Mwanamke hasomeshwi

Mwanamke hasomeshwi

Kichochoro

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2017
Posts
1,135
Reaction score
1,168
"Nina miaka 25 nipo Kigoma. Nilikuwa na mahusiano na mdada mmoja hivi, tangu mwezi wa tisa mwaka 2016 kipindi hicho yeye alikua mwanafunzi so sikutaka kuharibu malengo yake sikuwahi kumuuliza wala kumtaka kimwili mpaka akamaliza shule ndio tukakutana 2017.

Kuanzia hapo tulipendana sana mpaka tukatambulishana home yaani mahusiano yetu mpaka wazazi walikua wanafahamu. Ilikuwa furaha kwakweli.

Matokeo ya kidato cha nne yalipotoka akaenda chuo Tabora na mimi nikabaki Kigoma nikiendelea na mishe mishe za utafutaji huku tukiwasiliana kwenye simu kila siku.

Kiukweli nilimjali sana, nilimtumia hela ya matumizi kila mwezi, kila kiti kilichokuwa ndani ya uwezo wangu, nilimpa.

Sikutaka akose chochote, hata wazazi wake walipopungukiwa kwenye ada, mimi niliongezea pale wazee walipopungukiwa.

Hiyo ikafanya kwao wanipende mno. Nilitoa msaada kwao na mtoto pia.

Shida ilikuja 2020, alipata ujauzito. Kiukweli hakutaka kwao wafahamu. Tuliweka siri mpaka akajifungua ndio tukafikisha taarifa nyumbani.

Kwa bahati nzuri alijifungua mwezi wa kwanza baada ya kuhitimu chuo. Kwao walikua wakali ila badae walielewa wakatulia.

Nikampa mtoto jina la mama yangu. Maisha yakaendelea na kwao waliamini nitamuoa.

Kwa bahati mbaya miezi miwili badae Mama yangu alifaliki so mambo yakazidi kuwa magumu kwangu. Nikajikuta naahilisha suala la ndoa na yule binti ili nikae sawa. Tukakubaliana tusogoze mbele suala la ndoa Ili tujipange vizuri.

Badae wakati mimi ndio nakamilisha mambo yangu taratibu akaanza kubadilika akawa ananifanyia visa ilimradi tuachene tu. Suala la ndoa akawa halitaki tena.

Kiukweli mara kadhaa niliwahusisha ndugu zake ila wakawa wananipa tu moyo wakasema mimi ndio mkwe wao hakuna mwingine. Mtoto akatimiza mwaka. Yule mwanamke akiwa bado hataki kufunga ndoa na mimi.

Mwanaume niliendelea kumhudumia mtoto, nilimpenda sana mwanangu. Atake nini nisimpe? jina lake lilinikumbusha marehemu mama yangu.

Sasa ikawa tunasumbua sana kwenye masuala ya hela, yaani kila mwezi nilikuwa natuma pesa ya matumizi na siku za sikukuu mwanangu hakosi nguo mpya.

Ilikua natuma pesa mpaka muda mwingine nilihisi ananikomoa. Ila sikutaka kujali sana maana nilijua natuma kwa ajili ya mtoto wangu.

Sasa kimbembe kimekuja hivi majuzi, kuna jamaa nilikuta amepost picha za mwanangu huku akijisifu amekuza. Nilishangaa, kiukweli nilihisi kama naota.

Ikabidi nimfuatilie jamaa mpaka nikapata namba yake, nikampigia akaniambia ukweli kwamba yeye yupo Tabora na alikutana na huyu mdada huko chuo na kumbe walikua wana mahusiano tangu 2020 na ndio alimpa mimba.

Ilinibidi nimuulize mhusika mwenyewe (mama wa mtoto) akakiri ni kweli akaniambia na mtoto sio wangu ni wa huyu jamaa wa Tabora yaani hapo nilitamani hata kufa kwani nilipoteza muda na gharama nyingi kwa ajili ya mtoto.

Niliwaambia wazazi wake, kumbe mama yake alikuwa anajua ila aliogopa kuniambia. Baba yake tu ndo alifichwa.

Sasa baba yake yeye hataki mwanamke aolewe kwingine anataka mimi ndio nimuoe. Hata mahali hataki, yaani ameniambia nikachukue mke bureee.

Sasa mimi nachoomba unifikishie kwa wadau wanipe ushauri , nikaoe huyu mwanamke nilee mtoto asie wangu au niachane nae niendelee na maisha yangu?

Please usiache kufikisha ujumbe huu". Anonymous, Kigoma. C&p from
#WatuNiStory
 
Jamani tuendelee na msimamo ule ule, hawa ni wakutomber tuu sio kiweka ndani.

Kijana acha ujinga wewe acahana nae huyo demu endelea na mambo yako
 
Jamaa nilisoma kweny page ya @watustory
nikajua jamaa kwanza mshamba sijui wa wapi huko kigoma ndani ndani demu kafika chuo kakutana na watu wana swaga za maana kashakusalit bado unashindwa kumuacha aende unelete pigo za kiduanzi

Na mtoti sio wako na huyu msela nae kashamzalisha huyo demu kakataa kumuoa utaka kupigwa za kichwa nenda temana nae kashaleta chenga utaumia zaidi uje kujinyonga bure wa wapi wewe dunia hii majanga tupu
 
Grow up hiyo ni signal ya kukualert kuwa unaenda uelekeo sio ni juu yako kuendelea na safari wakati ushakosea njia au kutafuta njia sahihi na kuanza safari.

Sema mapenzi ni upofu unakuta mtendwa ndio analazimisha ndoa
 
Kwanza pole Sana kiongozi Kwa mtihani huo ulio kutana nao.

Pili nimesikia kesi nyingi Sana za wanawake kusomeshwa na kisha kuwageuka wanaume wao,hivyo wanaume tushituke tuachane na hizi mambo tutakufa mapema.

Tatu,huyo dada amekutenda Sana,haijalishi unapata sapoti Kwa Baba yake,lkn mwisho wa siku hautaishi na Baba yake Ila utaishi na huyo mwanamke,so wewe ndo utayeteseka na vituko vyake,mwanamke kama hakutaki kubali matokeo ni hatar Sana Kwa afya yako na Maisha yako,najua umemgharamia Sana na kuwekeza Mda wako na hisia zako kwake,Ila yaliyo pita sindwele Ganga yajayo wakati mwingine yanatokea haya ili uepushwe na balaa kubwa Sana.

Mwisho Kwa members wenzangu,mtu anapotaka ushauri ujue amekwama na akili yake imefikia mwisho,haijalishi Kwa mtazamo wako wewe inaona kitu cha kijinga au cha kipuuzi,lakini Kwa mlengwa limemfikia kooni,mnawafanya wengine washindwe next time kuomba ushauri, ukiwa huna cha kusema kumfariji mtu Kausha Tu kiongozi si lazima uchangie,ni hayo Tu .
 
Hao wanawake wasiojitambua wachache wasiharibu hadhi ya wanawake wote.

Nimesomesha wife, Tena bado tukiwa marafiki tu na hapakua na utaratibu wala mpango wa kuoana, just out of Love, lakini hadi Sasa nnavyoandika, ananilelea wanangu vizuri sana. Pamoja na mapungufu yake kama binadamu ila ni Mke Bora na zaidi ya yote mama Bora kabisa wa wanangu.

Hizo kesi chache zisijumuishe wanawake wote.
 
Acha uboya unaoje mtu asiyekupenda. Unamuoa mwanamke siyo baba yake. Hata baba yake akupende vipi, kama dada hakutaki ni kazi bure. Kwanza ni laghai na tapeli
 

Tulia Kwanza, Utaleta Ya Said Wa Mwanza

 
Yaani umeona janga na bado unataka kulibeba tena hilo janga uishi nalo.
Kweli mwana kulitafuta mwana kulipata.
Huyo baba anakusokomezea zigo ukahangaike nalo.
Hapo kimbia hata usigeuke nyuma Tena shukuru Mungu kakuokoa mapema.
 
Mkuu pole Sana hio stori yako Haina tofaut Sana na ya kwangu bt nakushauri achana na huyo mwanamke mapenzi hapo hamna tena na ukiendelea kumfatilia utapoteza mwelekeo wa maisha yako
 
Sasa Mr hapo unataka ushauri upi mtu hakutaki, na mtoto si wako. Kama ulimuhudumia kipesa nae si alikuhudumia kimwili.
Labda upewe ushauri jinsi ya kujiponya maumivu ya mapenzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom