Wanaume yanawakutaga

Wanaume yanawakutaga

Siyo lazima uongee na mtu... unachangia tu mada zinazoendana... unawapa pole ndugu wa pale...
Ok, wakikuuliza utatoa pole labda kwa mume wa marehemu, atapokea pole, kabla hujafika kule ndugu wengine wanaweza kuuliza, unamfahamu vipi marehemu?
 
wanachukulia poa kila kitu, wengine wanaogopa kuachwa ndo maana wanabebelea upuuzi afanyao mwanaume. hahaaaa Nifah I wish nikuone cku ukimfumania...
Huo ni zaidi ya upuuzi na kutokujiamini.
Hivi unadhani nitapigana au kufanya anything stupid?
Nitamuonesha tu kwamba hana ujanja,nimeona ujinga wake na huo ndio utakuwa mwisho wetu.
 
Ok, wakikuuliza utatoa pole labda kwa mume wa marehemu, atapokea pole, kabla hujafika kule ndugu wengine wanaweza kuuliza, unamfahamu vipi marehemu?
Unaenda na mwanamke.. alafu yule mwanamke ndiyo anakuwa kama rafiki wa yule marehemu... ukiulizwa unasema... marahemu ni rafiki wa huyu...
 
jamaa ana msiba mkubwa, hadi nimeukumbuka mchepuko wa jamaa yangu mmoja alipofariki, binti alizirai mara kadhaa sema ndo mchepuko na hata msibani hakufanikiwa kwenda coz tayari kuna walomfahamu.
najaribu kuwaza kwa sauti kama angefariki usiku ambao wapo wote na huyo jamaa sasa story ingekuwa nyingine
 
Misiba ya siku hizi watu wanaulizana wewe ni nani? na umetoka wapi ? Umekuja kufanya nini msibani ?
Nachojua mimi misiba yetu huku uswahilini unafika msibani salimia ulio wakuta kamata karata mnacheza last card mambo yanaendelea kama mmejuana miaka10 hivi
 
Good story...ni huzuni kwa Deo mtu alimjali kama rafiki hawezi kumuaga ipasavyo. Pengine angempigia usiku wake angeweza msaidia...pole Deo
 
Heheheheee
Sio tatizo,nitahakikisha namfanyia 'ziara za kushtukiza'
Mbona nitamfuma tu?
Mie mwanaume anidanganye labda niamue tu.
Unasema tu dada yangu mtu akiamua huwezi mdaka hata siku moja inategemea
Tu ni shughuli gani anafanya..atakupeleka kutokana na mazingira na utamuamin tu..
 
jamaa ana msiba mkubwa, hadi nimeukumbuka mchepuko wa jamaa yangu mmoja alipofariki, binti alizirai mara kadhaa sema ndo mchepuko na hata msibani hakufanikiwa kwenda coz tayari kuna walomfahamu.
najaribu kuwaza kwa sauti kama angefariki usiku ambao wapo wote na huyo jamaa sasa story ingekuwa nyingine

Yaani yangetokea wako pamoja Deo angekuwa anaisaida polisi, alafu ukute mke anamnaga wakati mwenzie anamajonzi.
 
Hilo siwezi kujibu, lakini walizoeana sana.
Sasa kwa nini Deo amtembelee huyo binti wakati mumewe anaposafiri kama hakuwa na nia ovu? Deo na huyo binti walikuwa wanaangalia tu, inamaana Deo alifurahi kwenda kumtumbulia macho huyo binti?
 
Sio ujinga, ndio akili mama.
Kila mtu ana njia mbalimbali za kusema nakupenda ama nimekosa. Ukitaka mumeo aishi kama senema za telemundo utaumia. sio kila mtu atafikiria kununua maua, dhahabu ama kulia machozi akisema nimekosa. Ukimuelewa mwenza wako utaweza kumpima na kufanya maamuzi, including maamuzi magumu
Hakuna kitu sipendi kama hicho.
Wanaume sijui wakoje?
Eti akijua kakosea atajikusanya anunue vitu kibao!

Nilivyo nitamtimua navyo....
Ila kuna wanawake wajinga wanavipokea na kuchekelea.
Namna hiyo si atakuwa anafanya makosa akijua atakununulia vitu nawe utapoa?
 
Sometimes majanga yanatokea kukufunga speed gavana. Deo alinipaga story nyingine, alitumwa kikazi Dodoma, akakutana na binti anasoma UDOM akitokea mikoa ya Kaskazini Magharibi, alimtokea mtoto lakini dada alisema mume wa mtu kwake sumu, Deo akawa single palepale. Wakahave fun, muda wote Deo alipokuwa katika ile safari.

Baada ya ile safari Deo akawa anakwenda Dodoma at least once a month kujivinjari na mwanafunzi wa chuo, alimhudumia kwa kila aliloweza. Sasa binti alitaka kujua mustakabali wa uhusiano akimaliza shule, Deo akamwambia ngoja kwanza, wewe soma hayo mengine yatakuja baadae.

Likizo moja bidada rafiki zake wa DSM wakamkaribisha, alikwenda kukaa nao wakawa wanamtembeza mjini, mmoja wao akakumbuka binamu yake anaishi mitaa ile, walikuwa watatu wakaamua kwenda kumsalimia binamu wa rafiki yao. Walikaribishwa.

Deo akiwa ametoka, aliporudi anamkuta mwanafunzi wa UDOM amejaa kwenye sofa siting room. Yaani pale pale akastuka akamwambia mkewe ninarudi sasa hivi, kuna ishu jamaa ananisubiri nilisahau na nikichelewa ninamkosa. Hakurudi mpaka saa sita usiku.

Nikamwambia yaani hiyo Mungu alikuangaza kabisa uache hii michezo utulie. Sasa hili ninadhani litamtuliza.
 
Hiyo ni intressant

http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Sasa kwa nini Deo amtembelee huyo binti wakati mumewe anaposafiri kama hakuwa na nia ovu? Deo na huyo binti walikuwa wanaangalia tu, inamaana Deo alifurahi kwenda kumtumbulia macho huyo binti?

Wakubwa hawasemi kila kitu, kama kusoma hujui na picha huoni?
 
Unasema tu dada yangu mtu akiamua huwezi mdaka hata siku moja inategemea
Tu ni shughuli gani anafanya..atakupeleka kutokana na mazingira na utamuamin tu..
Nakuambia hivi....
Mimi kudanganywa labda niamue mimi tu.
Na labda niwe simpendi ndio sitomfuatilia ila nitakuwa najua anachokifanya.
Acheni hizi mambo ya kujishusha,eti unakubali kabisa kuzidiwa ujanja!
 
Sio kuwa unakubali kuzidiwa ujanja, unaangalia majukumu uliyonayo na watoto unaamua kuprioritise mkiwa wote wajanja nyasi ndiyo zinaumia.
 
Back
Top Bottom