Wanawake mnaweza kujiuliza hili!

Wanawake mnaweza kujiuliza hili!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Nipo Nyerere road hapa katikati ya Jiji la Mwanza.Hapa nilipo kuna wadada wawili wote wameolewa na wamevaa sketi fupi sana.Kitendo hiki kinanifanya nijiulize maswali yafuatayo.Kwanza nikiri kuwa huu ni muendelezo wa wanawake kuvaa nguo za ajabu ajabu bila kujali wameolewa ama la.
'
Hivi mwanamke ambae ameolewa kwanini anavaa nguo za kuonesha maungo yake?
'
Sihalalishi mwanamke alieolewa kuvaa hivyo kwa kuwa sina mamlaka hayo,lakini pia huenda ambao hawajaolewa wakawa wanaonesha matangazo ya "biashara"!
'
Lakini inakuaje pale unapoifanyia maonesho biashara au bidhaa ambayo tayari imeshanunuliwa?
'
Au kuna sababu ya wake za watu kuonesha maungo yao?
 
Hivi kumbe mwanamke ni kama duka..., lazima lifunguliwe kuonyesha bidhaa ili kuvutia wateja..!?
Wengine kuvaa nguo fupi ni kupenda awe ameolewa au hapana.
Nilibahatika kushuhudia mdada aliyevaa nguo fupi (Arusha mjini) akizomewa na kumwagiwa maji machafu! Alidhalilishwa na kudhalilika sana ila nadhani atakuwa hajarudia kosa kwa sababu alipata fundisho maishani kwake.
 
Mavazi yana potray character ya mtu.Huna haja ya kuhangaika nao hata kama amevaaje,just ignore them na ufanye mambo yako ya muhimu tu coz mnavyozidi kuwatolea macho ndivyo wanavyozidi kurudia wakijua wamekamata concentration yenu.Mtu na heshima zako kwa nini uvae mavazi yanayokudhalilisha??
 
kama nguo alieivaa yuko okay nayo na anajisikia vizuri mtu mwingine anakereka nini?!....standards hizo za mavazi haya yanafaa haya hayafai kaweka nani?!
 
Kama mumewe hajamkataza acha avae, pengine wote wanapenda.

Binafsi sidhani kama kuna umuhimu wa mtu kukereka na mavazi ya mtu mwingine ambae hamhusu hata kidogo (sio mke, ndugu wala rafiki yako) maana kila mtu na mambo yake. Wewe unayoyaita maadili pengine mwenzio hayajui wala hayamhusu, kimaadili kwao wanafunga kaniki fupi tu chini na maziwa wanaacha wazi. Leo hii anakuja mjini, anajitahidi kujifunika kwa kiasi chake we unamsema kuwa anaenda KINYUME na maadili bila kufikiria kwamba maadili yako sio lazima yawe yake yeye.
 
kama nguo alieivaa yuko okay nayo na anajisikia vizuri mtu mwingine anakereka nini?!....standards hizo za mavazi haya yanafaa haya hayafai kaweka nani?!

yuko okey nayo??????? Wakati akija kukaaa anafunika na kimkoba chake??
 
Jijini joto kali jamani mbona mnawasema vibaya wake za watu?Je mkijua zaidi ya hizo nguo si ndio mtabaki midomo wazi,maana kutokana na joto wengine wameamua kutovaa ch.....kabisa ili kuendana na hali ya joto kali.
 
Kama mumewe hajamkataza acha avae, pengine wote wanapenda.

Binafsi sidhani kama kuna umuhimu wa mtu kukereka na mavazi ya mtu mwingine ambae hamhusu hata kidogo (sio mke, ndugu wala rafiki yako) maana kila mtu na mambo yake. Wewe unayoyaita maadili pengine mwenzio hayajui wala hayamhusu, kimaadili kwao wanafunga kaniki fupi tu chini na maziwa wanaacha wazi. Leo hii anakuja mjini, anajitahidi kujifunika kwa kiasi chake we unamsema kuwa anaenda KINYUME na maadili bila kufikiria kwamba maadili yako sio lazima yawe yake yeye.

hapa tunakuja kwenye kitu cha ethics, kwamba values zinainvolve choice, ethics standards zina change within time, na kwamba unachokiona kizuri mwenzio anakiona kibaya.. All in all utandawazi
 
kama nguo alieivaa yuko okay nayo na anajisikia vizuri mtu mwingine anakereka nini?!....standards hizo za mavazi haya yanafaa haya hayafai kaweka nani?!

Daaaaahhhhh!!
 
Utandawazi. Ila kusema la ukweli wanapendeza sana na ndiomaana wanaume hudindisha mihogo yao. Kama unavyofahamu mwanamke ni ua bwana

Ama kweli kukua kwingi kuona Mengi!
 
mtoa mada hajasema walifunika na mikoba.....na si kila anayevaa nguo fupi anajifunika na mkoba akikaa....
ovious kumbe hujawi ona... Kila avaae nguo za namna hiyo, akikaa lazima kipima joto kifanye kazi ya kufunika.. Si mpaka mtoa mada aseme mkuu
 
kila anayevaa?!??....you are totally wrong......maybe in your society but in mine hell nooo.....
 
mitazamo waliyonayo baadhi yao kwa kufikiri kuvaa nguo fupi ndio kupendeza ...thats all!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom