Habari za usiku huu great thinkers
Leo nimekuja niwaulize ninyi wenzetu wa upande wa pili..... Mnataka nini? Maana kila analofanya mwanamke ninyi mnakosoa tuu...hamnaga jema. Nitatoa mifano michache....
Mwanamke akiamua kujitoa kwako akawa anakupikia,anakufulia na kukufanyia usafi mwingine mnamnanga eti hajitambui.....atajitoaje hivyo kwa mtu hajamtolea mahari. Ikitokea mwanamke akawa kauzu akasema well sitafanya chochote hata ningekuja geto nikakuta hakujafanyiwa usafi,una njaa au una nguo za kufua najifanya sioni naondoka kama nlivyokuja....mnahamaki na kudai et sio waifu material....
Mfano mwingine ni kwamba mpo kwenye mahusiano....huyu bidada anaamua kukupa vyote....hadi vile vinavyowahusu wanandoa bila hiyana...inageuka kuwa sababu ya kumshusha na kumwona hana msimamo.. Ikitokea akabana mnahamaki...ooh unataka kumuuzia nani mbuzi kwenye gunia...
Mengine mtaongezea
Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu....
My dia fanya kile moyo wako unapenda sio kufanya ili kuwapendeza hawa viumbe. Simamia kile unachokiamini na kama ukiamua kufanya jambo fanya kwa sababu unafurahia na sio kwa lengo la kum-impress mtu maana hata ikitokea ikawa ndivyo sivyo no regrets. Inaumiza sana kama ulikuwa unafanya jambo kwaajili ya kumfurahisha mtu na kumbe yeye anaitazama bidii yako in a negative way. Tulio wengi tuna imani zetu za kidini,wengine wana misimamo yao wao kama wao binafsi.....simamia hapo...
Ni hayo tu. Usiku mwema