Wanawake hupenda kuonewa wivu……!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
Kama ulikuwa hujui, ni kwamba wanawake hupenda kuonewa wivu, lakini kwa kiasi kidogo tu. Lengo lake hasa ni kutaka kujua kama unamjali kwa kiasi gani. Wakati mnapoingia kwenye mghahawa ama kwenye Baa, mwanamke angependa ugundue kwamba kuna mtu amevutiwa naye, hata kama mtu huyo ni muhudumu.

Pia wakati wanaume wengine wanapowakodolea macho unapokuwa naye barabarani, ama wafanyabiashara wa mitaani wanapopiga kelele na miluzi ya kumsifia, angependa kuona utalichukuliaje hilo.

Unapoonekana kutofurahishwa na vitendo hivyo na kumtaka mtafute sehemu nyingine ambayo haitakuwa na rabsha, ama nawe utakapoonekana kuona fahari ya kuwa na mwanamke anayevutia watu, basi mpenzi wako huyo naye ataona kwamba yeye ni muhimu kwako.

Lakini ni lazima uwe mwangalifu usije ukajenga ama kuonesha wivu wa kupindukia, kwani hilo litamfanya mpenzi wako ahisi unamuona yeye si mwaminifu, au ni Malaya. Kumbuka wivu ukizidi sana huwa kero.
 
kibali

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
504
420
umesema kweli wivu ukizidi ni kero,lkn ni chachu ya mapenzi kwa wote(wanaume na wanawake),hata wanaume wanajisikia vizuri wanapoona wapenzi wao wanapata wivu kwa ajili yao kwa hiyo ni swala ambalo lina apply both sides si kwa wanawake tuuuu! Wivu ni mzuri ila kwa kiasi
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
umesema kweli wivu ukizidi ni kero,lkn ni chachu ya mapenzi kwa wote(wanaume na wanawake),hata wanaume wanajisikia vizuri wanapoona wapenzi wao wanapata wivu kwa ajili yao kwa hiyo ni swala ambalo lina apply both sides si kwa wanawake tuuuu! Wivu ni mzuri ila kwa kiasi

Inawezekana ni kweli, lakini ni kwa baadhi ya wanaume.... kuna wanume hawapendi kabisa kuonewa wivu kwa sababu wanajiamini na wanajua wajubu wao katika familia.....Kwa mfano mimi buinafsi, kuonewa wivu, hata kidogo naona kero tu......... Ila kwa wanawake, wao ndio burdani kabisa....
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,892
728,531
Lakini ni lazima uwe mwangalifu usije ukajenga ama kuonesha wivu wa kupindukia, kwani hilo litamfanya mpenzi wako ahisi unamuona yeye si mwaminifu, au ni Malaya. Kumbuka wivu ukizidi sana huwa kero.

kwahiyo unashauri tuwe na wivu wa wastani ambao sijui tutaupimaje.....................
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
kwahiyo unashauri tuwe na wivu wa wastani ambao sijui tutaupimaje.....................

Duh! Swali lako gumu kweli................. ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaa...... anyway nitaku-PM kukupa maujanja
 
Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,904
Kweli baba wivu una raha yake kwa wote mwanamke na mwanaume na nisehemu ya mapnz kama mtu hana wivu kbs anakuwa hajapenda kwa thati lkn akishapenda kwa thati ya moyo wako wivu unakuja automatically!cha msingi ni kuwa na uwezo wa namna ya kuucontrol usilete madhara au kero kwa mmoja wapo!
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,995

Mimi wivu sina kabisaa_badala yake nina hasira.
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
37,635
42,431
isije kuwa ni wivu wa kweli kweli wewe ukabakia unajichekesha chekesha tu.
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,995
kama kweli umependa na huna wivu,lzm una tatizo la kisaikologia kawaone wataalamu mkuu!

ni kweli ninapenda lakn kamwe sina wivu_mpnz wangu akifanya ndivyo sivyo ninachukia(kumbuka sioni wivu) na sioni shida kuachana nae pale inapobidi,...naona sina tatizo lolote kwa hilo na hivyo no need ya kuwa konsati hao wataalam........achana na wivu unaweza kujiua ama kuua
 
Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,904
ni kweli ninapenda lakn kamwe sina wivu_mpnz wangu akifanya ndivyo sivyo ninachukia(kumbuka sioni wivu) na sioni shida kuachana nae pale inapobidi,...naona sina tatizo lolote kwa hilo na hivyo no need ya kuwa konsati hao wataalam........achana na wivu unaweza kujiua ama kuua
Huu ni wivu wa wastan Igwe,sio ule wa kupigana na watu jaman,mie nisipokuwa nao basi cjapenda na huwa niko open ckupendi na mtu akisema ananipenda ile hali hana wivu na mie basi huwa namuona tapeli, tutaishia kupiga story tu kwan hunitoka hata moyon kbs!
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,995
Huu ni wivu wa wastan Igwe,sio ule wa kupigana na watu jaman,mie nisipokuwa nao basi cjapenda na huwa niko open ckupendi na mtu akisema ananipenda ile hali hana wivu na mie basi huwa namuona tapeli, tutaishia kupiga story tu kwan hunitoka hata moyon kbs!
hapa ni lazma tukubaliane kwamba watu/wanaume tuko tofauti na hii ni kutokana na mazingira tuliyokulia,..wivu wa wastani unaweza ukahisi lakn kamwe usiseme kitu(unajikausha)...sasa kama unajua kama mtu ajakuambia kitu kama cha wivu ni hakupendi basi unakosea,....its true mpnz wangu anasema namchukulia poa eti sababu simuonyeshi tu-wivu_lakn kusema kweli nampenda sana ila najikausha kisabuni,......thats how i/we do
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom