Wanaume wazidi kuadimikia Wilayani Rombo

Wanaume wazidi kuadimikia Wilayani Rombo

Hbr za jioni Wapendwa wana JF wenzangu??,Nimekuwa nikisikia mara kadhaa kuwa Wilaya ya Rombo,mkoa wa Kilimanjaro kuna shida sana ya ulevi,hivyo kupelekea akina Baba kutowajibika vema ktk majukumu ya familia km Baba.

Leo katika kufuatilia kipindi cha RIPOTI MAALUMU kinacholetwa na ITV,nimeona jinsi ulevi ulivyokithiri huko Rombo ambapo akina mama wanalalamika kuwa Waume zao hawatimizi majukumu yao ktk familia,wamekuwa legelege,kazi za Kutumia nguvu hawawezi kuzifanya,Mama mmoja amesikika akisema kuwa hata mambo ya chumbani hawawezi tena (poor performance).

Mwanaume mmoja alipoulizwa kuhusu hali hiyo hususani kushindwa kuwahudumia wake zao Mambo ya ndoa,alijibu kuwa yeye hana muda wala interest na Mambo ya ndoa.

Bibi mmoja alipoulizwa kuhusu hali hiyo amesema anasikitika kwasababu kizazi hicho kinaelekea mwisho kwasababu Wanaume wanazidi kuisha huko Rombo hivyo itakuwa vigumu kupata watoto kutokana na ulevi uliopindukia.

Aidha Ktk mahojiano ya mwandishi na vijana wengi,imeonekana kuwa vijana wengi wa kiume wameachana na wake zao kutokana na ulevi hivyo Wanaume hao wanalelewa na mama zao, huku watoto wao wakiishi na wake zao.

My take: Vijana wa Kiume kutoka Mikoa mingine twendeni Rombo tukawasaidie Wanaume wenzetu walevi kuwahudumia wake zao ili kizazi cha Rombo kiwe endelevu.

Chanzo: RIPOTI MAALUMU-ITV
Mkuu, huko SI naskia Kuna scandal ya wanawake kuwaua wanaume zao, au tunaaminishwa na maneno ya Watanzania!
 
Ok.Wakija Bongo kwao Inakuwa kitonga.
Mimi mwenyewe kuna siku nilienda mpakani upande wa Kenya, nikaingia kwenye Bar zao nikanywa soda.

Walikuwa wanauza K50, ambayo kibongo wanakata zaidi ya 1,000 tulikunywa 2.

Tulivyowapa buku 10 ya kibongo, wakaturudishia Ksh350 ambayo tulipo chenji tukapa 7,000 ya kibongo.

Wakenya wakawa wanatushauri mngenunua Tanzania
 
afgasintani kuna frusa za wadada wenzetu rwanda wamepata warembo tayari tuangaike na rombo kweri huyu mama frusa zingine zinatupita hivihivi ana taka tubaki na hawa cheusi dawa wetu
 
Mkuu, huko SI naskia Kuna scandal ya wanawake kuwaua wanaume zao, au tunaaminishwa na maneno ya Watanzania!
Inawezekana ni kweli, unajua mtu akiwa amelewa ukimsukuma kidogo anaweza kuanguka vibaya hata kupelekea kifo?!!,Kwa hiyo inawezekana Wanawake wa Rombo huwa hawaui kwa makusudi bali ni hali inayojitokeza kutokana na Wanaume wao kuwa wameelemewa na ulevi.Mimi mwenyewe huwa nakwepa Sana kugombana na mlevi kwasababu najua nikimshindilia ngumi moja tu,anaweza kufa nami kujikuta naingia kwenye murder Case.
 
afgasintani kuna frusa za wadada wenzetu rwanda wamepata warembo tayari tuangaike na rombo kweri huyu mama frusa zingine zinatupita hivihivi ana taka tubaki na hawa cheusi dawa wetu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Inatakiwa tuenzi Cha kwetu.
 
Siku ITV wamekuja huku, hiyo ndio ilikuwa target yao walipita kwa DED akawaelekeza waje kwa WEO fulani hapa ambaye huko katani kwake ndio wanapika mpaka gongo akawapeleka huko wanakouza.

Ni kweli huku pombe inaliwa, ila wanaopata hasara ni wale ambao wamekuwa mateja wa pombe maana siyo kila mmoja anahimili.

Huku hakuna biashara nyingine ya maana sana zaidi ya pombe na kitimoto.
Aisee ITV wamenifungua macho sana, yaani Walevi wa huko Wana vituko balaa,Kwa kweli ROMBO kuna walevi balaa.
 
Mimi mwenyewe kuna siku nilienda mpakani upande wa Kenya, nikaingia kwenye Bar zao nikanywa soda.

Walikuwa wanauza K50, ambayo kibongo wanakata zaidi ya 1,000 tulikunywa 2.

Tulivyowapa buku 10 ya kibongo, wakaturudishia Ksh350 ambayo tulipo chenji tukapa 7,000 ya kibongo.

Wakenya wakawa wanatushauri mngenunua Tanzania
Kwenda huko Kenya unaruhusiwa hata km huna passport??.
 
Daaah wiki iliyopita niliona part one ya hiki kipindi wiki hii sijajua part two itakua lini
 
Unavuka tu border wala hawakuulizi chochote. Labda kama ukipanda gari kwenda huko mbele maana nasikia wanaweza kusimamisha gari kukagua documents.

Hapo mpakani hata ukivuka mpaka kilometer 3 hawaulizi
Mfano boda ya sirari unasafiri mpaka kisumu unapita migori sema huko mbeleni wanakuulizi ukikaribia kuingia nairobi
 
Mfano boda ya sirari unasafiri mpaka kisumu unapita migori sema huko mbeleni wanakuulizi ukikaribia kuingia nairobi
Kwa huku, kutokea Tarakea-Rombo mpaka Nairobi ni Ksh 600 ambayo ni kama Tsh 10,000.

Kenya Mirungi inaruhusiwa wakati kwa Tanzania ni haramu.

Kwahiyo wabongo watafuna mirungi wanaenda kutafunia kwenye Bar za Kenya kwa uhuru au wakinunua huku wanatafuna kwa kujificha ficha.
 
Mimi niko Rombo huku. In short ni kweli huku ulevi umekithiri.

Kila aina ya pombe unayoijua iko huku Rombo.

Huku kuna pombe ambazo huwezi kuzikuta sehemu nyingine.

Kuna bia za 500 mpaka 1,000.

Suala la wanaume kutohudumia familia zao binafsi nimeona ni kama utamaduni wa wachagga. Hata wanawake hawaweki akilini suala hilo kwamba atasaidiwa na mwanaume.

Huku wanawake wanapambana mpaka machinga mitaani kutembeza nguo na viatu.

Unaweza kukuta ndani ya nyumba wote hawaelewani.

Mama anauza duka lake, mtoto ana kigrocery cha bia hapo hapo na huku mzee wa familia yeye anuza mbege.

Nimegundua pia mchaga anakuheshimu kama una 'kitu'

Vile vile suala la unaguzi wa wachagga huwa ni hadi wao kwa wao huku.

Mfano leo nimekytana na baba mmoja mahakamani anashtakiana na mwanaye kwasababu ya shamba. Mzee anamwapia mabaya mpaka basi.

Mwisho kabisa, mademu wa Rombk ni wazuri ila nakuasa ninwa kupiga na kusepa kama unapenda kwenu na famikia yenu. Kaoe kwingine
Kuna mzee mmoja yuko huku niliko ni mchaga kastafu jeshi ila anavyoishi ni kma msela!

Yani mkewe yuko Moshi ila yeye yuko mkoa mwingine yani mwaka unapita hajaonana na mkewe na hana anachokifanya!
 
Back
Top Bottom