Wanawake na Kununa/Kususa

halafu wanafanana kweli wakiwa wamenuna,
lol...sijui ndo nature?
Kuna wengine hawanuni wakagoma kusema tu , unakuta limama limenuna hata kupiga msuwaki halitaki eti linakukomoa usiombe denda. khaa! wanawake ni kipimo cha uvumilivu bana
 
Hii post yangu ya mwaka maana nakumbuka my wife alivyokuwa na mimba alikuwa anapenda vile vimishikaki vya vijiti vinavyouzwa stand kwenye vumbi na majivu kibao asipokula hivyo vi nyama ananuna nimekumbuka mbali sana ila sasa eti nikimkumbusha sasa hivi ananuna wanawake nyie
Vile vimishkaki vya paka eee!! nasikia wanakamata paka wazururaji wanachinja then wanauza nyama hivo navo nimevila sana, na sharti lake lazima niingie kituoni, imagine kituo kama mwenge kinavyokuwaga jioni.jasho jembamba linanitoka nakula mishkaki kama thetasini hv huwa vidogo kama punje ya karanga
 
Lakini Gaga unaweka hiyo minuno yako,
kwakuwa wa kumnunia yupo karibu, na yeye actually ameiaccept hiyo minuno,
kwa wengine usithubutu kabisa kununa, utajuta!!!!!!!!
utapotezewa si kitoto!!!!!!!!!!
Unaangalia situation unafikiri unanuna tu ovyo, unajua kabisa hapa nikinuna nitabembelezwa, ila kwa ukweli katika maisha ya kawaida huwa sina tabia ya kununa kabisa, yaani naweza kujifanya nimekasirika na kununa ila nikilala najikuta nimemkumbatia na kwa vile anajua amekosa atajituliza tuliii, nikistuka na kukumbuka nilikuwa nimekasirika inakuwa too late
 
Okada naona hapa ndo pale ile post ya kutingisha vibiriti inaaingia kabisa....lol

Mara nyingi inakua tu kutaka attention ya huyo mwanaume, bahati mbaya sana
ni kua guys wanaweza vumilia siku za kwanza akakubembeleza kama ulivyo taka
then siku zikizidi kwenda hatimae anachoka and does not give a damn umenuna/susa...

Kununa kila saa na kususa yaani mara kwa mara ni moja ya qualities ambayo
humfanya mwanamke apunguze mvuto na mapenzi kwa mwenza wake ila bahati
mbaya saana wadada wengi tufanyao hivyo hatuelewi ilo suala...
Kwa kweli dada Umeongea.
Unabembeleza mpaka unachoka kila siku zinaposogea.shida sasa akizoe hiyo Kudeka na kusikilizwa.
Juzi tu nimevunjiwa simu, eti hao wanaonipigia simu ndiyo wanafanya siku hizi me nisimsikilize na kumdharau, mpaka kakonda kwa fikra za kijinga,jamaani!!
yaaani ananikera sana, mpaka marafiki wananipa pole na siku hizi wameamua kumuita wife wangu PASUA KICHWA!!
 
Vile vimishkaki vya paka eee!! nasikia wanakamata paka wazururaji wanachinja then wanauza nyama hivo navo nimevila sana, na sharti lake lazima niingie kituoni, imagine kituo kama mwenge kinavyokuwaga jioni.jasho jembamba linanitoka nakula mishkaki kama thetasini hv huwa vidogo kama punje ya karanga
<br />
<br />
Gaga umeniua leo yaani umemchekesha my wife hapa anasema kumbe mko wengi
 
Wana JF, hebu nisaidieni. Kwa nini wanawake wengi huwa tunakawaida ya kuwanunia/kuwasusia wanaume/marafiki zetu? au ndio dalili ya mapenzi? Hii hata kwenye cinema utaiona sana, mwanamke anajifanya kununa/kususa na kuja na mkiwara mingi kama anataka kitu kwa mwanaume! Akikipata, basi utaona anacheka, anaona raha kubembelezwa kama mtoto!

Mbaya zaidi kwenye ndoa, hasa wa wale wenzangu wasiopenda kuambiwa ukweli, wale wanaojiona kuwa kila wakati wako sawa, basi wakirekebishwa/au kushauriwa na waume zao utawakuta wamevuta midomo hao! Kisa mwanaume hamsikilizi na kwa wanawake wengine, ni kama vile hawapendwi! mmh jamani hapo huwa nakwama, kwani mwanaume kukupenda ni yeye kukubakli kila unalosema wewe na akiwa tofauti basi umenuna? Mmh .....

Hapo kwenye bluu hapo jamani umepiga Ikulu. Yaani katika vitu vinavyonikera katika mahusiano ni exactly hicho ulichoandika hapo kwenye bluu. Ni mara mia ya mwanamke anayependa sana shopping kwa kuwa pesa zinatafutwa, tutatafuta kuliko mwanamke ambaye ni UNREASONABLE! Yaani kununa nuna tu! Aaaagh!!
 
Hahahahahaah! AshaD umenikumbusha kitu hapo kwenye bold, kuna wakati nilikuwa mjamzito nilikuwa nina tabia za kununa sana, basi nikawa nikinuna kama nimelala nae kitandani nahamia chini kwenye kikarpet nalala na yeye baada ya muda kidogo anakuja hapo chini tunalala wote huku ananibembeleza,
Sasa ikawa mazoea yangu nikikasirika naenda chini anakuja siku ingine nakubali kurudi kitandani na siku ingine nagoma na yeye hana budi kulala na mimi hapohapo mpaka asubuhi. Siku ya siku ikafika kama kawaida nikajinunisha nikalala chini, eeeeeh nikaanza kusikia mkoromo, nilivochungulia akawa amelala, yaani nikazidi kuvimba huku najifanya kupiga mihayo na kelele ili aamke wapi? baada ya masaa matatu mwenyewe niliamka chini nikajirudia kitandani tangu siku hiyo sikufanya tena na wala hatukuliongelea hilo lol!

Hahahahaha! Hiyo kali, kununa is fine ili isizidi sana jamani kina dada khaa! Yaani sasa mpaka inakuwa kero!
 
Kwa kweli dada Umeongea.
Unabembeleza mpaka unachoka kila siku zinaposogea.shida sasa akizoe hiyo Kudeka na kusikilizwa.
Juzi tu nimevunjiwa simu, eti hao wanaonipigia simu ndiyo wanafanya siku hizi me nisimsikilize na kumdharau, mpaka kakonda kwa fikra za kijinga,jamaani!!
yaaani ananikera sana, mpaka marafiki wananipa pole na siku hizi wameamua kumuita wife wangu PASUA KICHWA!!

Aisee pole sana mzee. Hapo sasa inakuwa siyo kununa tena bala ni mwanamke kuwa UNREASONABLE, hiyo ni kero kubwa sana kwangu!
 
Kuna zile za kununiana siku nzima, halafu usiku wa manane unaota unakula uroda 'bab kubwa!,'
kufumba na kufumbua unashtuka usingizini wewe na mamsap mmebanana ndivyo sivyo kiasi kwamba inabidi muendelee tu..
he he he...maisha haya! ...6"6 oiyeee!!!
 
Mwanamke siku zote ni mtu wa kupenda care, achilia mbali hisia zake kwa mwanaume wake. Hununa kumfanya mwanaume wake awajibike kwake!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom