Ukatili wa wanawake unasababishwa na wanaume...
-Kama mama wa kambo anawatesa watoto, mwanaume kachangia kwa sababu hakuweka msimamo juu ya malezi ya watoto
-Kama mama anamtesa msichana wa kazi, mwanaume kachangia kwa sababu wakati mwingine ni maudhi ya baba husababisha mama kuhamishia hasira kwenye shabaha dhaifu na kama si watoto, ni laizma msichana wa kazi atakiona cha moto, lakini pia kama mume anaonekana kumtamani binti wa kazi, mama anaweza kuwa mkali ili kufikisha ujumbe kwa binti kwamba akithubutu tu atakiona cha moto, kwani hawezi kumkabili mume.
-Kama binti katoa mimba au kutupa mtoto, ni lazima mwanaume atakuwa aliukataa huo ujauzito
Je unafikiri ni wapi mwanaume ataepuka sehemu ya lawama hizi.
Ni lazima na sisi tukubali kuwajibika kwani tunachangia hata kama ni kwa asilimia ndogo tu, lakini tuna mchango katika jambo hilo..........