Mama watoto wangu
Kaunga ,listen my dear.Binadamu mpaka amekua na ustaarabu amepitia katika stages tofauti tofauti japokua kuna tofauti ya ustaarabu wa mtu au jamii moja au nyingine.
'
Lakini mama,tunasahau kuwa kuna kanuni na sheria zinazoendesha ulimwengu huu na kanuni hizi hazibadiliki na ndizo zinazosimamia kila kitu.Kujiheshimu ni moja ya kanuni ya binadamu kutoka kwenye kanuni hizi zinazoendesha ulimwengu huu.
'
Kanuni hii haibadiliki kulingana na jamii bali ni kwa jamii zote za binadamu.Na kujisitiri ninakokuzungumzia hapa kunaeleweka,ndio maana mtu anapoamua kuwa wa dini hakuna anaemuambia namna ya kujisitiri,ANAJUA.
'
Kujua huko kunatoka kwenye kanuni hizo.Hakuna jamii isiyojua namna SAHIHI ya kujisitiri ndo maana Sylivio Berluscon aliwahi kuhoji tofauti ya mavazi kati ya kahaba na asie kahaba!
'
Hata hawa wanaopinga hapa namna sahihi ya kujisiti wanajua ila wanabisha tu.
'
Hivyo ninaposema kuwa binadamu ni kwa mujibu wa kanuni na sheria za ulimwengu au maumbile.
'
Kuwa binadamu kuna maana ya kujiuliza kuhusu sisi pamoja na mazingira yanayotuzunguka
'
Binadamu amepitia katika hatua hizo za kujiuliza na zama damu ni mojawapo,yale yaliyofanywa wakati ule japokuwa ni ya kijinga hayakumbadilisha binadamu asiwe binadamu bali kwa kuwa alikuwa anaendelea kujiuliza hatimae ameondoka kwenye huo ujinga,tatizo kuna watu wanataka kuturudisha kwenye zama za kijinga wakati tumeshatoka huko.
'
Ni sawa na mtu aje akuambie utumie barua badala ya sms!
'
Binadamu tangu kale amekua kama vile mtu anapozaliwa na hatua za kuelekea utu uzima,ulipokuwa mtoto uliyafanya ya kitoto na hakuna aliyekushangaa,tatizo unapokuwa mtu mzima na kuyafanya ya kitoto.
'
Na tatizo linaongezeka pale watu wazima wasipokuuliza kulikoni.Kuacha kuhoji ni kuwa sehemu ya tatizo.
'
Asiejiuliza ni mbuzi pekee!