Hawa ndio wanawake wetu wasomi, bado hatuelewi nini wanataka

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Wasaalam

Wakuu,

Leo asubuhi nilidamka mapema , wakati huu nilikuwa natoka kibaruani wakati najongea mdogo mdogo nyumbani nikapanda hewani nikampigia Mama, naam mama daVinci XV ,Nilimpgia asubuhi kwa sababu Mosi , ni Mila na Desturi zangu kumtaka hali kila uchao lakini pili nlitaka kuchota machache kuhusu siri nyingine zaidi na zaidi juu ya mwanamke ikiwemo yeye kuishi na Mzee wangu mpaka hivi sasa licha ya misuko suko ya ndoa na mahusiano.

Lakini Nikamuuliza pia kuhusu Mama mkubwa ambaye anaishi na Mzee wetu(bamkubwa) mpaka hivi sasa., nlimuuliza kuhusu mama mkubwa kwakuwa ni mwandani wa mama katika watoto wote wa Bibi yetu.

Kama ilivyo desturi ya Mama kuanza kunipa masomo kadhaa wa kadhaa juu ya mahusiano na maisha kwa ujumla huku Uvumilivu ikiwa silaha kubwa nayotakiwa kuishika mkononi na sio kuiweka mgongoni
Wakati wote Huu mama alikuwa na wasiwasi akidhani pengine nimekhitilafiana na mkamwanawe.(mpenzi wangu)

Baadaye nikarudi kulala nikijichekea nafsini mwangu kuhusu hii dunia yetu ya wanawake wasomi.

Ilikuwa hivi nilichukua uamuzi wa kumpandia hewani bi mkubwa kwanza hii ni desturi yangu kumtaka hali kila asubuhi kwakuwa tuko mikoa tofauti pili , ni kuongeza notes kidogo juu ya machache katika maisha hii ni desturi yake mama kutoa notes kila inapobidi.

Usiku wakati nipo shift ya Usiku , baada ya kumaliza majukumu yetu ya usiku , kwa kufanya medications na kufanya admission kadhaa na mengineyo yaliyotakiwa kufanywa., nlijongea taratibu kwenye kompyuta za Ofisi ili kupitia pitia kidogo yanayojiri katika ulimwengu wetu wa Urusi na Ukraine😅

Ni utaratibu wangu nikiwa night shift kusave bando langu na kutumia kompyuta za ofisi namaanisha simu itakaa kando kule.

WANAWAKE WASOMI
Pembeni kidogo walikuwa manesi (wote wanawake) ambao nlikuwa nao katika zamu ya usiku walishajitayarisha kwa ajili ya kupumzika, lakini walikuwa na stori chache kabla.

Mazungumzo yao yalikuwa ni matusi yanayofariji juu ya thamani ya wanaume kwa walezi huku wakisisitiza kuishi kama ma-single mothers .,huku mmoja akisimsititiza mwenzake zaidi.

Mie nikajifanya macho yangu yametaradadi na screen na nyoka EP ya jamal April lakini masikio na akili yangu bado vilikuwa juu ya maongezi ya wasomi hawa wawili., huu ni udodosaji ambao mwanaume sitakiwi kuufanya lakini masikio yaligoma kuisaliti mada hiyo iliyogusa vilivyo akili yangu.

Nikasema kutochukua notes chache kutoka hapo ingekuwa dhambi , dhambi nyeusi tii tii tii.

Huyu nesi mmoja ambaye alikuwa amezaa tayari alikuwa akimuelekeza mwenzie namna ya kuishi kama msomi (kwa mujibu wao)

Akawa anamuelimisha atafute mwanaume mwenye pesa tu azae nae kisha achukue mtoto wake,
yeye atulie tu na mtoto apambane naye hata akiachana nae iwe jukumu la mwanaume kama atahudumia au la asijishugulishe kuomba huduma ya mwanaume..lakini ni heri uzae na mwenye hela ili kama atakuwa na moyo wa kuhudumia mtoto wake basi mtoto apate huduma stahiki. Kuliko kuchagua hawa wanaume maskini wenzangu na mimi.

Akasisitiza mwanamke kutafuta pesa zake mwenyewe ili akomae kulea mtoto wake kuliko kufatisha Matakwa ya mwanaume., ambaye haeleweki mda wowote anaweza kukuacha hapa walisimamia wanaume wote ni sawa.,

Lakini hapa nikajiuliza kidogo mwanamke anataka nini zaidi?

hilo la kutafuta mwenyewe sawa tunalikubali , hatuhitaji mwanamke golikipa wa kusubiri kuletewa kila leo.

Lakini hili la kupigania usingle mother lilikuwa jambo jingine kwa hawa wasomi,

Ikanilazimu asubuhi kumuuliza bi mkubwa wangu kwa nini alidumu na mzee miaka yote. Akanimegea mengi. Kama ilivyo ada yake.

Lakini ukiachana na wanawake wa zamani kutokuwa na Elimu na kuwa wamama tu nyumbani nadhani kuna nyenzo nyingine iliyowafanya kudumu na waume zao hata sasa
Unadhani itakuwa nyenzo gani zaidi?
Hata hili naimani mama hakunichotea katika kile kitabu chake cha notes za siri za maisha.

Wanawake wetu wasomi wa sasa ambao pengine walitakiwa kuelimisha wengine juu ya namna ya kudumu na mwanaume ili kutoleta athari za mfarakano ambazo zinaweza kumjengea chuki mtoto juu ya mzazi wake mmoja.,ndiyo hao wanaopigania usingle mother. Wazae kisha wapambane na watoto wao wenyewe.

Huyu mtoto itamjengea picha gani kwa baba yake hapo badae CHUKI nyekundu isiyoweza kubadilika kuwa nyeupe kama ya mzee nasibu na yule dogo wa Tandale.

Maisha ya mahusiano na ndoa yana siri nyingi,, lakini kwanini wimbi la wanawake wengi hawa wasomi hivi sasa ndio wanapigania usingle mother ,PESA , au ELIMU?

Halafu cha ajabu hata wanaokwenda kwa wanasaikolojia kwa minajili ya kupata cancellin masingle mother wengi wasomi basi idadi yao ni Lukuki hivi sasa.

Elimu yao na kipato kidogo kinawafanya kuchagua kuwa masingle mother lakini hawana furaha na upendo kama wa mama zetu wa zamani ambao hawakuwa na Elimu wala vijisenti kama vya hawa wasomi wetu wa sasa.

Wanawake hawa ndio wanaongoza kuishi kwa visirani na sonona .

Wanawake wetu wanataka nini zaidi?
 
Wote hatuwezi jua wanawake wanataka nini ila, mwanamke akishakuwa na uhakika wa maisha yke bas huwa anakaa mbali na mwanaume anajitenga nasi wakiamini kwamba bila sisi wanaweza kuishi Tena kwa furaha zaid
Kabisaa mkuu ndiyo situation nliyokutana nayo kwa wasomi wale ...,
 
Huyo nesi aliyekua anamlisha sumu mwenzie..ni kwamba yeye aliingiaa chaka bovu..ss anajaribu kumdanganya na mwenzie asikubali kuolewa wakati ndoa haziko sawa...HIYO NI SUMU MBAYA SANA ANAMLISHA na kumpotosha...

Ila nikwambie deep down huyo nesi alitamani na yeye awekwe ndani..hakuna mwanamke hapendi kuhudumiwa kutunzwa au hata kupendwa...never....
Wengi wanaokimbilia kujizalia tu ni walishaktaaa tamaa anaona bora apaate watoto basi alee..maana ukute kwa tabia zake au sababu zingine zingine watu wanamkimbia......

Alichokua anamshauri mwenzie ni kumharibu na km ni bint mdogo basi anamshawishi adange mpk apate bwana mwenye hela amtegeshee mimba azae...haya atazaa na wangapi....stupid mind set

Usinglr mother unatakiwa uje tu automatically kwa mipango ya Mungu sababu sio kila mtu anapenda kutelekezwa

Ila huo usingle mother wakujitakia ni uboya...

Wazazi wetu wamedumu sababu walijua kuvumiliana ..kizaz chetu si wanaume wala wanawake wanaweza kuvumiliana..kosa kidgo kashaondoka kwao..kosa kidgo keshafukuza mke kaoa mwingine...

Ila wazaz qwtu walijikaza....angalia familia ambazo wazaz wamelea wawili..watoto angalau wanastawi...lkn familia nyingi ambazo zina talaka u akuta kidg ht malezi na tabia za watoto zinayumbA

Sasa nawaza sisi kizaz cha wasomi..miaka ijayo wToto wetu hawa sijui watakuaje..Mungu atusaidie

Mimi huwa namuomba Mungu anisaidie nilee watoto wangu kama nilivyolelewa mimi na wazaz wangu..angalau tu nitengeneze kiazaz chenye staha.na malezi mazuri (kifupi wanangu wawe kama mimi).
Nisingetaman wawe tofauti...kisa tu wazaz tuko busy ..kukosa upendo etc etc
 
Wengi wa wanawake wasomi wanataka uhuru na usawa, ambavyo vinawezekana kikamilifu wakiwa ma-single.
Ile kanuni ya asili, sawa na maandiko, ya KUTAWALIWA na mume wanaona ni kero..

Mwanzo 3:16
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
 
Daaah shukraaani mkuu, sana hapa nimeongeza kitu
 
Wengi wa wanawake wasomi wanataka uhuru na usawa, ambavyo vinawezekana kikamilifu wakiwa ma-single.
Ile kanuni ya asili, sawa na maandiko, ya KUTAWALIWA na mume wanaona ni kero..

Mwanzo 3:16
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Sahihi kabisaa mkuu,
 
Back
Top Bottom