvaaje na vipi according to different occassions.Ahsanten