asiyetabirika
Member
- Oct 14, 2019
- 46
- 56
Aisee nakumbuka ilikuwa asubuhi mapema kabisa jua kabla halija chomoza niliamshwa na mshua akanipeleka mtoni kuoga maji ya baridi baada ya hapo tukaendelea na safari ya kwenda kwenye nyumba ya mzee fulani hivi maeneo ya pale kijijini, ghafla nikakuta kuna watoto wengine wa rika langu nao wameletwa na wazazi wao ila wakawa wamepanga foleni huku wakiwa wamefungwa mashuka.
"ASIYETABIRIKA njoo huku utoe nguo zako nikufunge shuka kama wenzio" sauti ya mshua ilisikika huku akitoa shuka kwenye mfuko wa rambo alioushika mkononi, hapo sasa sensor za ubongo wangu zikahisi tukio litakalojiri maeneo hayo. Kabla sijafanya makeke yangu ya kupotea haraka katika hayo maeneo wakaja vijana wawili wakasaidiana na mzee wakanishika na kunivua nguo na kunifunga shuka nikawekwa kwenye foleni chini ya ulinzi mkali huku mzee akinikata jicho kali kuashiria kichapo ambacho angenipa kama kusingekuwa na watu wengine eneo lile mimi sikujali hilo.
Hofu ilinishika licha ya baridi lililokuwepo asubuhi ile ila mwili wangu ulichemka balaa maana stori nilizokuwa nikizipata kwa wenzangu waliokwisha katwa zilikuwa zinatisha mno. Nikajipa moyo mkuu kuwa nitakomaa , mara wa kwanza akaanza kukatwa alitoa sauti ya uchungu hali iliyopelekea mimi nibawe na mkojo na haja kubwa mda huo huo, nikapelekwa kwenye kachoo kalikokuwa kwenye ule mji chini ya ulinzi mkali, ila nilipofika mkojo wenyewe ulitoka kiduchuuuu na haja ikatoka hewa tu.Nikarudishwa eneo la tukio huku nikiwa nsha pagawa ramani zote za kuchoropoka zikiwa zimekuwa covered, asiyetabiria kapatikana.
Ikafika zamu yangu ilikuwa mida ya saa nne hivi asubuhi, likatolewa shuka nililofungwa nikatanua miguu kidogo, yule babu alizuga kama anavutavuta ile ngozi hivi mara paaaapu, rwaaaaaaa kisu kimepita yaani nilitoa sauti kali sana yaani sauti ilinitoka huku mwili ukitetema nikiashiria kiwango cha maumivu nilichokipata nililia kwa sauti KUU, nikapakwa dawa nikawekwa pembeni nikafungwa shuka tena huku mwendo ukiwa umebadilika. Hapo nikamuona mshua akitabasamu kidogo huku akiniambia "asiyetabirika sasa umekuwa mwanaume, umekamilika jikaze twende" huku akinipiga piga mabegani.
Sasa huwa nikiyakumbuka yale maumivu huwa sina masihara kabisa na vidada vinavyokatizakatiza kwenye anga zangu, kwa wananaume wote tuliopitia hizi mambo tukumbushane ule wakati mgumu tuliopitia, wale wa hospitalini hawataelewa chochote hapa.