Wanawake hawajaielewa ideology ya 50/50

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,425
9,823
Wanawake wa Tanzania bado hawapo tayari kui-practice au hawajaielewa hii ideology ya 50/50. Ukifatilia kampeni zao utaona kimsingi wanachokipigania sio usawa ila wanapigania upendeleo.

Fatilia uko ambapo hii ideology imetoka utaona wapenzi wakitoka out kila mmoja analipa bill yake, hakuna mambo ya kuomba nauli unapotaka kumtembelea mwenzako kitu ambacho ni tofauti na hapa kwetu.

Tukiamua tuondoe viti maalumu kwa wanawake pale bungeni kwa sababu ni kitu ambacho kinamu-underestimate mwanamke izo nafasi zipiganiwe na jinsia zote kwa kuangalia uwezo wa mtu nina uhakika hawa hawa wanaopigania usawa watapinga.

Tukiamua tuondoe suala la kugawana mali baada ya kuachana na kila mtu achukue mali aliyoitolea jasho yeye binafsi nina uhakika hawa hawa wanaojiita super-women watapinga. Ishafika hatua wanawake wanaona kuongwa ni haki yao, kupewa upendeleo ni haki yao hapo hapo wanataka usawa wa kijinsia.

Mwambie mwanamke usawa kwenye elimu, ajira, uongozi, kurithi mali atakuelewa ila mwambie usawa kwenye kumuhudumia mwenzake kama bado anajitafuta hapo utaitwa marioo, utaambiwa tafuta hela, utaambiwa mwanaume dhaifu unakwepa majukumu n.k.

Wanawake wanataka usawa kwenye kila kitu isipokua kwenye mambo ambayo yanamuingiza gharama/yanamuweka hatarini mwanaume hapo ndipo wanawake wanataka mfumo dume uendelee.

Leo hii ikitokea vita ni wanaume tu ndio wanaenda kwenye uwanja wa mapambano huu ni ubaguzi wa kijinsia kwa sababu mwanamke ananyimwa fursa ya kwenda vitani kuipigania nchi yake lakini mimi tangu nimepata akili ya kujifahamu sijawai kumsikia fermist yoyote anapigania haki ya wanawake kwenda vitani kwenye battle field itambulike kisheria.

Wanawake kuweki specific kama mnataka 50/50 basi 50/50 iwe applicable kwenye kila kitu na kama mnataka mfumo dume basi mfumo dume uwe applicable kwenye kila kitu. Acheni ujanja janja wa kudai 50/50 ya kulenga kwenye mambo matamu tamu tu.

Ni vile tu wanaume ni watu wa kupuuzia ujinga jinga ila tukiamua kurespond ni nyie ndio mtaumia. Just imagine wanaume waache kuonga/kuwahudumia kuna wanawake watakosa sehemu za kuishi na watakufa njaa.
 
NDO MANA MIMI NILISHAIKATAA HII IDEOLOGY YAO NDANI YA KICHWA CHANGU.MAANA SIWEZI KUBEBA MIMBA MIEZI 4NA NUSU HALAFU NIMPE MUME ABEBE.
 
NDO MANA MIMI NILISHAIKATAA HII IDEOLOGY YAO NDANI YA KICHWA CHANGU.MAANA SIWEZI KUBEBA MIMBA MIEZI 4NA NUSU HALAFU NIMPE MUME ABEBE.
Ni kweli kabisa ukiangalia hii ideology ya 50/50 kijamii, kiuchumi, kimaumbile n.k unaona kabisa inakataa. Wanawake wengi wanaoipigania wanaangalia kigezo cha uchumi tu wakishaona wana uwezo wa kijiuhudumia wanafikiri wapo sawa na mwanaumenkatika kila nyanja ila wanasahau mambo mengi sana ya muhimu
 
Ni kweli kabisa ukiangalia hii ideology ya 50/50 kijamii, kiuchumi, kimaumbile n.k unaona kabisa inakataa. Wanawake wengi wanaoipigania wanaangalia kigezo cha uchumi tu wakishaona wana uwezo wa kijiuhudumia wanafikiri wapo sawa na mwanaumenkatika kila nyanja ila wanasahau mambo mengi sana ya muhimu
Yaani kwa kweli wanawake wanapotoshwa sana
 
Back
Top Bottom