Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,443
Wanawake wengi duniani wamekuwa wakipata taabu jinsi ya kuoanisha na kusawazisha majukumu yao ya nyumbani na yale yanayotokana na kazi za kuajiriwa ama kujiajiri wenyewe. Kwa mwanamke yeyote (hapa naomba charminglady, lara 1, Ciello, Asnam, na Smile wanisikilize uzuri) ambaye ndiyo mara yake ya kwanza kupata mtoto, lazima atasumbuka na kujiuliza sana jinsi atakavyoweza kuyamudu majukumu yote matatu kwa pamoja. Yaani kuwa mama, mke na kuwa mfanyakazi mahali fulani.
Kuna wakati niliwahi kuongea na mwanamke fulani, kuhusu jambo hili akalalamika kwamba wanawake wana mzigo mkubwa sana linapokuja swala la kazi na malezi katika ndoa mpaka wanachanganyikiwa.
Aliniambia,
"Ninyi wanaume hamna huruma, unakuta mke ametoka kazini, akifika nyumbani amechoka, watoto wanamuhitaji kama mama na mume naye anamuhitaji kama mke, na hapo ndipo tunapochanganyikiwa."
Nikamuuliza kwa hiyo hilo ndilo tatizo linalowafanya mchanganyikiwe, kwa ni hamkujua kwamba mkiolewa kuna kuzaa na kulea?
"Ndio, tunafahamu hayo, lakini inategemea na majukumu aliyo nayo mwanamke. Kwa mfano una mtoto mchanga unanyonyesha, halafu mume anataka haki yake ya ndoa, sasa wakati mkiwa katikati ya tendo, mtoto anaamka analia, hapo ni wazi hutaweza kuendelea kuweka uzingativu kwenye tendo kwa sababu huwezi kuvumilia kumuona mwanao akilia, na hapo ndipo panapozusha malalamiko kutoka kwa mwenzio kwa sababu kitendo hicho kitamkera. Lakini pia mwanamke akitoka kazini zipo kazi za nyumbani ambazo zinamtaka yeye mwenyewe azifanye, na ni wanaume wachache sana wanaojitolea kuwasaidia wake zao kazi za nyumbani, wanaume wengi huipenda kwenda kwenye baa na kujumuika na marafiki zao au kukaa hapo nyumbani na kuangalia TV au kusoma magazeti, huku akiagiza tu kila kitu afanyiwe, huu ni uonevu, wanaume wanapaswa wabadilike."
Alimaliza kusema mwanamke huyo.
Hebu kina mama na kina baba wa JF nipeni uzoefu wenu katika jambo hili wanawake kwa upande wenu mueleze jinsi mnavyoweza kukabiliana na changamoto hizi na wanaume mueleze ni namna gani mnasaidiana na wake zenu katika kukabiliana na changamoto hizo.
Karibuni