Wanaume wazidi kuadimikia Wilayani Rombo

Wanaume wazidi kuadimikia Wilayani Rombo

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
19,371
Reaction score
14,515
Hbr za jioni Wapendwa wana JF wenzangu??,Nimekuwa nikisikia mara kadhaa kuwa Wilaya ya Rombo,mkoa wa Kilimanjaro kuna shida sana ya ulevi,hivyo kupelekea akina Baba kutowajibika vema ktk majukumu ya familia km Baba.

Leo katika kufuatilia kipindi cha RIPOTI MAALUMU kinacholetwa na ITV,nimeona jinsi ulevi ulivyokithiri huko Rombo ambapo akina mama wanalalamika kuwa Waume zao hawatimizi majukumu yao ktk familia,wamekuwa legelege,kazi za Kutumia nguvu hawawezi kuzifanya,Mama mmoja amesikika akisema kuwa hata mambo ya chumbani hawawezi tena (poor performance).

Mwanaume mmoja alipoulizwa kuhusu hali hiyo hususani kushindwa kuwahudumia wake zao Mambo ya ndoa,alijibu kuwa yeye hana muda wala interest na Mambo ya ndoa.

Bibi mmoja alipoulizwa kuhusu hali hiyo amesema anasikitika kwasababu kizazi hicho kinaelekea mwisho kwasababu Wanaume wanazidi kuisha huko Rombo hivyo itakuwa vigumu kupata watoto kutokana na ulevi uliopindukia.

Aidha Ktk mahojiano ya mwandishi na vijana wengi,imeonekana kuwa vijana wengi wa kiume wameachana na wake zao kutokana na ulevi hivyo Wanaume hao wanalelewa na mama zao, huku watoto wao wakiishi na wake zao.

My take: Vijana wa Kiume kutoka Mikoa mingine twendeni Rombo tukawasaidie Wanaume wenzetu walevi kuwahudumia wake zao ili kizazi cha Rombo kiwe endelevu.

Chanzo: RIPOTI MAALUMU-ITV
 
Kwa ambao hamjui rombo ilipo. Ramani hii hapa.

wanaume wa kenya ndio watafaidi mizigo kutoka rombo

ni mbali kinyama

Screenshot_20210831-175533.png
 
Vijana wa Kiume kutoka Mikoa mingine twendeni Rombo tukawasaidie Wanaume wenzetu walevi kuwahudumia wake zao ili kizazi cha Rombo kiwe endelevu.

"umemalizia vizuri, sema umefichua siri mkuu. twende kimya kimya" sasa fanya kufuta hicho kipande mkuu
 
Mimi niko Rombo huku. In short ni kweli huku ulevi umekithiri.

Kila aina ya pombe unayoijua iko huku Rombo.

Huku kuna pombe ambazo huwezi kuzikuta sehemu nyingine.

Kuna bia za 500 mpaka 1,000.

Suala la wanaume kutohudumia familia zao binafsi nimeona ni kama utamaduni wa wachagga. Hata wanawake hawaweki akilini suala hilo kwamba atasaidiwa na mwanaume.

Huku wanawake wanapambana mpaka machinga mitaani kutembeza nguo na viatu.

Unaweza kukuta ndani ya nyumba wote hawaelewani.

Mama anauza duka lake, mtoto ana kigrocery cha bia hapo hapo na huku mzee wa familia yeye anuza mbege.

Nimegundua pia mchaga anakuheshimu kama una 'kitu'

Vile vile suala la unaguzi wa wachagga huwa ni hadi wao kwa wao huku.

Mfano leo nimekytana na baba mmoja mahakamani anashtakiana na mwanaye kwasababu ya shamba. Mzee anamwapia mabaya mpaka basi.

Mwisho kabisa, mademu wa Rombk ni wazuri ila nakuasa ninwa kupiga na kusepa kama unapenda kwenu na famikia yenu. Kaoe kwingine
 
Vijana wa Kiume kutoka Mikoa mingine twendeni Rombo tukawasaidie Wanaume wenzetu walevi kuwahudumia wake zao ili kizazi cha Rombo kiwe endelevu.

"umemalizia vizuri, sema umefichua siri mkuu. twende kimya kimya" sasa fanya kufuta hicho kipande mkuu
[emoji23][emoji23][emoji23],sawa Mkuu.
 
Mimi niko Rombo huku. In short ni kweli huku ulevi umekithiri.

Kila aina ya pombe unayoijua iko huku Rombo.

Huku kuna pombe ambazo huwezi kuzikuta sehemu nyingine.

Kuna bia za 500 mpaka 1,000.

Suala la wanaume kutohudumia familia zao binafsi nimeona ni kama utamaduni wa wachagga. Hata wanawake hawaweki akilini suala hilo kwamba atasaidiwa na mwanaume.

Unaweza kukuta ndani ya nyumba wote hawaelewani.

Mama anauza duka lake, mtoto ana kigricery cha bia hapo hapo na huku mzee wa familia yeye anuza mbege.

Nimegundua pia mchaga anakuheshimu kama una 'kitu'

Vile vile suala la unaguzi wa wachagga huwa ni hadi wao kwa wao huku.

Mfano leo nimekytana na baba mmoja mahakamani anashtakiana na mwanaye kwasababu ya shamba. Mzee anamwapia mabaya mpaka basi.

Mwisho kabisa, mademu wa Rombk ni wazuri ila nakuasa ninwa kupiga na kusepa kama unapenda kwenu na famikia yenu. Kaoe kwingine
Asante mkuu kwa kutuasa.Kwa hiyo sisi tunaotarajia kuacha mbegu huko unatushari Nini?.
 
Back
Top Bottom