Wanaume waficha Wallet/pesa wakifika home.why?

Kuna harusi ya bestie yangu nilihidhuria kama miaka mitatu iliyopita, ukafika wakati baba kutoa mawaidaha, akamwambia mwanangu ni marufuku kuchungulia mfuko wa suruali ya mume wako au wallet au briefcase. huyu mzee alikuwa anajua maumivu ya roho unayoweza kuyapata mtu pale unapoangalia mfuko wa mwenzako umejaa halafu unapotoa list ya matumizi unapewa kiasi kisichofika hata robo ya kile ulichohitaji na hapa naongelea matumizi muhimu.

Siku hizi wanawake wengi sana wanalalamika waume zao hawatekelezi majukumu yao, Matumizi ya nyumbani kama chakula, kodi ya nyumba, nishati nk ni kama kero kwao. unaweza ukamwambia mtu gesi imeisha jibu utakalopata kwanini msitumie mkaa au mbona gesi imeisha haraka hivyo au mnapikaga nini na hiyo gesi wakati hakuna siku imepita hajala milo si chini ya mitatu kwenye hiyo nyumba. na gesi medunda nayo miezi miwili.

Kwa ujumla wanaume wengi siku hizi are running away from thier responsibilities. Hata kama mke anafanya kazi ni muhimu sana mkakaa mkapanga mipango yenu nasidhani kama mama atadai fedha kama anajua ni za shughuli fulani
 
Ndoa zina mambo mengi sana na kila walio ndani ya ndoa wakianza kusimulia humu JF bila shaka nywele zitasisimka,mi naona tuyaache hivo hivo mradi siku zinaenda watoto wanakua basi.Tusichokonoe sana undani wa ndoa maana tukifanya hivyo si ajabu wengi wa wanaJF ambao hawajaoa/kuolewa wanaweza waogope kutia mguu Kanisani/Msikitini!
 
Wanawake wengine ni MCHWA... wakiziona tu umeliwa utasikia hamna hiki, hamna kile mambo lukuki

Ila aspirin na utenzi wako wewe ni noma!
 
Eee Mungu nisaidie nipate garrrrrr,
Niweze ficha hela kwenye garrrrrr,
Manake waifu hana mamlaka na langu garrrrr,
Tunanyanyapaliwa si tusio na magarrrr,

Garrrrrr garrrrrrr garrrrrr garrr yangu.
Nakupenda sana garrr,
sina hela ya kununua garrrr,
naficha hela ili ninunue garrrrr,
Halafu nifiche hela kwenye garrrr.....

Wanawake wengine ni MCHWA... wakiziona tu umeliwa utasikia hamna hiki, hamna kile mambo lukuki

Ila aspirin na utenzi wako wewe ni noma!

Hahahaa...si unajua swahiba, sisi tusio na magari basi tabu tupu?

hatujui bei ya mafuta...............

Wala kupanda matuta,
Nauli twaitafuta,
Tusijepata matata,
Pesa hiyo twatafuta,
magari tutayapata

Na pa hela kuificha..........
 
Mmmh,

wamama wengine wa kichaga hawafai. Huo bwana lazima mke wakke mchaga

Hivi Karibuni kuna baba mmoja miaka sitini, alishanga watoto wanamweleza baba yao kuwa Mama kaenda kufungua nyumba yake huko Marangu Mtoni huku amemwaga mume wake kuwa anaenda kumwona mama yake mgonjwa. ndipo aliamua kumfuata nyumba. Lahaula kuja kufika nyumbani anakuta sherehe moja kubwa.

Mwanaume yeye alijua tu aaaamwwanamke anabwana mwingine aliyempa hizo pesa hivyo akamwacha mke, lakini ukweli ni kwamba mwanamke alikuwa akimwibia Mume wake kidogokidogo kiasi kwamba hakutambua kama anaibiwa. Fikiri katika umri wa miaka sitini kuachana kwa sababu hiyo

live story
 
Mmmmmm!!! haya maneno makali kidogo. Kama upo kwenye ndoa basi mshukuru mungu kwa uliyempata kama bado basi maneno kama haya usiyatumie tena. Maisha ya ndoa yana changamoto nyingi sana kwani mmekutana mkiwa watu wazima ambao mmelelewa katika mzingira tofauti. Pia kumbuka maisha ya uchumba yanatofauti kubwa sana na maisha ya ndoa, endapo utakuwa ndani ya ndoa utafahamu ninayo yasema japo si lazima utakayokutana nayo wewe na mwenzako atakutana nayo, kila mtu anakutana na vituko tofauti kwenye maisha ya ndoa. La msingi endapo utakutana na changamoto yeyote jaribu kukaa na mwenzako ili muweze kuweka mambo sawa.

kapos kama izi wanakuwa wameopoana kwenye baa ama!?
Spati picha aisee.
 
Kuna harusi ya bestie yangu nilihidhuria kama miaka mitatu iliyopita, ukafika wakati baba kutoa mawaidaha, akamwambia mwanangu ni marufuku kuchungulia mfuko wa suruali ya mume wako au wallet au briefcase. huyu mzee alikuwa anajua maumivu ya roho unayoweza kuyapata mtu pale unapoangalia mfuko wa mwenzako umejaa halafu unapotoa list ya matumizi unapewa kiasi kisichofika hata robo ya kile ulichohitaji na hapa naongelea matumizi muhimu.

Siku hizi wanawake wengi sana wanalalamika waume zao hawatekelezi majukumu yao, Matumizi ya nyumbani kama chakula, kodi ya nyumba, nishati nk ni kama kero kwao. unaweza ukamwambia mtu gesi imeisha jibu utakalopata kwanini msitumie mkaa au mbona gesi imeisha haraka hivyo au mnapikaga nini na hiyo gesi wakati hakuna siku imepita hajala milo si chini ya mitatu kwenye hiyo nyumba. na gesi medunda nayo miezi miwili.

Kwa ujumla wanaume wengi siku hizi are running away from thier responsibilities. Hata kama mke anafanya kazi ni muhimu sana mkakaa mkapanga mipango yenu nasidhani kama mama atadai fedha kama anajua ni za shughuli fulani
this is very true. wanaume siku hizi wanakimbia sana majukumu yao, mwisho wake wanaishia kuficha pesa kisa wasiombwe. sijui wanataka nani awatunzie wake zao na watoto zao. Ifikie mahal;i watambue wanapoamua kuoa inamaanisha wana uwezo wa kutunza familia, si kuleta pressure za roho, unaweza kuta nyumbani anabana na kuficha, ila huko nje anatumia hadi watu wawnamshangaa. shame.
 
Ila kweli jf inatuonyesha mengi. Ni kweli wapo wanawake wanafanya kazi ila wanataka hela ya mume ndo itumike. Mi na mke wangu wote tunafanya kazi, mshahara ukitoka tunaweka mezan tunapanga cha kufanya. Ingawa nazingatia mwanamke ni delicate na anahitaji vitu ving kuliko mimi na maswala ya urembo pia si una jua. Kwa hiyo unakuta maisha bomba kabisa. Tetesi, kuna wake wengine utakuta mnapeana hela ya matumiz pa day, sasa unakuta ukirudi unaulizwa hela imebaki shingapi na umetumia kununua nini na nini, change iliyobaki ananyang'anya au anasearch mifukon. Nafikiri ndo maana wanaume wengi wanaficha hela kama alivyoeleza dada hapo juu.
 
Eee Mungu nisaidie nipate garrrrrr,
Niweze ficha hela kwenye garrrrrr,
Manake waifu hana mamlaka na langu garrrrr,
Tunanyanyapaliwa si tusio na magarrrr,

Garrrrrr garrrrrrr garrrrrr garrr yangu.
Nakupenda sana garrr,
sina hela ya kununua garrrr,
naficha hela ili ninunue garrrrr,
Halafu nifiche hela kwenye garrrr.....
:lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol: Duh Big brother you just made my day..........Hii kali sana au valuer nini zinaongea hapa................dah yaani nimecheka hadi nimetoa machozi
 
Leo kabla sijarudi home nilikaa na marafiki kama sita mahala kupoteza muda ,kuna mmoja wetu akasema mume wake kila akifika home anamwangalia kama mkewe kalala na yeye anajifanya kalala. kwa vile giza anamwona mumewe anahangaika kuficha wallet hadi sometimes chini ya kapet, chooni na wakati mwingine chini ya kitanda.

wakiamka asubuhi mke anamwambia mumewe kuna vitu vinahitajika kununua mume anamwoshesha kwenye dressing table kwamba ana kiasi kile tu anachokiona, wakati mwingine akirudi na akianza kukoroma yule dada anaangalia kule alikoficha anakuta anazo pesa, then anaacha vilevile,akiamka akimwambia majukumu majibu ni yaleyale kujifanya hana pesa wakati anazo.

Mimi niliona kitu cha ajabu sababu unafichaje halafu chumbani, kwa nini usiache kwa gari au ofisini.Wadada wawili walimuunga mkono wakasema ni kweli wanaume wengine wanatabia hiyo hadi mmoja wao aliamua kumfundisha adabu mumewe alipoficha tu yeye akachukua zote kulipokucha wanaenda kazini anamwona anatafuta akauchuna hadi jioni ndio alimrudishia na kumwambia amwamini asiwe anafichaficha pesa au wallet
sasa swali langu kwa wanaume wa jf ni kweli huwa mnafanya hivyo? na mnafanya kwa manufaa ya nani?Ni nini kinapelekea mtu kuamua kufichaficha kihivyo
Hii ni Mpya, maficho mpaka chumbani .
 
mhh mzee mbona umechukua neno moja ume conclude kabisa na kutukana? hatari hiyo Yo Yo!!
HAMNA BANA.....mitanzania inakera bana.....jitu lapanga toka kwake kuja kuweka thread kama hizi.......hv hizi zinasaidia nini?

...hamna mambo mengine mjifunze?
 
Afadhali cc tunaficha fedha na tunahudumia familia, fedha ya mwanamke ukiiona siku hiyo ufanye sherehe.

kama unajijua unahudumia familia vizuri kwa nini ufiche?
Hamna lolote, mnaficha ili mkwepe kugharamia baadhi ya mahitaji.
Tabia mbaya hiyo.
 
HAMNA BANA.....mitanzania inakera bana.....jitu lapanga toka kwake kuja kuweka thread kama hizi.......hv hizi zinasaidia nini?

...hamna mambo mengine mjifunze?
wewe ndio unakera umeona post ina nyota ngapi ila inaonekana siri yako imefichuka pole mwaego, acha kuficha wallet yako! na wenzio sio tunapanga tangu kwetu tunatembea nazo laptop na mobile ukitaka pole secretary
 
HAMNA BANA.....mitanzania inakera bana.....jitu lapanga toka kwake kuja kuweka thread kama hizi.......hv hizi zinasaidia nini?

...hamna mambo mengine mjifunze?
Mambo mengine kama yapi kaka!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom