Wanawake kuchanganyika na wanaume Kanisani

sliding

Member
Mar 3, 2017
82
57
Mimi ni muumini wa Kanisa la Roman Catholic.

Utaratibu wa Kanisa umetenga upande wa wanaume na upande wa wanawake.Kinachonikera ni pale unakuta wanawake wanaingia kanisani na wanakuta upande wa akina mama nafasi zipo lakini baadhi yao hawapendi kukaa upande waliopangiwa wanaamua kujichomeka kati kati ya wanaume kitu ambacho mwanaume huwezi kwenda kukaa upande wao.

Najiuliza hivi huu ujasiri wanautoa wapi?Tena si wamama watu wazima ila ni mabinti.Huku si kuharibiana usikivu wa ibada?

Unaanza kuwaza mengine wakati uko kwenye ibada!Au hua mnatumwa na shetani?

Kama viongozi wa Kanisa mpo hebu jaribuni kulikemea hili,hasa Kanisa kuu Kigoma mabinti wanapenda sana kujipachika kati kati ya wanaume hata kama upande wao kuna nafasi.
 
Mimi ni muumini wa Kanisa la Roman Catholic.Utaratibu wa Kanisa umetenga upande wa wanaume na upande wa wanawake.Kinachonikera ni pale unakuta wanawake wanaingia kanisani na wanakuta upande wa akina mama nafasi zipo lakini baadhi yao hawapendi kukaa upande waliopangiwa wanaamua kujichomeka kati kati ya wanaume kitu ambacho mwanaume huwezi kwenda kukaa upande wao.Najiuliza hivi huu ujasiri wanautoa wapi?Tena si wamama watu wazima ila ni mabinti.Huku si kuharibiana usikivu wa ibada?Unaanza kuwaza mengine wakati uko kwenye ibada!Au hua mnatumwa na shetani?Kama viongozi wa Kanisa mpo hebu jaribuni kulikemea hili,hasa Kanisa kuu Kigoma mabinti wanapenda sana kujipachika kati kati ya wanaume hata kama upande wao kuna nafasi.
Labda tuu nikusahihishe. Kanisani hakuna upande wa wanawake wala wanaume. Ila ni mazoea fulani yaliyo jijenga. Kaninisani hakuna limitation mahala pa kukanyaga. Hata ww unawwza simama hata madhabahuni. Kama ww ni msomaji wa biblia rejea pale mahali ambapo pazilia lilipasuka katikati likatenganisha patakatifu pa patakatifu na sehemu nyingine ya waumini

My take

Binafsi nakuona hupendi kukaa na akina mama. For ur reasons. Huenda una mihemko or whatever.

Nawasilisha.
 
Mkuu Preta habari za miaka 2 -3 hivi ya kupoteana. Maana sijakutia machoni pa JF kitambo Kiasi.

By the way nili miss sana michango yako . Karibu tena mkuu Preta

Turudi kwenye mada, kama umeenda kanisani kutega mingo (wazee wa kung'oa nanga vyombo vya mgiriki) utapotezewa concentration (makini) ya misa, ila kama umeenda kusali tu, Haina shida aisee, neno utapata na kulishwa mana ya kutosha.
 
Utamaduni wa wanawake na wanaume kukaa sehemu tofauti walituletea wazungu, wakati wao walikuwa wanakaa kwa kujichanganya. Ukisoma kitabu cha Ferdinand Oyono HOUSEBOY inaonesha makatekista walikuwa wanatembeambea katikti ya korido wakiwa na fimbo huku wakiangalia mwafrika atakaye acha kusikiliza mahubiri na kuwaangalia watu ili atandikwe bakora.
Ukiingia kanisani unawaza ngono, lazima msichana akikusogelea utaanza kuwakwa tamaa wakat si wengine huwa tunawaona watu tukitoka nje ya kanisa. Mle ndani ni kumtafakari Yesu na matendo yake tu.
Kemea pepo lako badala ya kuwaandama wadada wa watu.
 
We mleta mada kwanza ni mpotoshaji mkubwa kanisa katoliki halina utaratibu wa kutenganisha jinsia ndani ya kanisa kama ulivyo sema. Halafu suala la utulivu ni wewe tu hata usipokaa na mwanamke kama hujawa na akili ya umeenda kanisani kufanya nini basi ni dhahiri utulivu utakupita kushoto.
 
Mimi ni muumini wa Kanisa la Roman Catholic.

Utaratibu wa Kanisa umetenga upande wa wanaume na upande wa wanawake.Kinachonikera ni pale unakuta wanawake wanaingia kanisani na wanakuta upande wa akina mama nafasi zipo lakini baadhi yao hawapendi kukaa upande waliopangiwa wanaamua kujichomeka kati kati ya wanaume kitu ambacho mwanaume huwezi kwenda kukaa upande wao.

Najiuliza hivi huu ujasiri wanautoa wapi?Tena si wamama watu wazima ila ni mabinti.Huku si kuharibiana usikivu wa ibada?

Unaanza kuwaza mengine wakati uko kwenye ibada!Au hua mnatumwa na shetani?

Kama viongozi wa Kanisa mpo hebu jaribuni kulikemea hili,hasa Kanisa kuu Kigoma mabinti wanapenda sana kujipachika kati kati ya wanaume hata kama upande wao kuna nafasi.
Wewe una pepo linalokufanya Ukereke kwa wao kukaa huko, au linalokufanya ufikirie maovu.

Ikiwa wamekaa na wanasikiliza neno/mafundisho ya kiroho...Je Wanakukera nini? Wanakukeraje?

Ikiwa wewe unaconcetrate kusikiliza mafundisho ya kiroho, Je unapata wapi muda wa kujiuliza hayo?

Jibu hayo mawili nijaribu kukusaidia zaidi.
 
Back
Top Bottom