Deo aliniambia one Friday amefika nyubani anamkuta wife amevimba akamwambia kila Ijumaa wewe unatoka unarudi Jmosi asubuhi, yaani mimi niko hapa kulea watoto wako tu, mwanaume huonekani. Basi Deo akajua kimenuka leo hakutokeki hapa. Mida ya saa mbili tatu binti akapiga simu, I'm bored, njoo, Deo akamwambia leo siwezi kwenda viwanja, binti akasisitiza njoo basi unipe a good night kiss. Base Deo anasema kwenda kule story zikaanza, mambo ya henessy, mziki, kustuka ni saa 12 asubuhi.
Deo alitoka pale, straight butcher akanunua nyama, akaenda Ferry kusanya samaki, akatafua sato pia, kutoka. Amefika nyumbani wife anatengenezea watoto breakfast hataki hata kumwangalia. Basi Deo akaweka mizigo kwenye sink la jikoni, akaenda kuoga na kulala.
Mke ameingia jikoni anakuta ile mizigo, akaanza kuosha na kuweka kwenye freezer. Baadae akaenda chumbani mwenyewe baba nanii, samahani sikujua kumbe ulikwenda kututafutia sisi, nikutengenezee nini mume wangu. Akajibu supu.