Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,395
Kama ulikuwa hujui, ni kwamba wanawake hupenda kuonewa wivu, lakini kwa kiasi kidogo tu. Lengo lake hasa ni kutaka kujua kama unamjali kwa kiasi gani. Wakati mnapoingia kwenye mghahawa ama kwenye Baa, mwanamke angependa ugundue kwamba kuna mtu amevutiwa naye, hata kama mtu huyo ni muhudumu.
Pia wakati wanaume wengine wanapowakodolea macho unapokuwa naye barabarani, ama wafanyabiashara wa mitaani wanapopiga kelele na miluzi ya kumsifia, angependa kuona utalichukuliaje hilo.
Unapoonekana kutofurahishwa na vitendo hivyo na kumtaka mtafute sehemu nyingine ambayo haitakuwa na rabsha, ama nawe utakapoonekana kuona fahari ya kuwa na mwanamke anayevutia watu, basi mpenzi wako huyo naye ataona kwamba yeye ni muhimu kwako.
Lakini ni lazima uwe mwangalifu usije ukajenga ama kuonesha wivu wa kupindukia, kwani hilo litamfanya mpenzi wako ahisi unamuona yeye si mwaminifu, au ni Malaya. Kumbuka wivu ukizidi sana huwa kero.