PeeWee
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 1,332
- 3,191
Unakunywa chai?Ngoja ninywe Chai kwanza labda nina njaa 😊
Hii yaweza kuwa dalili mojawapo ya broke🤣🤣🤣🤣
Unakunywa chai?Ngoja ninywe Chai kwanza labda nina njaa 😊
Haya yote hayana maana kama mwanamke hajavutiwa kimapenzi na wewe, mwanaume utayafanya haya yote na zaidi ya haya, lakini kama mwanamke hakupendi, you'll get almost nothing in return realMamy Dr. MariposaWanawake tunapenda Kupendwa, Kuheshimiwa, Kuthaminiwa, kusikilizwa,Kusifiwa, kuhudumiwa na mambo mengine mazuri kama hayo.
![]()
Kuhusu kupendwa
tunapenda upendo unaoonekana kwa vitendo, hususan uvumilivu wakati wa shida, na upendo wa kweli huondoa hofu na tunakuwa huru zaidi Na mwanamke aliye huru ndiye anang’ara zaidi.Halafu anakuwa sio mchoyo😜.
Kuheshimiwa mbele za watu na hata faraghani.Maoni yetu yawe na uzito. Tukiheshimiwa, ujasiri wetu unaongezeka. Na mwanamke mwenye ujasiri anajenga familia vizuri.Usitegemee kuheshimiwa kama hujisheshimu na huheshimu wengine.
Kuthaminiwa na kuwekwa kipaumbele hususan mbele ya watu. Kuchaguliwa sisi kwanza. Juhudi zetu pia ziheshimiwe
Tukijua sisi ni kipaumbele, tunafurahi na tunafanya bora zaidi bila kulalamika hususan kitandani.
![]()
Kusikilizwa. Mwanamke wakati mwingine anapitia changamoto nyingi huenda Kila mtu anaweza kumlaumu lakini ni vizuri akasikilizwa kwa upole na kueleweka kisha akapewa ushauri.Tukisikilizwa, mioyo yetu inatulia. Na moyo uliotulia unazaa mawazo mazuri.
Tunapenda kusifiwa mfano "Umejitahidi." "Umevaa vizuri." "Nimekuona umependeza” umepamba nyumba vizuri.
Sifa ndogo inaamsha Ile hali ya kuendelea kupenda na kuvumilia. Inatupa nguvu ya kujitahidi zaidi kila siku.
Kukumbatiwa. Tunapenda sana kwa sababu kunaponya uchovu wa siku nzima na kutoa faraja kwa mwanamke na kumfanya ajisikie vizuri.Kukumbatiwa kunatoa uhakika wa kuonyesha kuwa "nipo nawe". Hapo ndipo tunapopata nguvu ya kupambana tena.
Tunapenda kuhudumiwa.Mfano kununuliwa zawadi ndogo ndogo na hata kubwa. Mfano Nguo za ndani,Saa,Gauni,Viatu, Kupelekwa sehemu nzuri kupumzika, Pesa kidogo ya matumizi na vitu kama hivo. Tunapenda pia kuulizwa "Umekula?" "Umelala?" "Nikusaidie nini?
Huduma ni lugha ya upendo. Inatufanya tujisikie salama na kutunzwa.
![]()
Tunapenda ushirikiano,Mfano Katika malezi ya watoto kupeleka mtoto clinic,shuleni na kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani.
Mwanamume anaposhuka na kushiriki, mzigo unapungua. Na mwanamke asiyechoka ndiye anang’ara na kunawiri vizuri.
Kuhusu pesa si kipaumbele sana kwa mwanamke kama kutakuwa na upendo, heshima, ushirikiano na uwajibikaji.
Mpe mwanamke upendo, heshima, kipaumbele na ushirikiano. Utashangaa jinsi atakavyonawiri na katika nyumba yako upendo na amani vitatawala.
Uttoh tumekutapel nini jamani
Yaani nimekukuna almost 5 years then leo uchepuke useme sikukuni vizuri. Seriously!!!Kama humkuni vizuri je?
Ulitakiwa kupata breakfast 😋😅😅😅😅😅
Inawezekana
Nilipaswa kunywa Juice,Supu au nini?
Nikuepo mbona hiyo nili comment janaUlikuwa wapi? 🤭😜
Usituharibie kwa kijana wako
Umenena 🤣🤣Ilikuwa Before hajajua zingine 😜
Tanga raha😂😂Hili ni jina tu la kizungu.
Mimi napata Chai yangu ya Tanga hapa.
Imepikwa na Mama yangu.
Tamu balaaa!
Na Vitumbua vya Nazi.😋
Tupe nafasi nyingine uone
😅😅😅😅 Tunabadilika kulingana na wakatiKweli vipaumbele na mahitaji kwa Wanawake yanabadirika kila muongo
Sisi miaka yetu ya 47, bibi zenu hawakuwa na na haya mahitaji yenu
Nilipojichanganya kuongeza mke wa tatu miaka ya 2010' hapo ndiyo nikakutana na haya mahitaji/vipaumbele
Hadi nikahisi ananifanyia kusudi nijutie kumfanya mke mdogo 🙌
Hapana, wanaume wanaupendo wa dhati. Wanapenda mwanamke mmoja tu. Wengine hao wanatamani tuNa nyie mkionja nyingine mna change vilevile