Wanawake,mabint mlioolewa,ambao hamjaolewa je hii ni sawa??

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,713
Kuna mzee nilikutana nae kwenye basi nikielekea Mwanza kutoka Arusha, katika stori nikajikuta namuuliza yule mzee, nikija kuoa ili ndoa yangu iwe na amani nifanye nini?

Akanijibu kuwa;
Ukija kuoa mjukuu wangu jitahidi kumjali, kumpenda na kumheshimu mke wako na zaidi ya yote mwache awe yeye usitake awe mwanamke unaemfikiria kwenye mawazo yako, ukapelekea kutaka kumbadili.

Utasambaratisha ndoa!!
 
mh! kuna ukweli hapo ila sasaaa.., dah?
Anywy, mungu naomba unibariki na unipitishe salama hapa kwene hili suala la ndoa.
 
ukweli mtupu
ni vigumu kumbadilisha mtu mzima completely awe vile unavyotaka
wengi hufeli,wachache sana hufaulu,na wengine wengi hujidanganya kuwa wamefaulu
kumbe ukweli mdada anapretend tu kuwa vile wewe unapenda
Hawezi kuishi na pretence maisha yake yote so matokeo yake
atarudi kuwa yeye...HAPO NDIPO AMBAPO WANAUME WENGI HUSEMA......
.............. I WISH I KNEW !!!!!................
 
Una busara kuliko huyo babu.
 
Vipi huyo mzee hakusema chochote kuhusu nyumba ndogo na vidumu?!, maana hiyo kitu ni tata, kuna watu wanaishi vizuri sana kwenye ndoa zao lakini huwa wanachepuka kwa siri sana
 
Ooh kumbe hiyo ndo siri ya mafanikio, ni nzuri sana , mh lakini kunavitabia lazima virekebishwe jamani.
 
Sasa kama mkeo ni mtu wa kujirusha maana yake umwache tu aendelee kuwa hivyo!!! kuna vitu lazima kurekebishana baadhi ya vitu ili tabia zenu hizo mbili ziweze kuwezana.
 
Hata mimi pia niliukubali huo ushauri ni mzuri sana!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom