Ni bora uolewe Mke wa pili na Mwanaume mwerevu kuliko ujitie kuolewa kama mke mmoja na Mwanaume asiyejielewa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
12,827
29,217
NI BORA UOLEWE MKE WA WAPILI NA MWANAUME MWEREVU KULIKO UJITIE KUOLEWA MKE MMOJA NA MWANAUME ASIYEJIELEWA!

Anaandika, Robert Heriel.

Angalizo; Ujumbe huu utawahusu binti zangu tuu, na wanawake wote werevu ikiwapendeza wafuate maneno yangu. Hivyo ni kusema ujumbe huu sio wa watu wote.

Taikon Hana shida na ndoa za mitara, binti yangu usiogope ndoa ya wake wengi Ila ogopa mwanaume asiyejielewa.
Mwanaume asiyejielewa hata akuoe wewe pekeako na asichepuke bado atakufanya usijisikie furaha katika maisha yako. Ataondoa sababu ya wewe kuishi Duniani, hutaona raha hakika nakuapia binti yangu.

Ni Kheri uolewe na Mwanaume Mwerevu hata Kama ni mke WA kumi huko, usijali huyo atakupa furaha wewe na watoto wako.

Mwanaume asiyejielewa hajui thamani yako, na Kama hajui thamani yako kamwe hawezi kujua namna ya kukupenda. Namna ya kukupa furaha.

Mwanaume asiyejielewa atajali zaidi watoto wake huku akisahau wewe ndiye uliyemzalia. Hataona shida kukunyanyasa kisa watoto uliomzalia.

Ni Kama Mwanamke asiyejielewa pia, atawajali na kuwapenda watoto kuliko amjalivyo na kumpenda Mume wake.

Ni kweli wanaume ni wachache kuliko ninyi wanawake, tena katika haohao wachache kupata mwanaume Mwerevu pia ni shughuli pevu.

Sasa basi ukishakutana na Mwanaume Mwerevu, ukajiridhisha kuwa huyu ni Mwerevu, huyo mpende na mkabili bila kujali Status yake, iwe ameoa au hajaoa, iwe anawatoto au Hana watoto.

Hakuna sheria inayokataza wewe kuolewa mke wa pili iwe Kidini au kidunia. Sheria zinasema usitamani mke WA jirani yako, na haisemi usitamani mume WA jirani yako. Mume hamilikiwi, mume anayoruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja.

Linapokuja suala la maslahi yako kama mwanamke usifikirie jamii itakuonaje, Ila fikiria wewe na watoto wako utakaowaleta watakuchukuliaje.

Binti yangu, najua sasa hivi bado ni mdogo, Pengine ukaona Baba yako nimezeeka au nimetumia Mvinyo ndio maana naongea haya, Ila ukikua kidogo na unaingia katika ndoa utaelewa Baba yako nilikuwa nasemaje.

Binti yangu, ukiwa unachagua Mume WA kumuoa hakikisha unafikiria zaidi watoto utakaowazaa ambao muda huo hawapo. Hao ndio uwafikirie Kwanza kabla hujafanya maamuzi. Usiendekeze ubinafsi wako ukaathiri watoto.

Mtoto ni Wamama akiwa Mpumbavu na akiwa hajielewi.
Mtoto huwa wa wote(yaani Baba na Mama) akiwa Mwerevu na anajielewa.

Kadiri mtoto akiwa Mwerevu ndivyo anavyoimarisha ukaribu wa Mama na Baba.
Kadiri mtoto anavyokuwa mpuuzi ndivyo anavyozidi kuzorotesha ukaribu wa Mama na Baba.

Hata hivyo, Maamuzi ni yako binti yangu. Sikuchagulii maisha, Ila wajibu wangu kama Baba ni kukuongoza na kukushauri katika njia iliyonjema. Baba mwema hupenda mafanikio ya binti yake.

Mimi Baba yako unaniona ni mkali, kuna wakati unanichukia lakini ni Kwa ajili yako binti yangu. Sipo hapa kukudekeza ili uje uharibike huko Baadaye.

Mwanaume Mwerevu ukizaa naye hata mkiachana kamwe hawezi kukuchukia, atakusaidia wewe na mwanao, atavumilia na kukuelewa mapungufu yako ya hasira na chuki. Hatajali hivyo kwani anakuelewa, atakusaidia iwe Kwa ukali au Kwa upole lakini atakusaidia wewe na mwanao.

Lakini ukizaa na Mwanaume Mpumbavu na asiyejielewa hata Kama anauwezo WA kifedha jua umeumia binti yangu, utateseka Sana, dunia itakusonda vidole na hata yeye mwenyewe anaweza kukusonda vidole na kukukera, hatajali hasira na chuki zako kwani hajui wewe ni mwanamke, hajui wanawake huongozwa na hisia hivyo kukasirika na kuchukia ni rahisi pale wanapouziwa au kupatwa na Jambo baya. Yeye hatajali hivyo.

Hatajua kuwa wewe ni Mama wa m/watoto wake hata Kama mmeachana.

Mwanaume Mwerevu atakuchukulia wewe Kama mtoto wake, atakuwa kwako Kama Baba, nawe utakuwa binti yake hivyo atakuvumilia na kukustahi, atakufundisha Kama mtoto, akikuelekeza na wakati mwingine akikuadhibu Kwa upendo,

Lakini mwanaume asiyejielewa atakuchukulia wewe Kama Mkubwa mwenzake, atakuwa mtu wa kukulaumu na kukukaripia Kwa sababu hajui saikolojia ya wanawake ilivyo.

Ataona mambo mengi unafanya makusudi kumbe ni kweli wakati mwingine unasahau. Badala ya kukufundisha yeye atakulaumu na kukutukana. Badala ya kukuadhibu Kwa upendo, yeye atakupiga Kwa kukukomoa Kwa hasira akilenga kukuharibu.

Mwanaume Mwerevu kwako atakuwa kama mwalimu. Ukikosea Kupika au Jambo lolote, basi yeye atafanya badala yako Jambo lilelile ulilolikosea, kisha atakuambia hivi ndivyo inavyofanywa, kisha atakufundisha mpaka uhitimu.

Lakini mwanaume asiyejielewa ukikosea ataanza kukulaumu na kukutukana au kununa nuna Kama Mwanamke(asijue yeye ni mwanaume), wengine hufikia hatua wanatukana mpaka wazazi wako. Asijue Kwa wazazi wako uliishi Kama mtoto na sio kama mke, na hapo kwake utapaswa uishi Kama mtoto ili uwe mke bora.

Mwanaume asiyejielewa hutishia kila mara kukufukuza kumaanisha kwake yeye, wewe mi Stranger tuu.
Lakini Mwanaume Mwerevu hawezi kukawambia maneno Kama hayo isipokuwa kukukumbusha ahadi yake kwako ya kuishi na wewe siku zote za maisha yake labda kifo kiwatenganishe, au Siku utakayomsaliti na kusex na Mwanaume mwingine ndio siku mtakayoachana.

Mwanaume Mwerevu ni lazima Ajue kukabiliana na mapungufu na tabia zako mbaya ili kuzirekebisha kwa vile anakupenda kasoro tabia moja ya usaliti wa kutoka nje ya ndoa.

Mwanaume Mwerevu kamwe hawezi kukusamehe siku utakayomsaliti na kutoka na Mwanaume mwingine.
Lakini mwanaume asiyejielewa anaweza kukusamehe kutokana na kutokujiamini kwake, na ujinga wa kutokujua kufanya maamuzi sahihi.

Binti yangu, ukiona mwanaume amekufumania na akakusamehe jua huyo hakupendi, na hajielewi, yupo kwako Kwa sababu zingine lakini sio Upendo,

Mwanaume anayekupenda Ile yenyewe siku ukim-cheat alafu akajua ndio siku hiyo hiyo atakuchukia kuliko mtu yeyote Yule. Na Kama hatakuwa mwangalivu wa kujitawala anaweza kujidhuru au kudhuru watu wengine.

Mwanaume Mwerevu atakupa nafasi kwenye Moyo wake kadiri wewe umpavyo nafasi katika moyo wako. Ukimpa namba moja naye atakupa namba moja, ukimpa namba mbili naye atakupa vivyo hivyo.

Mwanaume Mwerevu kamwe hawezi kupambana na wewe Kama mkewe Ila atakufukuza tuu, na ukiwa mkaidi basi atakuondosha.

Lakini mwanaume asiyejielewa hupenda kushindana na wanawake, kuwekeana Ligi zisizo na maana, kususa, kununa nuna kama mtoto wa kike.

Mwanaume Mwerevu atajua namna ya kukubembeleza na kukutuliza hata Kama unahasira au umenuna kiasi gani.
Mwanaume asiyejielewa yeye kubembeleza atachukulia Kama kujidhalilisha, kujishusha ilhali yeye ni mwanaume tuu, anashindwa akili hata na Jogoo.

Mwanaume Mwerevu Kama hajaoa au hajawahi kuoa kamwe usiruhusu akuoe ikiwa wewe unamtoto/single mother. Hawezi kuwa Mwerevu huyo, na hajatumia hisia zaidi kuliko Akili.

Usitegemee furaha kwake Kwa maana bado ni mchanga, Kama bado hajawahi ishi na Mwanamke na kumlea hiyo mwanamke kama mtoto wake, atawezaje kumuoa na kuishi na Mwanamke mwenye mtoto asiyewake akavumilia mapungufu ya wewe binti yangu na mwanao?

Binti yangu, niishie hapa, usisahau na Maneno mengine niliyowahi kukupa.

Eid Mubarak!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
10,414
14,330
NI BORA UOLEWE MKE WA WAPILI NA MWANAUME MWEREVU KULIKO UJITIE KUOLEWA MKE MMOJA NA MWANAUME ASIYEJIELEWA!

Anaandika, Robert Heriel.
Wife namuambiaga kabisa kwamba mimi mke nitaongeza ila siwezi kuongeza mke wakati yeye hali bata.

Nataka mimi niongeze mke wakati nina vyangu na mke mkubwa anakula kuku wa kutosha apunguze stress za uke wenza.

Wake wengi ukiweza hata wanne unakuwa nao,alafu raha uwe 30-45 hwpo unakuwa na maguvu ya kula mzigo sawasawa.

Sio unaona wakw wengi una miaka 60 alaa
 

Akili 2

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
897
1,054
NI BORA UOLEWE MKE WA WAPILI NA MWANAUME MWEREVU KULIKO UJITIE KUOLEWA MKE MMOJA NA MWANAUME ASIYEJIELEWA!

Anaandika, Robert Heriel.

Angalizo; Ujumbe huu utawahusu binti zangu tuu, na wanawake wote werevu ikiwapendeza wafuate maneno yangu. Hivyo ni kusema ujumbe huu sio wa watu wote.
Ooohh ukianza kuwaelewa wanawake wanataka nn just unaelekea kufa
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
12,988
23,252
Tangu nimeanza kukiri kuwa nina mke, nachinja watoto kama vile hakuna idadi…. mwanamme usiogope kuambia demu kuwa umeoa inaongeza thamani yako kwake.
 

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
12,827
29,217
Tangu nimeanza kukiri kuwa nina mke, nachinja watoto kama vile hakuna idadi…. mwanamme usiogope kuambia demu kuwa umeoa inaongeza thamani yako kwake.

Wanawake hawapendi mtu asiye kwenye mahusiano, wanapenda kuchukua vilivyomilikiwa.
Hapo ndio hujiona washindi na wanajiamini.

Ukisema upo single mwanamke anajiuliza Kwa nini huna mtu, kwamba hupendwi, anaangalia kasoro zako zaidi kuliko ubora wako.

Ukisema Una mke au mchumba anaangalia ubora wako zaidi kuliko madhaifu, ataangalia ni vitu gani vimemfanya huyo Mchumba au mke uliyenaye akukubalie.
 
9 Reactions
Reply
Top Bottom