Wanawake na Simu ya mkononi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake na Simu ya mkononi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tumain, Nov 22, 2009.

 1. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  JF napata experience na wife yaani simu ya mkononi mara nyingi iko chumbani, ndani ya begi, etc? huwezi kumpata on time hata kama issue ni very urgent lazima upige kama mara tatu na kuendelea...??
  Do you experience the same kwa wake/girlfriends wenu na unashauri nini kifanyika?? inaboa sana hii.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Very true.....
  Wanawake hawajui
  maana ya simu ya mkononi....
  Baadhi yao.
  Wengi utakuta simu iko jikoni yeye
  yuko kibarazani...
  Wanatia hasira hadi basi...
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  tuna-solve vipi hii problem is long overdue.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  kamanda kama una moyo mdogo unaweza kudhani unamegewa, maana huwaga najiulizaga sana hapa tatizo huwa nini?, hata umwambieje umuhimu wa simu, lakini story ni ile ile,
  siyo nyie peke yenu hata mimi
   
 5. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  I always ask her,hivi hiyo simu yako ni ya kiganjani au mezani?Learn to cope man,u'll never get used to it.

  Wanajua,ni vile tu hatujafahamu why they do that.

  Kumegewa tena... ..mmmh.....huko mbali sana mkuu.

  Kumbe siko peke yangu!I have had my big share of the same. Wakuu ni kuzidi kukumbushana tuu.Sidhani kama unaweza kufanya zaidi ya hilo.Mkumbushe(baadaya ya kumwambia 1000 times jinsi unavyokerwa na katabia haka) tena na tena.
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Tatizo litakuja pale ambapo kwa bahati mbaya mwanadada anapiga simu ya kiganjani ya mwanakaka mara kadhaa afu simu iwe haijapokelewa....atapindiwa midomo na kununiwa mpaka akome ubishi! Mkuki mtamu kwa nguruwe hahaha
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I am a staunch advocate for personal freedom.

  Kuwa na simu ya mkononi maana yake si kwamba upatikane kila nukta.

  Unaweza kuwa na simu ya mkononi na kuamua kuizima wikiendi nzima usipatikane, as long a huna obligations za kukuzuia kufanya hivyo.Swali, je mliwekeana mikataba inayoeleweka na wake zenu wasizime simu zao au kuziweka mbali?
   
 8. M

  Mundu JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Topic au thread hii ni kuwa anayepigiwa simu ni muhusika wa anayepiga. Sasa mpigiwa azime simu siku nzima bila ya upande wa pili kujua kuwa simu imezimwa, lol hapo kuna walakini.

  Pili, tunazungumzia simu zinazoita afu hazipokelewi.
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kumegwa siyo issue kubwa kwangu ila tu unataka kutoa ujumbe fulani au maagizo fulani..dunia imerahisishwa badala yake uta-call mpaka saa nyingine unaamua kuchukua hatua ya kwenda mpaka eneo la tukio say home au business centre..time, money imeshatumika...kukumbusha gani huko bana mimi wananiboa sana!
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  we are talking about marriage life here, kwa hiyo sidhani kama ni busara mke wako akazima simu week-end nzima, eti kisa ni personal freedom, mkataba ni ndoa mliyofunga, we unataka kutuambia kuwa kila kitu mnachokifanya ni lazima mkiwekee mkataba?
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hujajibu swali bado, kuwa katika uhusiano, au hata katika ndoa, hakushurutishi mtu kupokea simu.Kuna wengine hawapendi kupokea simu nyakati zao za kupumzika.

  Swali liko pale pale, kuna makubaliano kwamba simu zote zipokelewe?

  Maana mimi sina makubaliano na mtu kwamba nitapokea simu zote, na mara nyingine nazima simu, mara nyingine sipokei tu, ninaimagine kuna kinadada wengine wako hivyo hivyo, sasa kama hamna makubaliano siwezi kuwalaumu.

  Nauliza, kuna makubaliano ya kupokea simu zote?

  Ndiyo maana wengine hatutaki kuoa, na wengine hawataki kuolewa.Kwani kuna ubaya gani mtu akiamua sitaki kupokea simu saa hizi? Kupokea simu lazima?

  Frankly, hii habari ya kutaka kuwa in touch na mtu 24-7 inaonyesha insecurities tu.
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Makubaliano ya kupokea simu zote? what sijakuelewa? husband na wife waweke makubaliano ya kupokea simu? itakuwa very new innovations sijakupata ndugu??
   
 13. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Bruray,

  Mtoa hoja amezungumzia wewe kumpigia simu mke wako asipokee si kwa kwa sababu ameamua kutopenda kupokea simu ya mtu yeyote (Sidhani kama hii ni kweli kwa mumewe), ila simu iko wazi ila mwenye simu hayuko karibu na simu au ameiweka ndani ya handbag kiasi cha kwamba ikiita hawezi kusikia mlio.

  Frankly speaking, kwa wale waliooa au wenye wachumba, inaweka roho juu sana pale unapotaka kuwasiliana na mke wako/mchumba halafu eti simu inaita bila kupokelewa.

  Kuna kitu tunapashwa kujifunza hapa (hasa kwa akina mama/dada).

  Tiba
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Obviously tunaelea katika sayari tofauti, just because somebody is your husband/ wife haina maana kwamba una m own.

  Kuna wengine kwa sababu mbali mbali muda mwingine wanataka kupumzika na hawataki kusikia mlio wa simu, sio tu kutoka kwa mke/mume, bali pia ndugu jamaa na marafiki.

  Mimi pia nina hiyo formula, nikiamua kupumzika simu naweza kuizima au hata nisiangalie, sasa kama sina makubaliano na mtu kwamba nipokee imu muda wote utanilaumu vipi?

  Hao wake zenu mna makubaliano nao kwamba watapokea kila simu? Maana kama hamna makubaliano mtakuwa mnaendekeza mfumodume tu kwamba "mke wangu lazima apokee simu zote" bila makubaliano, na hapo ndipo mnapokosea, wengine mnapiga simu kila baada ya sekunde mbili, na frankly this is a turn off kwa watu wengine hawapendi.

  Ndiyo maana nikauliza mna makubaliano?

  Kuoana haina maana ya kuununua uhuru wa mwenzako.
   
 15. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280

  Mkuu this is too academic which doesnt exist in the real world we live in? KWAMBA ETI MNA MKATABA? Hapa tunaongelea watu kwenye mahusiano..ambao they owe obligations to each other..to make life move...

  Personally, huyu mleta hoja nimemuelewa. Nina rafiki yangu, hiki kitu ndo nadhani kinamgombanisha sana mara kwa mara na mke wake. Anapiga simu...kumbe handset iko jikoni au kwingineko..she simply doesnt care--If I may say so.

  Mkuu kama umeoa hakuna tena issue za mkataba au nini..its just point ya mawasiliano. Mfano..wewe uko kazini...mwenzio yuko nyumbani..na mlikubaliana wewe utawapitia watoto shuleni jioni...ghafla ukapata dharura..sasa ukimpigia wife akawachukue watoto..huoni kwamba usipompata utakuwa umeharibu mambo? mifano ni mingi....

  Katika dunia tunayoishi..hoja zako haziko practical.

  Unless uniambie kwamba hutaki kuwa na simu kabisa. (Personally mimi sina simu ya mkononi!) Nikikuhitaji nitakutafuta. Na wala si kwamba niliamua hivyo kwa nia mbaya au anything..ni uamuzi tuu..sitaki kuwa na simu ya mkononi. Simple.

  Masanja
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hili ndilo tatizo,

  Mnaingia katika mahusiano bila mkataba wala makubaliano kwamba simu zote zitapokelewa.

  Halafu simu zikichuniwa mnakuja kulalamika.

  Kweli sawa hiyo?

  How can this be too academic wakati mimi nishakupa real life experience kutoka maisha yangu mwenyewe?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Nov 23, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Bluray...mkataba wa nini kwenye mahusiano ya kindoa? Vitu vingine ni common sense tu na kuleta mambo ya mikataba ya kijinga kijinga ni ku complicate mambo. Masanja hapo katoa mfano mzuri kabisa. Mke au mume anapokupigia simu siyo mara zote anataka kujua uko wapi na unafanya nini. Inawezekana kabisa mwenzako akawa kapatwa na dharura. Vipi kama mtu gari yake imeharibika na amekuwa stranded? Hivi utamweleza na akakuelewa kweli kuwa alikuwa anajaribu kukupata lakini wewe ulikuwa hujisikii kupokea wala kuongea kwenye simu? Talk about vyanzo vya ugomvi and look no further than this.....
   
 18. m

  mkulu Member

  #18
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bluray naona ameamua tu kubisha .... kila kitu kiko wazi hapo na kinaeleweka!!
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Bluray hana mke, hivyo ni vigumu kwake kuelewa tatizo hili. Hili tatizo lipo na nahisi litaendelea kuwepo... Wengine hupenda tu kukuta kuna miss call ngapi kwenye simu zao ama kuna msg ngapi...
   
 20. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maana huwezi kusikia nimeoa, kwa ajili ya mambo kama haya.

  Mimi nataka nipokee simu muda ninaotaka, na nisipotaka nisipokee.

  Na hata nikioa ndoa yangu haitabadilisha hilo, unajuaje ma schedule na timetable yangu yanaendaje?

  Bottom line ni makubaliano katika uhusiano yakoje, kuna wengine hawataki hata hizo cellphone, sasa kama unataka mtu awe reachable all the time hawa wasio na cellphone utasemaje?

  My point ni kwamba hizi expectation kwamba mtu atakuwa reachable all the time bila ya kuongea na kukubaliana hivyo haziko realistic, na mnaweza kuwa mnaji set up for disappointments tu.
   
Loading...