Wanawake kuweni na huruma, mchumba hasomeshwi

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,037
71,271
Huyu ndugu yangu ambaye kwangu ni kaka, alikapata kadem kakiwa kidato cha nne kakawa kamefaulu ushindi wa kukapeleka vyuo vya kati.

Jamaa akafanya mpango, akakatafutia shule ya private, kidato cha tano mpaka sita, huku akikalipia ada, na mazaga zaga kama yote kakafaulu nakuingia chuo kikuu.

Jamaa akatambulisha kale kadem kwa akina familia zetu na ukoo kwa ujumla. Demu akaingia chuo kikuu fulani hapa nchini kwa bahati mbaya hata mkopo akakoswa. Jamaa akaendelea kulipa ada, na gharama zoteeee kwa huyu mke mtarajiwa

Mwaka jana, mwezi 8 tukaenda kutoa kishika uchumba kwao na mwanamke! Kumbe demu alivyokua pale chuo, akaanzisha mahusiano mapya na mkufunzi wake

ndugu zangu, juzi ,juzi juzi hiii ya jumatano, huyu mkufunzi kaenda kutoa mahali kimya kimya kwao na demu na wameipokea milioni 2.

Hata sisi kujua, tumejua kwa bahati bahati tu maana walitaka iwe siri. Kwa kuzingatia muda na pesa alotumia kama sehemu ya uchumba huyu kaka yetu

Ushauri wenu hapa, utasaidia lakini ushauri wenu uegemee mambo mawili tu

1- Kisheria, unawezaje kupata fidia? Maana miaka mitano sio mchezo

2 - Ni adhabu ya kijadi/kiganga tumpe huyu mbwa? (Binafsi niliwaza tumfanye awe malaya kwelikweli au tumpe mkosi ambao hatokaa kupata mume)

Haiwezekan awafadhaishe sana wazazi wetu, na kutia aibu. Unyama unyama, haki ni mbinguni.

Mrejesho nitawaletea!
 
Kisheria hakuna adhabu inayomhusu kwakuwa alikuwa mchumba tu.

Huyo jamaa aweke akilini kuwa alikuwa anamsomesha mtoto yatima. Atapata thawabu kwa MUNGU

Usahuri wangu: Jamaa akubali kumuacha aolewe, wala asimchukie. Kwakuwa Demu ataolewa na mtu mwenye fedha, jamaa ageuke kuwa X awe anapiga mechi za ugenini kisha atumie akili kidogo tu, fedha zake zote alizotumia kumsomesha ataona zinarudi. Tena huyo Binti anaweza hata kumbebea Mimba akiwa hukohuko kwa mumewake.

Wanawake akili zao ni tofauti na sisi wanaume tunavyowafikiria.
 
Uzi wako utasababisha watu waache kuwatunza wachumba wao
Hawa viumbe sio wa kutunza kama Mke au kichumba.

Wee ukiwa naye Piga, kwenye kumsaidia wee kua kama unahonga.

Usifanye Uwekezaji yakwamba nahurumia Mke mtarajiwa.
 
Kisheria sidhani kama kuna msaada, ila kwenye hiyi option ya pili yapo mengi tu yanayowezekana na kwakua anaefanyiwa hatakuwa ameonewa, basi atazunguka mpaka anazeeka.

Jamaa kazingua sana kusomesha mwanamke, ila hiyo isiwe sababu ya kuacha kukomesha hizi tabia.

NB:Msiwaamini wanawake kiasi cha kuwekeza muda na gharama zenu kubwa.
 
Kisheria sidhani kama kuna msaada, ila kwenye hiyi option ya pili yapo mengi tu yanayowezekana na kwakua anaefanyiwa hatakuwa ameonewa, basi atazunguka mpaka anazeeka.

Jamaa kazingua sana kusomesha mwanamke, ila hiyo isiwe sababu ya kuacha kukomesha hizi tabia.

NB:Msiwaamini wanawake kiasi cha kuwekeza muda na gharama zenu kubwa.
Ndio kusomesha alizingua, lkn bado tabia kama hizi Sio za kufumbia macho .

Ametupa maumivu makali mnooo !!.

Amewafedhesha wazazi , huwezi Amin Et sahizi Akina Mama wanahangaika Nako , Et Nako kanaliaaa na msamaha juu
 
Ndio kusomesha alizingua, lkn bado tabia kama hizi Sio za kufumbia macho .

Ametupa maumivu makali mnooo !!.

Amewafedhesha wazazi , huwezi Amin Et sahizi Akina Mama wanahangaika Nako , Et Nako kanaliaaa na msamaha juu
Kwahiyo kanalia na kuomba msamaha kakiwa na maana ya kwamba karudiane na ndugu yenu na mahari ya mkufunzi irudishwe, au kanalia ili msamehe na kusahau ?
 
Kwahiyo kanalia na kuomba msamaha kakiwa na maana ya kwamba karudiane na ndugu yenu na mahari ya mkufunzi irudishwe, au kanalia ili msamehe na kusahau ?
Ndio wanaleta habari za kurudisha Mahali ya Mkufunzi


Lkn Mimi japo sio muoaji, nmemwambia JAMAA, APIGE CHINI JUMLA.

ila tukape Adhabu maana hakafai
 
Hakuna kitu mtafanya, ametoa sadaka.

Si tulishakubaliana mchumba hasomeshwi na mwanamke haaminiki?

Liwe funzo kwake na kwa wengine wanaovunja makubaliano ya vikao.
Vya kufanyika vipo Man, DUNIA ni hiii hii .

Unajua Bro, ni wale wanaume wema sana yaan wale ambao akipata demu, anatulia tuliiii.
 
Ok, kwahiyo Kishika Uchumba nacho tupotezee?

Mi nadhan wakati mwingine Umasikini tunajitafutia wenyewe Kwa kupuuza fedha zetu na kuzichukulia poa poa.
Kishika uchumba chenu nendeni mkachukue. Ni haki yenu kurudishiwa.

Ila wala msifanye fujo, daini kistaarabu tu, msionyeshe kama mmechukia. Maana Malipo ya wema wenu yataendelea kuwaandama na kuwaumiza hao wazazi na huyo Binti kwa namna nyingine.
 
Back
Top Bottom