Wanawake ni waroho sana au wanakomoa?

Wanawake ni waroho sana au wanakomoa?

Wala hawana uroho, matatizo tu ya kiuchumi yanakusumbua. Siku hali ikikaa sawa wala hautamind, actually utajikuta unambembeleza kula na kunywa.
 
Wanawake wengi wa kibongo wanaishi maisha fake.
Sasa huyu tunayemuongela hapa ufeki wake ni upi? Chipsi kuku ama njaa?
Mtoa mada, siku zingine kutana nae kwa mama ntilie aagize makande.
 
Unampigia simu demu wako mida ya saa tisa, anatoka nyumbani mpaka sehemu ulipo. Anaagiza kinywaji na kumuita mhudumu wa jikoni, niletee kuku nusu na chips. Wewe umetoka nyumbani hujala huko? Unajua nina bei gani mfukoni? Kuweni wastaarabu.

Ni afadhali akiwa peke yake wengine huja na lundo la marafiki
 
Hahaha..pole sana kaka. Hv kwani ni lazima kuwa na mwanamke?
 
Unampigia simu demu wako mida ya saa tisa, anatoka nyumbani mpaka sehemu ulipo. Anaagiza kinywaji na kumuita mhudumu wa jikoni, niletee kuku nusu na chips. Wewe umetoka nyumbani hujala huko? Unajua nina bei gani mfukoni? Kuweni wastaarabu.

Umenikumbusha kuna uncle wangu huwa anawashangaa sn wanawake hawa "we itakuwaje kila siku unakuwa na hamu ya kula kuku tuu"
 
Badala ya kumuuliza mwenyewe, unakuja kulalamika humu!!
Mimi kuna mmoja nilimuuliza, hivi unapoagiza unajua nina kiasi gan mfukoni?!
 
Duh watanzania tumefikia hatua ya kupigia hesabu ya chakula? Jamani ni kinyesi tu hicho mwisho wa siku.
Mi nimejiuliza tu, kama huna kitu mfukoni umemwitia nini binti wa watu kwenye kiota cha makulaji na manywaji??
 
Mi nimejiuliza tu, kama huna kitu mfukoni umemwitia nini binti wa watu kwenye kiota cha makulaji na manywaji??

Ni kumuonea huruma, hapendi basi tu. Mshauri aichague CDM 2015 ili maisha yawezekane.
 
Mkuu acha ubahili kumnunulia chakula mpz wako unaona issue
 
baadhi wana ongozwa na matumbo appointment ni lazima hotelini
 
Back
Top Bottom