Wanaume wote tukumbushane machungu ya kisu cha jando

Wanaume wote tukumbushane machungu ya kisu cha jando

Mi nilijipeleka mwenyewe tu siku hiyo niliona Braza na Binamu wanachukuliwa kwa Fix nyingi kwamba kuna tukio la muhimu wakavaa wakapendeza kuelekea kwenye tukio. Nikaona haiwezekani tukio linipite nikalilia kwenda so wazee wakashauriana pale wakanichukua namimi. Nilichokikuta huko Daaah ilikuwa siyo poa, 2000 iyo. Bora ningechelewa chelewa kidogo niende na madogo ambao walifanyiwa ganzi zilikuwa zimeanza kutumika
 
Ile better kitoto kikiwa kidogo ni fasta tu,wanaweka kimpira flani then paap tayari ondokeni.siku moja tu dogo kasahau.ile ya kukatwa kule apana maumivu yake nimesoma mada ya jamaa hapa nikakumbuka

Yaan ingekua optional kukatwa ama kuto kukata haki vilee mwanangu nisingempeleka
Nina ucle wangu ananiambia ile experience /maumivu anahisi mpk leo kila akikumbuka kisu cha ngariba
Yaan mwili unamsisimka
 
Aisee hatari Sana mwili una sisimka Sana nikikumbuka ila mimi ili tumika topaz daaah

Ilikuwa siku ya jumamos majira ya saa nne hasubuhi mwaka 1997 kambi ilikuwa pembezoni mwa mto
Basi tulikuwa wawli mimi na kaka yangu tulipo fika kambin tulikuta hakuna foleni kubwa Sana

Hivyo bas mimi nikaambiwa nisubir kaka akatangulia azikupita dakika mbili na sikia kelele za brother mama nakufa Ile nataka ni sepe Nika dakwa mkono na mshua Ana nambia tulia. [emoji848]

Basi zamu yangu ika fika ni kaingia kilingen vua nguo zote Nika we kwa Kati yan Kuna mtu mzima Ana kaa chin afu una kaa mbele yake Ana kumbana miguu kwa kupitisha miguu yake juu yako afu Ana pitisha mikono yake akitokea mgongon Ina pita kwenye kwapa alafu Ana kuziba macho na kukubana kifuan

Aisee dk moja na sikia chaaaa topaz ime pita Ata kulia si kulia ila Maumivu ilikuwa natoa machoz bila kupenda
Nika we kwa joto (dawa Fran hivi nyekundu hivi) alafu tuka fungwa fungwa dawa dawa Fran hivi za kienyeji mikonon kama saa kiunon kwamba Ina ipenda kufungwa kwenye jamaa alie katwa safari kurud home aisee ilikuwa hatari Lakin salama

Pole sana mkuu
 
Dah, nakumbuka nilipokuwa mdogo nikiwaona mabraza na kanga kitaani.natamani na Mimi niwe kama wao, kumbe kinacho fanywa hko ni zaid ya jehanamu aisee. In short nikikumbuka unapata hamasa ya kukitumia hiki kifaa
 
G
Sitaki kukumbuka maana sio kwa msoto ule
Mkuu

Sisi watoto wa dot com hatukukutana na hayo maumivu

Nakumbuka tulienda home kwa Dokta mzee alisema anajisikia kuumwa. Tulipofika nikageuziwa kibao. Nikalazwa kwenye kitanda cha hospitali.

Miguu ikapenyezwa chini ya chuma la kitanda then mzee akanishika mikono docta akanichoma sindano.

Nilijitahidi kuangalia baada ya kuchomwa sindano nkaona dushe limekuwa kubwa kinoma

Wakati anakata ile ngozi sikusikia maumiv ila nilijitahidi kuinua shingo nione daah niliona damu nikachanganyikiwa

Wakati wa kushona ndiyo kulikuwa na maumivu kiasi. Nyuzi ziliachwa humo humo bila kutolewa ilikuwa ni kukiosha kidonda tu hadi nikapona.

Kiukweli wa dot com hatujakunata na maumivu kama yenu Mkuu.

Poleni
Aisee nakumbuka ilikuwa asubuhi mapema kabisa jua kabla halija chomoza niliamshwa na mshua akanipeleka mtoni kuoga maji ya baridi baada ya hapo tukaendelea na safari ya kwenda kwenye nyumba ya mzee fulani hivi maeneo ya pale kijijini, ghafla nikakuta kuna watoto wengine wa rika langu nao wameletwa na wazazi wao ila wakawa wamepanga foleni huku wakiwa wamefungwa mashuka.

"ASIYETABIRIKA njoo huku utoe nguo zako nikufunge shuka kama wenzio" sauti ya mshua ilisikika huku akitoa shuka kwenye mfuko wa rambo alioushika mkononi, hapo sasa sensor za ubongo wangu zikahisi tukio litakalojiri maeneo hayo. Kabla sijafanya makeke yangu ya kupotea haraka katika hayo maeneo wakaja vijana wawili wakasaidiana na mzee wakanishika na kunivua nguo na kunifunga shuka nikawekwa kwenye foleni chini ya ulinzi mkali huku mzee akinikata jicho kali kuashiria kichapo ambacho angenipa kama kusingekuwa na watu wengine eneo lile mimi sikujali hilo.

Hofu ilinishika licha ya baridi lililokuwepo asubuhi ile ila mwili wangu ulichemka balaa maana stori nilizokuwa nikizipata kwa wenzangu waliokwisha katwa zilikuwa zinatisha mno. Nikajipa moyo mkuu kuwa nitakomaa , mara wa kwanza akaanza kukatwa alitoa sauti ya uchungu hali iliyopelekea mimi nibawe na mkojo na haja kubwa mda huo huo, nikapelekwa kwenye kachoo kalikokuwa kwenye ule mji chini ya ulinzi mkali, ila nilipofika mkojo wenyewe ulitoka kiduchuuuu na haja ikatoka hewa tu.Nikarudishwa eneo la tukio huku nikiwa nsha pagawa ramani zote za kuchoropoka zikiwa zimekuwa covered, asiyetabiria kapatikana.

Ikafika zamu yangu ilikuwa mida ya saa nne hivi asubuhi, likatolewa shuka nililofungwa nikatanua miguu kidogo, yule babu alizuga kama anavutavuta ile ngozi hivi mara paaaapu, rwaaaaaaa kisu kimepita yaani nilitoa sauti kali sana yaani sauti ilinitoka huku mwili ukitetema nikiashiria kiwango cha maumivu nilichokipata nililia kwa sauti KUU, nikapakwa dawa nikawekwa pembeni nikafungwa shuka tena huku mwendo ukiwa umebadilika. Hapo nikamuona mshua akitabasamu kidogo huku akiniambia "asiyetabirika sasa umekuwa mwanaume, umekamilika jikaze twende" huku akinipiga piga mabegani.

Sasa huwa nikiyakumbuka yale maumivu huwa sina masihara kabisa na vidada vinavyokatizakatiza kwenye anga zangu, kwa wananaume wote tuliopitia hizi mambo tukumbushane ule wakati mgumu tuliopitia, wale wa hospitalini hawataelewa chochote hapa.
 
Aisee umenikumbusha mbali sana, Mimi nilikua wa pili katika foleni ila wakwanza wetu alikatwa vibaya sana, kipindi hicho hakuna ganzi,
First of all unapigwa mtama ukianguka tuu tayari ngariba kashafanya yake
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatariiii
Oo oo ooh[emoji445]
Oo oo ooh[emoji445]
Sipitiii madimbeee shauri ya heriiiiii mama kaniambiaaaaa[emoji445]
(Kiitikio: Mbelaaaaaa[emoji444])
Nenda jandoniiii mpaka siku ya kurudiiii[emoji445]
(Kiitikio:mbelaaaaa[emoji444])
Ntakupa shilingiii , kitambaa na miwani[emoji445]
( kiitikio:Mbelaaaa[emoji444])
Na viatu chiniii utakavyo kanyagiaaa[emoji445]
(Kiitikio:Mbelaaa[emoji444])
[emoji441]Leo nimerudiiiii nipe ahadi zangu tulizoaganaaaaaa[emoji441]
(Huuu wimbo ulikuwa unaimbwa alfajiri jandoni [emoji23] wakati wa baridi kaliiii[emoji234][emoji249].
 
Mimi nilienda hospital ni kama napasaswa tu hakuna maumivu kabisa. Pole mkuu.
 
Yaani kama wote tungekuwa tunapitia machungu yale, hata hawa mashoga mitaani wasingeonekana.[emoji16][emoji16]
Kwahiyo mkuu waliopitia hospital ndo mashoga [emoji3][emoji3][emoji3] watu bhana...
 
Kwahiyo mkuu waliopitia hospital ndo mashoga [emoji3][emoji3][emoji3] watu bhana...
Nilisema ni vigumu sana kwa lijamaa ambalo mkuyenge wake umepita kwenye kisu cha ngariba halafu aje autelekeze yaani asiutumie kama inavyotakiwa, eti autelekeze halafu aanze kubonyezwa yeye kunako 0712
 
Back
Top Bottom