Wanawake na Simu ya mkononi?

Ndiyo maana huwezi kusikia nimeoa, kwa ajili ya mambo kama haya.

Mimi nataka nipokee simu muda ninaotaka, na nisipotaka nisipokee.

Na hata nikioa ndoa yangu haitabadilisha hilo, unajuaje ma schedule na timetable yangu yanaendaje?

Bottom line ni makubaliano katika uhusiano yakoje, kuna wengine hawataki hata hizo cellphone, sasa kama unataka mtu awe reachable all the time hawa wasio na cellphone utasemaje?

My point ni kwamba hizi expectation kwamba mtu atakuwa reachable all the time bila ya kuongea na kukubaliana hivyo haziko realistic, na mnaweza kuwa mnaji set up for disappointments tu.
Kila la heri dogo...utaweka mikataba mingi sana kwenye maisha yako lol...una muda wa kuweka mikataba mpaka wa kupokea simu ...duh...kweli hiyo sayari mimi niko far from it...

Watu tunanunua simu kwa ajili ya kurahisha mawasiliano yakiwemo mawasiliano rasmi (business, official) na vilevile mawasiliano ambayo siyo rasmi (informal) kama vile family issues, friends, social life...

wewe kila kitu kwako ni formal lazima iwe na mkataba..duh...
 
nyinyi naona mnataka kugeuza wanawake 'watumwa' wa simu zao sasa.

mwanamke yuko nyumbani kwake, mnataka akenda chumbani kupumzika abebe simu, akenda jikoni kupika abebe simu, akenda ****** pia abebe simu!

tofauti na mwanamme ambe mna mifuko ya suruali mnaweka simu zenu saa zote na inawafuata mnapokwenda........wanawake hatuna vitu hivyo....and some of us cant be bothered na 'kutumikia' simu saa zote anyway! (simu yangu iko kwenye silent mode all the time)

ukitaka kuwasiliana na mie mkeo, niwekee simu ya ndani ambayo nitaisikia mlio wake popote nitakapokuwepo nyumbani bila ya kutumikia simu kwa kuibeba saa zote
 
JF napata experience na wife yaani simu ya mkononi mara nyingi iko chumbani, ndani ya begi, etc? huwezi kumpata on time hata kama issue ni very urgent lazima upige kama mara tatu na kuendelea...??
Do you experience the same kwa wake/girlfriends wenu na unashauri nini kifanyika?? inaboa sana hii.
hili tatizo sio la wanawake peke yao! hata wanaume pia wanalo sana! kwahiyo naweza kusema kwamba ni tabia ya mtu tu jinsi alivyojizoesha!
 
Kusema kweli huwa shida ni wapi pa kuweka simu, nikiwa barabarani lazima iwe mkobani na kukiwa na kelele kama zile za k'koo siwezi kusikia, nikiwa nyumbani ndio kabisa nikiwa napika au kufanya kazi za nyumbani simu haiwezi kuwa mkononi na pia nazunguka nyumba nzima mara jikoni mara chumbani kwa watoto mara kibarazani mara msalani nk, ukisema huko kote ninakoenda niwe nimeshikilia simu mkononi ina kuwa taabu kwa kweli

nakubali pia kwamba tukiolewa au kuoa inabidi kupokea simu za mwenzio ili kuwa fair, huwezi kushare maisha na mtu tena wa karibu kiasi kwamba lolote likitokea la emergency wewe ndio wa kwanza kupewa taarifa, etc halafu ukazima tu simu bila kum fahamisha...the same applies kama una watoto, inabidi simu iwe on ili likitokea lolote linalohitaji msaada wako upatikane ki urahisi...labda usiwe na simu, na hata kama usipokuwa na simu lazima iwepo tu njia nyingine ya kukupata haraka

kwa kifupi naelewa point yako Tumain, shida ni jinsi ya kuifanya hiyo simu ya mkononi iwe ya mkononi kweli na siyo ya mkobani au ya juu ya kabati etc
 
Ndiyo maana huwezi kusikia nimeoa, kwa ajili ya mambo kama haya.

Mimi nataka nipokee simu muda ninaotaka, na nisipotaka nisipokee.

Na hata nikioa ndoa yangu haitabadilisha hilo, unajuaje ma schedule na timetable yangu yanaendaje?

Bottom line ni makubaliano katika uhusiano yakoje, kuna wengine hawataki hata hizo cellphone, sasa kama unataka mtu awe reachable all the time hawa wasio na cellphone utasemaje?

My point ni kwamba hizi expectation kwamba mtu atakuwa reachable all the time bila ya kuongea na kukubaliana hivyo haziko realistic, na mnaweza kuwa mnaji set up for disappointments tu.

vizuri sana...maisha ya ndoa sio ya kumfaa kila mtu, wengine huwa wanaingia kichwa kichwa tu, halafu muda si muda wanatoka kwa kasi ya ajabu, kuna watu wameumbwa kuwa bachelors maisha yao yoote!
 
nimekuja kugundua kuwa humu ndani ya JF kuna watu wana ubishi wa UKOO, wa kurithi, yaani hata kama swala lipo wazi ni lazima aligeuze anavyotaka yeye ili aanze ubishi
 
lakini jamani msi-complain sana ni kweli swala la simu ya mkononi kwa kina mama ni issue hivi sometimes mtu unakuwa jikoni uko makini na mapishi simu iko room mpaka ukumbuke eeh naweza kupigiwa ndo utakimbia kuchukua simu hapo tayari ku na more than 4 miss call
Mala unafua ,ogesha watoto we umebebelea tu simu ..hata mie inanitokea mala kibao ila swala la kuzima simu hapana
 
vizuri sana...maisha ya ndoa sio ya kumfaa kila mtu, wengine huwa wanaingia kichwa kichwa tu, halafu muda si muda wanatoka kwa kasi ya ajabu, kuna watu wameumbwa kuwa bachelors maisha yao yoote!

sure Triples
 
tuna-solve vipi hii problem is long overdue.

Nadhani kila mtu ana namna yake ya kutatua hii kadhia, kulingana na mazingira inavyotokea.
Mie kuna wakati nilipiga simu kama mara sita, inaita tu haipokewi. Kuja kuuliza kumbe mtu anafua nje na kaacha simu chumbani kitandani, na issue ilikuwa urgent sana. Nilitoa mkwara kwamba iwapo simu ya mkononi inageuka ya mezani basi kunakuwa hakuna haja ya kupiga. Ikawa nikipiga haijapokelewa basi sipigi tena, na akipiga sipokei. Kitendo hiki cha mimi kutopiga tena wala kupokea simu yake kikawa kinamkera sana hata yeye, akajua uchungu wa kutopokea simu.
Utatuzi ni kwamba alinunua kamba ile ya kuning'inizia, anakuwa nayo shingoni muda wote. Kwa sasa simu zinapokewa kama kawaida, simu haikai katika pochi tena.
IT WORKED!
 
wawekeeni wake zenu sm za ndani.......hapo mtasaidia sana.

wangu mie aliona sipokei simu zake nikiwa nyumbani kaamua kuweka ya ndani sasa hana malalamiko!
 
Nadhani kila mtu ana namna yake ya kutatua hii kadhia, kulingana na mazingira inavyotokea.
Mie kuna wakati nilipiga simu kama mara sita, inaita tu haipokewi. Kuja kuuliza kumbe mtu anafua nje na kaacha simu chumbani kitandani, na issue ilikuwa urgent sana. Nilitoa mkwara kwamba iwapo simu ya mkononi inageuka ya mezani basi kunakuwa hakuna haja ya kupiga. Ikawa nikipiga haijapokelewa basi sipigi tena, na akipiga sipokei. Kitendo hiki cha mimi kutopiga tena wala kupokea simu yake kikawa kinamkera sana hata yeye, akajua uchungu wa kutopokea simu.
Utatuzi ni kwamba alinunua kamba ile ya kuning'inizia, anakuwa nayo shingoni muda wote. Kwa sasa simu zinapokewa kama kawaida, simu haikai katika pochi tena.
IT WORKED!

So it worked finally ah!

Mbona hukutustua/tujulisha?

Hongera.
 
one day yes kuna wanaume wakwale nafanya nao kazi mapema tu saa nne asubuhi mmoja akawa anampigia wife aache maagizo home ..kapiga mala nyingi sana simu haikupokelewa jamaa alilalamika vya kutosha na kudai huyu mwanamama atanieleza alitokea mwelevu mmoja akamwambia wanawake ndo wako hivi kama huamini ngoja nimcall wangu uone akapiga weeeeeeeeeeeeeee ikawa vile vile na mwingine naye akasema na mie ngoja nimjaribu wangu mambo yakawa yale yale ndo jamaa akakamu down
so ni vitu ambavyo vipo na vinatoka hasa na majukumu ya kinamama ,mala aandae chai ,mala akalishe kuku ,mala akakamue maziwa ..mala ....eeh nk nk
 
.....Hili tatizo si kwa sisi wanawake tu, mie my fiance ana hili tatizo.Utakuta nampiga simu hadi nashikwa na hasira kumbe simu kaacha kwenye gari yeye yupo ofisini.
Mie ugonjwa huu kwa kweli sina, kila sehemu ninapoenda lazima my cell phone iwe pembeni yangu, hata nikilala lazima iwe pembeni yangu.
 
Simu za mkononi huwa zina profiles ambazo mtu unaweza kuchagua profile mojawapo kutegemea na mazingira; Noisy environment, Quiet environment, wengine wanaita Discreet, Silent, General, Loud, Light Only na pia unaweza ukacustomize setting zako ukalipa profile jina utakalo. Hii inawezesha kubadili features mbalimbali ikiwemo milio na ya simu na volume zake ili kuweza kuwa reachable ktk mazingira tofauti, kwa hiyo suala la kusema simu ilikuwa chumbani wakati mimi nilikuwa jikoni linatakiwa lisiwepo.
 
Jamani mbona mnaenda mbali sana? Issue hapa ni kuwa simu inakuwa mbali na mhusika si kwamba inakuwa imezimwa au vipi kama nimemwelewa vema mtoa mada. Sasa kisichojulikana hapa ni nini? kina mama na majukumu ya nyumbani kafika mara aangalie watoto, aingie jikoni kupika n.k. saa ngapi atakumbuka kumove na simu jamani? Mimi ni mmoja wao inatengemea siku hiyo nimeshukaje ndani ya gari kama wakati nashuka simu ilikuwa kwenye pochi basi siweziikumbuka hadi baadae sana ambapo naanza kazi ya kureturn missed calls lakini kama nilishuka ikiwa mkononi basi itafikia kwenye meza sebuleni hivyo hata nikiwa jikoni ikiita nitaisikia.

Sisi sio kama ninyi waheshimiwa mkifika home mnafikia juu ya kochi unaanza kuangalia mechi za mpira lazina simu yako uwe nayo
 
Nadhani kila mtu ana namna yake ya kutatua hii kadhia, kulingana na mazingira inavyotokea.
Mie kuna wakati nilipiga simu kama mara sita, inaita tu haipokewi. Kuja kuuliza kumbe mtu anafua nje na kaacha simu chumbani kitandani, na issue ilikuwa urgent sana. Nilitoa mkwara kwamba iwapo simu ya mkononi inageuka ya mezani basi kunakuwa hakuna haja ya kupiga. Ikawa nikipiga haijapokelewa basi sipigi tena, na akipiga sipokei. Kitendo hiki cha mimi kutopiga tena wala kupokea simu yake kikawa kinamkera sana hata yeye, akajua uchungu wa kutopokea simu.
Utatuzi ni kwamba alinunua kamba ile ya kuning'inizia, anakuwa nayo shingoni muda wote. Kwa sasa simu zinapokewa kama kawaida, simu haikai katika pochi tena.
IT WORKED!

simu shingoni inawezekana nyumbani, sasa hapa Bongo kwetu na vibaka wotee hawa mtaani tutoke tumevaa simu shingoni? siku moja si tutarudi nyumbani bila simu wajameni??, na pengine turudi bila shingo kabisa...
 
Dawa ni kumnunulia Twanga pepeta au Philips savy ikiita nyumba nzima wanasikia hata kama kwenye daladala.
 
Simu za mkononi huwa zina profiles ambazo mtu unaweza kuchagua profile mojawapo kutegemea na mazingira; Noisy environment, Quiet environment, wengine wanaita Discreet, Silent, General, Loud, Light Only na pia unaweza ukacustomize setting zako ukalipa profile jina utakalo. Hii inawezesha kubadili features mbalimbali ikiwemo milio na ya simu na volume zake ili kuweza kuwa reachable ktk mazingira tofauti, kwa hiyo suala la kusema simu ilikuwa chumbani wakati mimi nilikuwa jikoni linatakiwa lisiwepo.

Sinkala, labda inategemea na simu na inategemea kuna umbali gani toka jikoni hadi chumbani, kuna simu hata ukiweka sauti ya juu kabisa hailii kama ile ya mezani, na ukiwa kwenye kelele nje unaweza usiisikie...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom