"tangu nimzae mtoto wangu sinahamu kabisa na mumewangu sijawahi pata raha ya tendo la ndoa"
Kama mwanamke hapati raha ya tendo la ndoa, tatizo ni la nani? Hisia zake kwa mwanaume wake zimepungua?
Kwanini zipungue baada ya kuzaa?
Mwanamke tayari ashajiaminisha hapati raha wakati wa tendo, moja kwa moja inaonyesha anafanya tu pasipo hisia na hii performance lazima iwe ya kawaida kabisa. Na labda huwa anamuwekea tu aingize ili tu mwanaume afike kisha kazi kwisha.
Kwa hali hiyo unategemea huyo mwanaume asichepuke?
Huyo mwanamke yeye anaishi vipi tendo miaka zaidi ya nane halifurahii?
Umemuuliza kama anayo alternative ya kukidhi hitaji hilo ipasavyo?
Huo ni upande wa mwanamke, upande wa mwanaume hatujahusikia kujua nini kinamsibu kumhusu mwanamke.
Kuwa na mali na pesa ni tofauti kabisa na kuwa na Furaha, hili lazima litambulike.
Furaha huletwa na mambo mbalimbali katika maisha ambavyo mara nyingi siyo kuwepo kwa mali wala pesa.
Next time usilinganishe furaha ya mtu na mali alizonazo. HAKUNA UHALISIA WA UWIANO.
Usihukumu kwa kusikiliza upande mmoja. Pata muda kusikiliza na upande wa pili.
Hapa hakuna balance na atatupiwa lawama mmoja bila kufikiri upande wa pili.