Imeshazoeleka na inajulikana hivyo siku zote miaka yote karne zote kwamba mwanamke ni kiumbe mwenye Aibu lakini ki ukweli siku hizi/karne ya leo mpaka umkute mdada ana aibu ile ki ukweli na sio ya kuigiza katika 100 utawapata wawili au mmoja au usimpate kabisa.
Nashindwaga kuelewa ni haya maisha ya sasa hivi ndio yamewapa kujiamini au ndio ile na nyie kutaka kuonyesha mnaweza kukodoa uso kwa uso?
Unaandaa appointment na mdada,anakukubalia vizuri bila tatizo Anafika location mnapiga story mnacheka mna enjoi,Chakula kinakuja mdada ni anakula huyooo wakiume akasome,kuna ile inatokea kwenye plate ya chakula kuna vitu huli Mfano umeagiza Wali na Samaki kwenye mboga wakaeka Nyanya chungu,bamia Mimi hua silagi hizo basi ntazitoa ntaeka pembeni,mdada akiona utamsikia HULAGI HIZO? KWANINI? EBU LETE HUKU WE NDIO HUJUI VITU VITAMU KWELI,bas anahamishia kwenye sahani yake anagonga.
Siku hizi unamsimamisha mdada ana simama unaongea nae anakutolea mimacho hadi unasahau kumuomba Namba unabaki kumuuliza dada Njia hii ni ya kwenda wapi? kwa jinsi isivyo na haya Atakupiga mjicho atakufyonza Fyonzo hilooooo Hadi unaeza sema Nishaelewa njia n ya wapi.
Mdada una mtongoza,unajua raha ya kutongoza ni ile hata mwanamke uwe unaangalia pembeni bwana ili mwanaume atoe yoteee,ila siku hizi mdada wakati unamtongoza ni kama vile yupo chumba cha Paspot size kakaa kaambiwa aangalie CAMERA yani ni anakukodolea macho A to Z mpk unajikuta una hairisha unamwambia ka Vipi ntakucheki kesho..
Wanawake hamna aibu siku hizi Jamani, na kwakujua kuigiza hamjambo mkiwa na wapenzi zenu mnajitia vipoleeeeee ila subiria sasa mzoeane aseee unaeza hisi unadate na DUME mwenzako toto Linaongea aibu kwishaaaaa...wakija wageni ndio atleast anazuga tena Wakiondoka anarudi kule kule.
Ki ukweli hili jambo bwana mliache Sifa ya mwanamke kubwa ni Aibu Aibu bwana..ustarabuuu,hekimaaa Huyo ndio mwanamke wa shoka,ila nyie wakaza macho ki ukweli mnatuweka katika DUNIA nyingine kabisa.
Sitosahau yule dada nilie mkanyaga bahati mbaya Jana kwenye Mwendokasi,Nilikunjiwa/benuliwa mdomo nikahisi ni Kisheti au kau kau au dada wa watu mdomo una matatizo...