Habarini wana jamii forum wenzangu,
Hope ni wazima wa afya...
Jana mida fulani ya jioni nilikuwa mimi na rafiki yangu kwenye gari aina ya Noah tunatoka zetu town tunarud mitaa ya home ambako ni mbali na town.
Tukapaki gari mitaa fulani sio mbali na town tukasema ngoja tupate soda mbili tatu, sasa hapo sehemu tulipokuwa tunakunywa soda kwa pembeni kulikuwa na dada mmoja maji ya kunde mkali kinoma anachezea simu yake sijui alikuwa anachati au vipi, basi jamaa yangu akamuita dada vipi unaweza kujumuika na sisi tubadilishane maana??
Lakini jamaa yangu akiwa na imani kabisa huyo dada atakaa.Cha ajabu yule dada hakukataa akajumuika tukamkaribisha soda achukue, au kama anakunywa bia aagize, akakataa akasema ameshakunywa kipindi sisi hatujaja, basi sote zikaendelea mpaka mida ya saa moja na nusu dada wa watu akatuzoea vibaya na kutuamini kwa muda mfupi tukawa marafiki,
Akasema yeye anafanya kazi zake ndogondogo za kuuza nguo za kike, tukamwambia na sisi tuna duka la mzee la bolts na nuts tunamsaidia ila tumepanga miataa ya Uchira kama kilometa 12 kutoka moshi mjini.
Sasa baadaye jamaa yangu akamshawishi yule dada kama hatojali anaweza akaondoka na sisi twende maeneo tunakoishi akapajue kama hatajali halafu tutamsindikiza,
KWANINI YULE DADA ASIKUBALI,TUKAONDOKA NAYE TUMETEMBEA KAMA KILOMUTA 9 HIVI, JAMAA YANGU AKASIMAMISHA GARI AKAMUULIZA HIVI WEWE DADA MBONA UNAJIAMINI SANA YAANI SISI WATU WENYEWE HUTUFAHAMU VIZURI NA USIKU HUU UNAKUBALI KUJA TUNAPAOISHI UNAJUAJE KAMA SISI NI MAJAMBAZI AU WABAKAJI???
Akacheka mwenyewe akasema nyie mtakuwa watu wazuri tu mnaonekana,jamaa akamwambia ashuke kwenye gari akampa 5000 ya nauli akamwabia nenda nyumbani wewe sio mtu mzuri hata huogopi watu.........
Mara nyingi nimekuwa nikiwaona hata wakinadada wakiambiwa panda lifti twende hawawazi wanapanda haaaaaaoooooooooooooooo ........
Kwanini wanawake hamuogopi vya watu???????