Angalau hapo kwa red kidogo nakuelewa.
Pale inapobidi sawa lakini siyo eti tunaamka wote afu haraka haraka nakimbilia kutandika kitanda.... Over My Dead Body..... Afu ni kweli una bahati kuolewa na msukuma asee, wife alishasafirigi kusafirisha msiba kwa siku tatu..... Neti alivyoiacha ndivyo alivyoikuta, mi najichomokea kitandani kama panya!! Alibaki anatikisa kichwa na kutimiza wajibu wake.
Wifey labda nilipitiwa by then umri ukiwa mchanga kwenye ndoa. Na kwa bahati mbaya au sijui nzuri haya maisha yetu ya extended family, ndani ya mwaka mmoja wa ndoa tayari naishi na shemeji zangu na wadogo zangu afu nifanye kazi za kina mama? OMG!! ...... Labda wenzetu mnaishi maisha ya kizungu zaidi kwamba nyumba nzima uko wewe na mmeo na mwanenu mmoja tu hapo kidooooogo naweza kuwaelewa.
Umri huu na vibinti ndo vinaingia sekondari mzee mzima niingie jikoni? NO WAY asee.
Ntaendelea kubakia baba wa kiafrika mwenye kufuata maadili ya kiafrika.
Nakala kwa wazee wenzangu
Dark City,
Mtambuzi,
Kaizer