Huo si utandawazi bali ni UTUNDUWAZI.
Msichoelewa mitandao karibuni yote kama Facebook, Instagram, Telegram, Twitter, Imo, Badoo n.k huhusika kutangaza huo ufuska (pornographies/picha na video za ngono "X") kwa 90%.
Nashukuru sana Mungu kunipatia upeo wa kutohusika na hizo inshu tangu 2012 nilikuwa natumia WhatsApp, Google, You Tube, Sky sports na Goal.com kwa kuingia kujifunza maarifa ya kidunia kama kusoma Encyclopedia, Afya, habari za michezo n.k.
Nikikuona hueleweki kwenye himaya yangu naku-block na kufuta kabisa no yako kwenye diary au email account ya Google.
2017 nikaelimishwa na Jamaa mmoja kuwa JF inajielewa kama wakiona kuna upumbavu umetumwa wanakupiga ban ndiyo nikaanza kutumia JF na kuwa Mraibu hadi sasa hivi.
TV pia zidhibitini kwa Watoto kuangalia miziki ya wanaocheza uchi na makatuni yanayotangaza ushoga.
Kupanga ni kuchagua, maisha ni wewe mwenyewe unavyoyaishi.