Wanaume waliotaka kunioa nikakataa hawa hapa

Wanaume waliotaka kunioa nikakataa hawa hapa

sio kwamba sipendi kuolewa jamani au sio kwamba sijawai kupata wa kunioa , ila yaani waoaji wangu sijui nisemeje .ngoja niseme kwa ufupi muamue wenyewe

muoaji namba moja
huyu jamaa kweli kabisa alitaka kuniweka ndani hata sasa hivi nikitaka ila story yake ipo hivi
huyu jamaa ni rafiki yake na boss wangu . wanafanya biashara zingine pamoja.wanajuana miaka na miaka .alinijulia ofsini pia boss wangu akawa anamwambia bwana miss yupo fresh muoe huyu .jamaa alishaoa sema mke akaondoka na alishaolewa na jamaa mwingine ana mtoto mmoja . na ni muhenga tu fresh ambazo ndo flavour zangu..jamaa akanitongoza kweli nikakubali .tukaanza mahusiano.kusema kweli sijawai kumpenda hata sema nikawa nalazimisha tu niolewe yaishe. maana ana nyumba ana gari yupo fresh .nilipanga nitampendea mbele ya safari
siku moja akanialika home kwake nikalale huko .sikuwai kufika kwake , usiku mmoja huo nikaenda kwake ilikuwa ijumaa nikashuka kituoni akaja na gari tukaingia mtaani hadi kwake ni jirani na huyo boss wangu japo yeye haishi hapo anakaa nje ya nchi anakujaga tu mara chache.ndo maana nilienda usiku.
nyumba ilikuwa nzuri saaana kwa nje nikasema mama mwenye nyumba mimi Mungu anipe nini tena jomonii?
haya nikashuka kwenye gari mlango ukafunguliwa nikaingia ndani .mama weeeeeeeeeeeee
Yaani palikuwa pachaaaafu pachafu .yaani jamani mimi sio msafi wala msidhanishie nina dharau ,am the coolest person ever! Yaani sofa ni chaafu zimechooka yaani hata panya haishi mle.nikatoa khanga yangu kwenye pochi nikatandika nikakaa huku full chafya *****.

Mdogo wake wa kiume alikuwa anaandaa msosi nikamwambia nikusaidie akasema poa yaani jikoni nilivofika na navopenda msosi apetite ilikata toka siku ile mpaka kesho jomoni . in short that house was hell men

Chumbani sasa.
Chumbani sasa. Yaani nguo zote zimetundikwa kwenye kitanda yaani masuruali mengine yamefuliwa mabichi ,maana kilikuwa kipindi cha mvua, yaani hakuna hewa kusema kweli. Nikamwambia bwana hee twende tukalale kwangu hapa mbu hivi pia nina pumu nitakufa humu . japo sina pumu nilidanganya.

Tukaondoka usiku huo hadi kwangu saa saba hiyo
Hapo nimeshikwashikwa hadi basi nimekereka wee
Pole sana dadangu. Kama humpendi huyo mwanaume nakushauri usiolewe naye. Maana kwenye ndoa ni kifungo kibaya sana, sasa ukifungwa na mtu usiempenda hautakuwa na furaha kamwe. Uchafu. Mwanaume akishaoa na akaishi na mwanamke halafu akaachwa huwa hiyo ni hali ya kawaida kabisa hivyo kama upo serious kuolewa naye wewe ndo wajibu wako kumshugulikia mpaka awe masafi. Tena hapo ndo chukua credit kabisa anza purukushani mapemaaaaaa
 
wewe unatafuta excuse baada ya kuona ndoa zimekaza awamu hii, kama alikua mchafu wewe ulikua na nafasi ya kumbadilisha tena ndani ya wiki tu.

tulieni story haijaisha mbona mnanihukumu?
Ila kuna wanaume ni wasafi jamaaaani, usiombe!!!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] we miss una mambo sanaa..vituko havikuishi
 
wewe unatafuta excuse baada ya kuona ndoa zimekaza awamu hii, kama alikua mchafu wewe ulikua na nafasi ya kumbadilisha tena ndani ya wiki tu.
wewe kama hutaki kunioa waoaji wapo bna wewe tulia nikupe story
 
Back
Top Bottom